Shule ni St. Joseph's Convent School. Mwaka wa 1967

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,909
30,253
ZAIDI YA MIAKA 50 ILIYOPITA

Shule ni St. Joseph's Convent School.
Mwaka wa 1967.

Darasa Form 1D.
Class Teacher Mrs. De Souza.

Darasa hili mchanganyiko Wasichana na Wavulana.

Form 1C Wasichana watupu.
Form 1A na Form 1B Wavulana watupu.

Nasoma darasa moja na Edward Makwaia sasa Chief Edward Makwaia wa Siha Usukumani amerithi kiti cha marehemu baba yake Chief David Kidaha Makwaia.

Nimemuona Chief David Makwaia katika runinga taarifa ya habari akiongoza Sherehe ya Wasukuma.

Haraka nimeingia Maktaba nikakuta katika picha zake nyingi nilizonazo hizo nilizoweka hapa ndizo za zamani zaidi mwaka wa 1967.

Picha hizi zimenirudisha nyuma sana.

Katika picha hizo yuko Juma Mwapachu na mdogo wake sasa marehemu Wendo Mwapachu, mama yetu Mary Mackeja akimwangalia Edward akikata keki ya siku yake ya kuzaliwa.

Nyuma ya mama wa kwanza kulia ni Wendo na nyuma ya Edward ni Andrew Gordon.

Mimi wa kwanza kulia nikifuatiwa na William Mfuko na Juma Mwapachu.

Nilipomrushia Ted picha hii kaniandikia, "Sidney tulikuwa wadogo."

Hakika tulikuwa watoto.

Screenshot_20210923-220903_Facebook.jpg
 
View attachment 1950087
ukitulia na kuwaza kwa undani haya maisha ya duniani huwa ni mafupi sana, nafikiri kuna maisha mengine baada ya kifo.

Hapa ni kama juzi tu - binafsi nilikuwa hata sijazaliwa kumbe dunia ilikuwepo na watu waliishi... maisha, kuzaliwa kuishi na kifo ni siri nzito.

Hongereni sana watoto wa town kwa birthday !!
 
Ila babu Sidney inaonyesha ni mtoto wa kishua.

Mimi ni wa 90s na sijawahi kua na rafiki msherehekea birthday kuanzia utoto mpaka leo.
Castr,
Zile zilikuwa nyakati nyingine kabisa.
Mambo yalikuwa mepesi.

Wala hata hivyo si wote tukisheherekea birthday.

Mimi sikupata kusheherekea birthday hadi sasa uzeeni tena wanangu ndiyo wananinunulia keki.

Utashangaa siku imefika mimi wala sikumbuki.

Ghafla wananivizia wanatoa keki hela wamechangishana tena hawa wanangu wa kike.

Sababu ni kuwa mimi Mswahili hatuna utamaduni huu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom