Miaka 50 uhuru: Zile siri kuu [confidential] za kiasiasa zenye umri wa miaka 25 na zaidi zifunguliwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 50 uhuru: Zile siri kuu [confidential] za kiasiasa zenye umri wa miaka 25 na zaidi zifunguliwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DSN, Dec 3, 2011.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Jamii inapoishi kama jamii,familia,kikundi,kabila,Taifa kuna migongano na maelewano.Hivyo kutokana na migongango na maelewamo hayo uzaliwa dhana mpya na hivyo kuibua hatua nyingine ya maendeleo katika jamii husika,dhana hiyo katika migongano, kutofautina au kuelewana ikiwa wazi uitwa mwafaka au makubaliano na dhana hiyo hoyo ikifichwa uitwa SIRI.

  Kwa Mataifa yaliyoendelea Mataifa hayo ukaa na SIRI miaka 25 kisha baada ya hapo iliyokuwa inaitwa SIRI ufunguka na kuwa wazi kwa umma,na kwa watu wengine kizazi cha zamani na kipya ujifunza kupitia SIRI hiyo au kwa kuitengenezea sinema, tamthiria au kuitungia kitabu ambacho uigeuza SIRI ile kuwa ni funzo na sehemu ya jamii mpya.

  Kwa miaka yetu hamsini ya uhuru Tanzania tumepiga hatua japo kwa wengine ambao pia wanaona vingine kwa jicho pana kuwa tungekuwa tumepiga hatua kwa mbali sana kulinganisha hapa tulivyo sasa kwa kuwa tuna rasilimali na rasilimali watu wengi sana.Hivyo kasi ya kukua kwetu na kasi ya tuliyonayo katika kukua huko kimaendeleo vinatofautina sana.

  Hivyo naona ni wakati sahihi kwa watu makini,waelevu na wenye busara,miaka hamsini ya uhuru ni mingi sana,kama ni mtu mzima anawajukuu wenye umri wa miaka mitatu mpaka mitano sasa.Kwa Mantiki hiyo SIRI KUU [CONFIDENTIAL] ZA SERIKALI ZENYE MARKA UMRI WA MIAKA 25 NA ZAIDI MPAKA 50, ZIWEKWE HURU JAMII IJIFUNZE KUPITIA SIRI HIZO.

  Hivyo kuna mambo ambayo siku za nyuma miaka ya hamsini, sitini na sabini kuna yale yaliyofanyika nyuma kwa SIRI kwa niaba ya SERIKALI ni vyema sasa yakawekwa wazi ili jamii IPUMUE yani ipate nafasi ya kujua A na Z ya zama hizo na kuchua nafasi hiyo kujifunza na kupata majibu magumu ambayo wananchi wamekuwa wakijuliza toka kipindi hicho.

  Zamani Tanzania hii miaka ya hamsini,sitini,na sabini mwanamke kuvaa suluari [Salawili] ilikuwa ni Uchuro kwa jamii lakini leo hii,karibuni vijiji vyote wanaona kawaida Mwanamke Kuvaa nguo hiyo.

  Hivyo hivyo ile iliyokuwa SIRI miaka hiyo kwa sasa sio SIRI tena bali inageuka kuwa ni funzo au Mwalimu wa Jamii kwenye hatua za mchakato wa maisha ya watu kati ya kizazi na kizazi.

  Hivyo ni wakati muhimu watanzania wakajua UKWELI HALISI WA MAMBO MUHIMU YA MSINGI AMBAYO,WAKATI HUO YALIKUWA GUMZO KWENYE JAMII KAMA VILE MIAKA MITANO YA SASA YA WANANCHI AMBAO WANATAKA KUJUA RICHMOND,DOWANS NA KAGODAA,NA AMBAYO KWA MUJIBU WA SETRIKALI SI RAHISI KUACHA WANANCHI WAJUE KWA FAIDA YA SERIKALI NA WANACHI HAO PIA.Ni sawa na ugomvi wa Baba na Mama kuanika wazi mbele ya watoto wadogo,lakini pindi wakikua watajua na wao kwa wakati huo watakuwa na uwezo mzuri wa kupima usahihi wa ugomvi ule na kuwa nani alikuwa sahihi kati ya Baba au Mama.

  Kufunguka kwa SIRI KUU hizo kunafungua vifungo vya kiroho vya wahusika wa mikakati hiyo [Mission] na kuwafanya kuwa huru na hivyo kuonyesha na kufundisha jamii kuwa SIRI KUU [CONFIDENTIAL] ni vitu vipo katika Seriali nyingi duniani na kuwa Serikali AIWEZI KUENDESHWA BILA SIRI na kuwa katika jamii ni vitu vipo muda na wakati ndio vinatoa ushawishi upi ufuatwe hiki au kile kijulikane kwa watu wote ili kuondoa madhara na mlipuko wa vulugu wa tafsiri ya hiyo SIRI katika wakati husika.

  Mfano yaliyojili kwenye kuta za IKULU kati ya CHADEMA na RAIIS WETU,kwa sisi tulio nje ya kuta hizo atujui wamekubaliana nini na vipi ghafra CHADEMA WAMEKUWA NI TOFAUTI KABISA NA WALE WA MWANZO.LEO HII WANASEMA WANAJITO KWENYE SWALA LA KATIBA NA HUKU HAWATOI MAELEZO YA KULIDHISHA.

  LAKINI KWA WANANCHI KUANZA KUFUNDISHWA KUKUBALI BAADHI YA SIRI KUU [GENUINE LAKINI] KAMA YA CHADEMA NA RAIS KUWA NI SIRI AMBAYO WENGINE HATUJUI KILICHOTOKEA TUNAONA KAMA MAIGIZO LAKINI NDIO IMETOKEA NA MAISHA YANAENDELEA.BASI NI VYEMA KUANZA KUELIMISHA UMMA KIMAPOKEO NA HIVYO KUONDOA MITAFARUKUA ISIYO YA LAZIMA AMBAYO INAWEZA KULETA MAAFA.

  NIWAKATI SAHIHI KUFUNGUIA SIRI ZA ZAMANI ZA MIAKA YA 60S NA 70S ILI KUTOA ELIMU NA MAFUNZO MAPYA KWA VIZAZI VIPYA INAKUWA NI ELIMU KWA WALE WA ZAMANI INAPONYA MAKOVU.

  Nimawzo yangu tu kama Mwanajf

  Nawasiilisha.
   
Loading...