Miaka 50 baada ya uhuru.

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Kuna mzungu mmoja namjua kwa jina la Mark anamiliki hekari mia kadhaa za ardhi mitaa ya kijiji cha Ifunda.Kwa kifupi huyu bwana anawanyanyasa sana wanakijiji wanaoishi maeneo yanayozunguka mashamba yake.Siku moja nilikuwa nikipata lunch baada ya kazi pale Ifunda ndipo nikashuhudia akina mama kadhaa wamekamatwa na walinzi wa kimasai wa huyu mzungu.Kosa la akina mama hawa lilikuwa ni kutafuta uyoga na kuokoteza kuni ndani ya eneo la huyu mzungu.Kwa kosa hilo,walipelekwa kituo kidogo cha polisi ifunda na kuchapwa bakora kadhaa na kuonywa wasirudie tena.Walinzi hawa wa kimasai inasemekana wamekuwa wakiwakamata watoto wadogo wanaojaribu kuvua vijisamaki katika kijito kinachokatiza eneo la huyu mzungu na kuwapiga sana.Kama haitoshi,watoto hawa hulazimishwa kuwatafuna hao samaki waliowavua wakiwa wabichi vivyo hivyo.Mbaya zaidi inasemekana J.K ni swahiba wa karibu wa huyu mzungu na mara kadhaa amekuwa akimtembelea kisirisiri huko shambani.Inanisikitisha,anyway nakutakia maandalizi mema ya sherehe ya miaka 50 ya uhuru wa taifa letu.
 
wanafunzi wa tz.jpg

wanasheherekea miaka 50 ya uhuru.



shule za igunga.jpg
 
Back
Top Bottom