Miaka 50 ya BAKWATA: Rais Magufuli achangia TZS Mil 30, asema mali za Waislam zirudishwe kwa Waislam

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,057
10,715
Karibuni wadau tupate nasaha za viongozi wetu wa dini na Taifa.

Viongozi waalikwa ni pamoja na:
- Makamu wa Raisi mama Samia.
- Jaji mkuu
- Rc Makonda

Updates.........

KATIBU MKUU.

- Anasoma taarifa ya kazi ya BAKWATA, kiutendaji, kijamii, kiuchumi nakadhalika.

MHESHIMIWA MUFTI ZUBERI.

- Anashukuru kwa viongozi kuitika wito.

- BAKWATA imetimiza miaka 50 toka ianzishwe mwaka 1968.

- Anamuomba Waziri mkuu ataoe neno kwanza kisha makamu wa raisi na badae ataendelea kumkaribisha Mheshimiwa Raisi

WAZIRI MKUU

- Anapongeza wazo la kuanzisha maadhimisho kama haya.

- Dini taasisi muhimu kwani zinawajenga na kuwaandaa watu wetu kuwa raia wema nchi iwe na amani, utulivu na mshikamano. Dini pia zinachangia sana kutoa huduma mbalimbali za jamii nchini kama za kielimu, afya na maji. Tunawashukuru sana viongozi wa dini. Anapongeza pia uongozi wa BAKWATA kumaliza migogoro ya kidini misikitini.

- Anamkaribisha Makamu wa Rais.

MAKAMU YA RAIS.

- Tuna mipango mizuri ili hatuna budi kuhakikisha tuna BAKWATA moja ili tufanikiwe.

MUFTI (Anaendelea))

- Anashukuru kwa jitahada za Raisi zilizowezesha ufadhili wa ujenzi wa msikiti wa kinondoni toka Falme ya Morocco.

- Anashukuru mali za waislam kurejeshwa na serikali.

- Anamkaribisha Rais aongee.

RAIS MAGUFULI

- Anashukuru kwa mwaliko

- Serikali ninayoiongoza tutasimama na waislam na dini nyingine zote na hata wasiokuwa na dini.

- Nawashukuru pia Waislam kwa kura mlizonipa.

- Miaka 50 ni mingi na natambua mmfanya mengi ikiwamo kulinda umoja.

- Katika kipindo hicho mmchangia pakubwa maendeleo ya nchi hii, mmetaja huduma za shule, afya, huduma za kijamii nakadhalika.

- Ombi langu kwenu tuendelee kutunza amani na mafundisho ya mitume wetu. - Kinachotuletea matatizo wakati mwingi ni migogoro. Tujitahidi kuepuka migogoro. Mimi naamini Mungu wetu ni mmoja na hivyo tushikamane.

- Kuhusu mali za waislam niliagiza viongozi wote wahusika wahakakikishe zimerudi kwa waislam. Naomba waislam wote wahakikishe mali hizo hazirudi tena kule zilizokopotezwa. Najua walionyanganya mali hizo wamekasirika. Kikubwa nawaomba mniombee kwa Mola.

- Tunaendelea na mipango mbalimbali ya kuleta maendeleo ya nchi yetu, elimu bure, reli ya umeme, kununua ndege tisa, tunajenga bwawa kubwa la umeme, tunafufua reli kwenda arusha, barabara bagamoyo tanga, nyakanazi, kufunga umeme maeneo mengi, kuongeza bajeti ya afya n.k.

- Fedha za kufanya hayo tumezipata kwa kubana mafisadi na kuzuia watumishi hewa. - Tuna wajibu wa kujenga taifa letu.

- Nakupongeza sana Mufti, wewe ni mtu wa tofauti sana. Nakumbuka nilipokuwa msibani kwa Mzee Kikwete nilikuona ukiwa kaburini unachimbua udongo. Hakika sijapata kuona mfano huo kwa kiongozi mkubwa kama wewe. Hujikwezi, hujioni, unaheshimu kila mtu.

- Nakubaliana na Mheshimiwa waziri mkuu, kuwa maadhimisho haya yasisubiri miaka 50.

- Nimekuja na hela kidogo shilingi milioni 30 mtapanga wenyewe mtakavyozitumia iwe kwa maendeleo yenu au kunywa soda.
Anakabidhi kitika kwa Mufti

AMEMALIZA.


Habari zaidi..


Rais John Magufuli amehudhuria kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzani (BAKWATA) yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

UPDATES

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

“Leo hii kwetu ni siku muhimu sana kwasababu ya kumpata kiongozi wetu rais Magufuli kwani ana majukumu mengi lakini tumepata bahati ameungana nasi,”- Waziri Mkuu Kassim majaliwa

“Namshukuru Mufti Mkuu kwa kubuni siku ya leo ambayo imetuunganisha waislamu wote na ninadhani jambo hili lisiwe miaka hamsini tu maana wengine tunaweza tusiikute angalau tuwe na siku moja kila mwaka itakayotukutanisha waislamu wote,”- Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

“Dini zetu hapa nchini kwetu kama serikali ni taasisi muhimu sana kwani zinasaidia kuwajenga watu katika maadili mema na waislamu kazi hiyo wanaifanya vizuri sana,”- Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

“Utulivu tulionao leo nchini unatokana na mchango wa dini zetu kwa kusaidia kutangaza amani na kuhamasisha watu kwa wamoja na ndio maana leo tunaringa kuwa na amani na mshikamano,”- Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

“Dini zetu zinatoa sana huduma za maji katika taasisi za shule na afya kwa kuchimba visima na kutatua shida hiyo na sisi tunawashukuru sana kwa kuunga mkono jitihada za serikali,”- Waziri Mkuu Kassim Mjaliwa

“Mufti wetu toka ameingia madarakani leo ana miaka mitatu na mimi ninaridhishwa na uongozi wa Bwakwata tumeshuhudia ndani ya miaka hiyo migogoro imekwisha kabisa katika misikiti yetu,”- Waziri Mkuu Kassim Mjaliwa

“Ninawaahidi kuwa tutaendelea kuwaunga mkoni ili kuhakikisha shughuli zote zinaenda vizuri zikiwemo za Bakwata,”- Waziri Mkuu Kassim Mjaliwa

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU

“Wakati kaimu katibu Mkuu wa Bwakata alipokuwa akisoma ripoti nimeona mipango mingi ya baadae na ninamuomba Mungu itimie lakini haitaweza kutimia iwapo hatutaacha mazoea ya nyuma na kuiunga mkono Bakwata ya sasa,”- Makamu wa rais Samia Suluhu

RAIS MAGUFULI

“Leo tumeanza vikao vya kamati kuu kwa muda wa siku tatu lakini nilimueleza Mufti kutokana na heshima niliyonayo kwa viongozi wa dini ni lazima nishiriki katika hafla hii ndio maana ilibidi tukabadilishe nguo zetu za kijani tusije tukawakwaza viongozi wetu,”

“Serikali ninayoiongoza siku zote tutasimama pamoja na waislamu, wakristu na hata wale wasiokuwa na dini ili kuifikisha nchi yetu katika sehemu nzuri,”

“Ombi langu kwenu tuendelee kudumisha umoja wetu na kudumisha amani yetu huku tukiendelea kufuata mafundisho yote ya mtume wetu na kinachotukwamisha ni mogogoro na ninauhakika huwa inaletwa na shetani hivyo hatuna budi kusimama imara,”

“Serikali ninayoiongoza inapenda madhehebu yote na ndio maana alipokuja Mfalme wa Moroco nilimuomba ajenge Msikiti Mkubwa sana Tanzania sikumuomba Kanisa najua watu wengine watashangaa ni kwanini lakini mimi ninaamini Mungu wetu ni mmoja,”

“zipo mali za waislamu zilizochukuliwa na nimeanza kushugulikia tangu niko Waziri wa ardhi nilikutana na Shekhe Mkuu wakati huo kuzungumza nae kuhusu suala hilo na nilichokigundua wakati ule waliohusika kuzigawa ni waislamu wenyewe,

"Baada ya kusoma document nyingi nilichogundua waliohusika kuuza mali za Waislamu ni Waislamu wenyewe"

“Mufti Zubeir alinifuata na kuniambia kuwa wakati ule ulishindwa lakini tunaomba utusaidie maana mwenye mamlaka ya ardhi ni rais na aliniambia huku amenikazia jicho ndipo nilipoona kuwa Bakwata wamepata kiongozi,”

“Zile mali zilizokuwa ngumu kurudisha nimezifuta na ndio maana Mufti amesema mali zimeanza kurudi hivyo ninawaomba msije mkazirudisha kule zilikotoka,”

“Mpaka sasa uchumi wa nchi yetu uko juu na tunayafanya haya sisi kama viongozi wenu kwa manufaa ya watanzania wote, katika kufanya mema lazima utapingwa na ndio maana tunaomba mtuombee kwa Mwenyezi Mungu ili hizi ndoto ziweze kutimia,”

“Ninataka niwaambie tumepata wapi fedha za kukamilisha mambo yote tuliyoyafanya kwani zilikuwa zinapotelea kwenye mikono ya watu wachache na hivyo tukaamua kuwabana mafisadi,”

“Wakati Mzee Kikwete amepata msiba kule Msoga nilienda kumpa pole wakati wanachimba kaburi nilimuona Mufti Aboubakar Zubeir anatoa udongo kaburini nilimuona ni mtu wa pekee maana sijawahi kumuona padre wala mchungaji anafanya hivyo ,”

“Mufti Katika kipindi chako cha uongzi wa miaka mitatu umewaunganisha watanzania na inawezekana leo wasione lakini ukifa watasema hawajawahi kumuona Mufti kama wewe kwani haujikwezi, umetanguzliza maandiko na Mungu mbele,”

“Tusisubiri hadi miaka hamsini mingine maana wengi hatutakuwepo sasa ni vizuri tukapanga muda mfupimfupi ili tuwe tunakutana na kupanga mipango ya baadae,”

“Nimeona nije na fedha kidogo kiasi cha shilingi milioni thelathini nitakukabidhi Mufti muone jinsi mtakavyofanya mtamua wenyewe jinsi mtakavyozipangia matumizi,”
 
Kupitia kituo namba moja cha habari nchini TBC ,
Magufuli ni mgeni rasmi katika maadhimisho miaka 50 ya Bakwata,
Bila shaka rais atawajibu mashoga kwa kupitia vifungu vya dini,
Makonda kamaliza kuongea
Endelea kubaki hapahapa kupata kile kinachojiri
UPDATES
Waziri mkuu Kassim Majaliwa anatoa salam
Magufuli anaongea
Magufuli anatoa mchango wake kidogo wa milioni 30 kwa ndugu zake waislamu,naamu wanamshukuru kabisa
TAKBIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIR
Magufuli anasomewa dua maalumu ya kumlinda na mabeberu na walinda mafisadi nchini
 
Kupitia kituo namba moja cha habari nchini TBC ,
Magufuli ni mgeni rasmi katika maadhimisho miaka 50 ya Bakwata,
Bila shaka rais atawajibu mashoga kwa kupitia vifungu vya dini,
Makonda kamaliza kuongea
Endelea kubaki hapahapa kupata kile kinachojiri
Rais atawajibu mashoga kuhusu nini?
 
Kupitia kituo namba moja cha habari nchini TBC ,
Magufuli ni mgeni rasmi katika maadhimisho miaka 50 ya Bakwata,
Bila shaka rais atawajibu mashoga kwa kupitia vifungu vya dini,
Makonda kamaliza kuongea
Endelea kubaki hapahapa kupata kile kinachojiri

Angalau kidogo Taarifa umetulia na umejitahidi kuiandika vizuri na kueleweka haraka na siyo ile nyingine ambayo ' ulipopomika ' mno.
 
1545054841447.jpeg


Atazungumzia kuhusu hao?👆🏾
 
Karibuni wadau tupate nasaha za viongozi wetu wa dini na Taifa.

Viongozi waalikwa ni pamoja na:
- Makamu wa Raisi mama Samia.
- Jaji mkuu
- Rc Makonda

Ni matumaini yangu baada ya hapo basi mara moja tutaona Maisha ya Mtanzania yanaanza kubadilika hasa wale Ndugu zetu ' Wakulima ' waliopo huko Vijijini huku tatizo Kubwa la Watanzania wengi kutokuwa na Ajira / Kazi sasa nalo likibadilika kwani naamini hao Viongozi wa Dini wote waliopo hapo wakiomba Kwake Maualana / Mola mambo yanaweza kuanza kubadilika.
 
Mambo yabadilike?
Jiwe doesn't give shit what kind of god created him
Ni matumaini yangu baada ya hapo basi mara moja tutaona Maisha ya Mtanzania yanaanza kubadilika hasa wale Ndugu zetu ' Wakulima ' waliopo huko Vijijini huku tatizo Kubwa la Watanzania wengi kutokuwa na Ajira / Kazi sasa nalo likibadilika kwani naamini hao Viongozi wa Dini wote waliopo hapo wakiomba Kwake Maualana / Mola mambo yanaweza kuanza kubadilika.
 
Nipo hapa live namsubiria aongee.....!! Nadhani pia atagusia suala la hao mabeberu, lazima tu atajibu hoja, japo sio rasmi.
 
Back
Top Bottom