Miaka 50 baadaye: Je Unaiamini Serikali? Kwa nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 50 baadaye: Je Unaiamini Serikali? Kwa nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 19, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Hadi hivi sasa kama Mtanzania umesikia mengi kuhusu uongozi na utawala na matokeo yake katika maisha ya Watanzania. Umesikia sera mbalimbali zikifanyiwa kazi na mafanikio yakitangazwa. Kuanzia ujenzi wa barabara, mahospitali, kliniki, miundo mbinu mingine mingi na mipango kadha wa kadha ya maendeleo. Yawezekana umeweza kushuhudia juhudi mbalimbali za maendelo zinazofanywa na serikali. Utakuwa umesikia mipango na malengo mbalimbali ya serikali na pia kuna mambo umeyaona mwenyewe au kusimuliwa jinsi serikali ilivyofanya kuleta maendeleo.

  Na siku za karibuni bila ya shaka umesikia hatua mbalimbali za jinsi gani serikali imechukua kuonesha uongozi. Kuanzia sakata la Ngeleja na Jairo, sakata la BP na Mafuta na sasa sakata la Maige na wanyama. Yote yamefanyika katika kuonesha kuwa serikali iko "on top" of things; Bunge liko "on top" na kuwa viongozi waliochaguliwa "wanasikiliza wananchi".

  Lakini muda wote huo yawezekana umeona mengine mengi ambayo yameacha maswali. Katika kuadhimisha miaka hii hamsini unajisikiaje zaidi:


  a. unaamini serikali zaidi?
  b. Unaiamini lakini unataka uthibitisho?
  c. Unaishuku mara zote?
  d. Unashuku maamuzi yake?
  e. Huamini kabisa?
  f. Unaangalia watu gani wa serikali wanasema au kuamua; yaani unaamini katika watu binafsi kuliko taasisi zao?
  g. Hujali lolote linalofanywa na serikali?

  Kwanini?
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Siimani serikali lakini naangalia watu gani wa serikali wanasema na kuamua; - naamini katika watu binafsi kuliko taasisi zao.

  Sababu: Serikali kama serikali ina dalili zote za 'institutional failure & a lack of leadership at the top' lakini kuna watu mmoja mmoja wenye uwezo na nia ya kufanya vizuri na wamekuwa wanajitahidi kutenda within a 'rotten system' e.g. Mh. Magufuli. Huyu amekuwa anajitahidi sana lakini katika hali ya kushangaza waziri mkuu na hata rais mwenyewe kwa nyakati tofauti wamekuwa wanamfunga speed-governor 'hadharani'.
   
 3. d

  daligo JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2011
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 535
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  The president cant be trusted,Parliament(arians) cant be trusted& judical system cant be trusted hence nothing to be trusted at all for that case siiamini serikali kabisa not once not at all
   
 4. HT

  HT JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mh! MMKJ,
  mi siamini kama tuna serikali, anayebisha anithibitishe uongo. Kabla hatujajadili yote nionyeshe hiyo serikali, then nitajua kama nipo ktk kundi gani!
   
 5. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Maamuzi ya serikali mara nyingi ni ya kushuku cause of hypocricy there in it!!! mara nyingi wanasema hivi ilhali wanamaanisha vile! quite the opposite of what they say na kutenda! angalia inshu ya mafuta wiki chache zilizopita na sakata la BP, inshu ya utoroshaji wanyama kupitia KIA, posho za polisi 100000/=,1500000/=, Jairo na matamsha ya Pinda nk nk!
   
 6. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Kwangu 'e'
   
 7. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  mimi nashuku maamuzi ya serikali

  sababu:1. maamuzi ya kukurupuka yanayotolewa na serikali na vyombo vyake bila kufanya uchambuzi wa kina wa maswala husika mfano sakata la mafuta na umeme
  2. Serikali kuishia kuunda tume lukuki kuchunguza tuhuma mbalimbali ilhali mapendekezo ya tume hizo hayafanyiwi kazi yoyote wakati tume hizo zinakua zimepoteza muda mwingi na fedha za umma.
  3. viongozi wa serikali kufanya maamuzi si kwa maslahi ya nchi bali ya kwao binafsi na hasa wanapoingiza siasa na kujitaufutia umaarufu wakati wananchi wanataabika mfano mgogoro wa mstahiki meya na waheshimiwa wabunge wa DSM.
  Ngoja niishie hapo maana ni nyingi mno.
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Never did and never will I!!!!!!
   
 9. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nimeishi awamu zote nne...
  1. Awamu ya kwanza,jibu langu lingekua A. (Hapo ni silver jubilee remember)
  2. Awamu ya pili,jibu lingekua C
  3. Awamu ya tatu.....D
  4. Awamu ya nne.....E kwa kweli...without doubt!

  Kwa kuwa tupo leo na si jana, serikali ya leo Siiamini kabisa,
  • Ni beyond kipimo cha kuamini watu binafsi kwasababu hakuna aliye kwenye nafasi ya kusema au kuamua ambaye ana nguvu ya kufanya hivyo binafsi....ni "caucus" ndiyo inaamua....na siiamini hata kidogo! Ninaowaamini hawasemi wala hawaamui....unfortunately!
  • Ni beyond kutaka uthibitisho,kwasababu muda niliojiwekea wa kusubiri uthibitisho ulishapita siku nyingi.
  • Ni beyond Kuishuku mara zote au kuishuku kwa maamuzi yake kwasababu it's no longer a gray issue....it's solid BLACK, indeed! Na sasa imeamua kutokufanya maamuzi yeyote!
  Well,kuhusu kwamba ninajali lolote linalofanywa na serikali au la......I'm not very sure....I'm not really sure kwa mfano,kama ningekutana na mmojawao kichochoroni, karibu na kwetu nisingemtupia jiwe zito usoni!...sijui!
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Aug 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Mnakiamini chama cha Mapinduzi kinachoongoza serikali hiyo?
   
 11. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2011
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ... inawezekana pia katika mada hii kujiuliza pia kwamba SERIKALI ya CCM siku zote hizi, MIAKA 50, inaweza kujivunia nini kama ushahidi tosha wa mafanikio ya kubadilisha maisha ya Watanzania kutoka kwenye dimbwi la umasikini uliokithiri.

  Vigezo A hadi G vinaweza kujibika kwamba serikali imekuwa a self serving institution, period. Ngonjera zote tunazosikia ni za kulinda ulaji, na not necessarily to serve the people. Ndio, kwani serikali ingepaswa kuwa imewafanyia nini Watanzania? Kama kuna mwenye macho anayesubiri aambiwe atazame, labda anafaidika na madudu ya hao
   
 12. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  A big NO!
   
 13. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #13
  Aug 19, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Sio kutokukiamini tu nina hasira nacho, usitake nipate Ban Mwanakijiji.
   
 14. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #14
  Aug 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Binafsi siamini kama kuna serikali bali naamini kuna kundi la wanyonyaji.
   
 15. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #15
  Aug 19, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Atiiiii?????:coffee:
   
 16. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #16
  Aug 19, 2011
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />

  Mkuu kwa tahadhali weka keyboard mbali, maana I can feel u..!
   
 17. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #17
  Aug 19, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Kuanzia Serikali mpaka chama nawapa big NO
  Siamini kama kuna serikali maana haionekani haipo na kama inaexist naomba MWKJJ unionyeshe ilipo maana ingekuwepo ingekuwa na maamuzi kuhusu mustakabali wetu
  Siamini katika chama maana ndo kabisa zao la serikali hii isiyoaminika na nina hasira nacho mbaya maana kimezaa serikali ambayo haipo na haifanyi kazi
  Tumebakiwa na kikundi cha watu wanaojiita serikali ambao wanafanya mchezo wa kuigiza wa kuongoza nchi fulani ambayo haipo
   
 18. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #18
  Aug 19, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Mh, kila ninachotaka kuandika naona kama sitaeleweka maana
  leo nina hasira sana, anyway, ngoja nisome maoni ya wengine
  kwanza wakati nikitafuta neno lenye tafsida kidogo.
   
 19. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #19
  Aug 19, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Bishop nina hasira ambazo naweza zimalizia kwenye keyboard yangu
  Nimekuja ofcn na shati ambalo halijapasiwa na toka jana juzi usiku sijauona umeme na ukirudi unarudi saa nane za usiku unakatika saa kumi alfajiri na sitauona tena mpaka saa nane za usiku kesho yake.
  Na eti tunasema tuna serikali au chama cha siasa kinachoendesha serikali
   
 20. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #20
  Aug 19, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Ndiyo maana nimeamua nisichangie kwanza nisome mijadala ya wengine...
   
Loading...