Mzee Mwana Kijiji I saluti you!
Kabla ya kujibu maswali yako (a) - (g) naomba tufahamishane kwamba kwamba tulipata uhuru miaka 50 iliyopita sii issue na haimaanishi kwamba lazima sasa tuwe na maisha kama ahera! Uhuru na historia ya nchi yetu kwa ujumla ni vitu tuanvyo takiwa kuvienzi pamoja na mapungufu yaliyopo bado itabakia kuwa historia ya nchi yetu no matter tumefikaje hapa tulipo.
nina sababu zifuatazo kuandika hayo maandishi hapo juu kama ifuatavyo:-I am out.
- Ni kweli kwamba nchi yetu in raslimali nyingi zikiwemo madini na kadhalika, ila kwa maoni yangu kuwa na madini bila technology bado its a problem, na ukuachilia mbali waarabu waliotajirika kwa mafuta siifahamu nchi yoyote ambayo imetajirika kwa kuuza madini, kuchukua kwa mfano nchi kama urusi ambaya ina madini zote unazozijua (kasoro tanzanite!), lakini wao sii nchi tajiri kuliko zote duniani ukizingatia kwamba walizigundua miaka mingi iliyopita (nafikiri mzee bado unamkumbuka Mandleeve aliyetengeneza periodic table of elements). nchi za africa ni africa ya kusini tu na walianza miaka mingi sana iliyopita. nchi nyingine ziko vitani kugombea nani anakula zaidi na ndiko tunakoelekea!!.
- kuhusu nchi yetu na miaka 50 na bado bado huduma za jamii haziko sawa ni tatizo ila kumbuka nchi ambazo hazijawahi kuwa koloni na zina hata maandishi yake kama Ethiopia wana nini?
- Nafikisiri una mfahamu Christopher Amergo Columbus aliyevumbua Amerika ni Mhisipania na Hispania ilianza biashara miaka mingi ikiwemo ya utumwa lakini hadi leo wao na jamaa za Wareno wako kwenye PIGIS, zile nchi chokambaya kuliko zote europe, zaidi ya kucheza football hamna kitu
- so, kabla ya kujiuliza maswali (a) - (g) inabidi tuifahamu historia yetu na tujue tuna nini na ni nini hatuna, if you ask me tungejitahidi tukatumia resources za kutosha tuchague vijana wenye pass nzuri tuwalipie kwenye vyuo vizuri wasomee taaluma za sayansi za uchumi na madini halafu warudi wafanye kazi! (angalizo: wawe wazalendo si wazamiaji). Wajerumani na wajapani walifanya hivyo baada ya vitakuu ya pili ambapo nchi zote zilikuwa magofu kwa kupigwa mabomu n sasa uchumi wao uko juu.
- mwisho, tuuheshimu uhuru wetu kwani ni historia yetu, Ujerumani na Japan wangekaa kuanza kutoana macho kwamba nani kifikisha nchi yao kwenye vita kuu wasingeinuka!!
@Nyantella, pamoja na kwamba hoja imesimama 'katikati' nikukumbushe tu kuwa Tanzania ilipata uhuru around the same time na Malayasia & Singapore. Hizi nchi mbili hazina hata robo ya rasilimali ilizinazo Tanzania. Lakini angalia wako wapi leo. Pia hoja kwamba Tanzania inabidi iwekeze kwenye elimu 'in theory' nakubaliana na wewe, lakini, hivi ni kweli Tanzaina haina wasomi? Hawa wanaojiita Ma-Dr ni waganga wa kienyeji au ni watu gani hasa?
Mimi naona tatizo like kwenye leadership. Hapo ndio chimbuko la matatizo yetu. Mzazi akiimbiwa mtoto ni mwizi lakini akakaa kimya usitegemee mtoto ataacha kuiba. Mbaya zaidi ni pale mzazi anawakataza 'law-enforcement agents' wasimguse mtoto. Kwa mfano, kwa nini hatujaambiwa hatma ya Jairo? Kwa nini? alifanya kosa au hakufanya kosa? Hivi Jairo ni illiterate? Waliochonga deal ya kusafirisha wanyama hai ni darasa la saba? au waliondaa mikataba ya madini yetu ni 'mamndenyi' (sorry kuna kuna mtu anatumia hii ID). Na huyu Dr. Masaburi aliyepiga mnada UDA naye hajasoma?