Miaka 5 ya Rais Magufuli na maendekeo ya vitu, na kuachana na maendeleo ya watu

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Messages
4,095
Points
2,000

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2012
4,095 2,000
Magufuli oyee🇺🇸(soma hadi mwisho tarehe 9+9+9 katika kuna tukio litatokea too pain)

Magufuri kama utakumbuka ulipoichukua nchi umarufu wako ulipanda kuanzia asilimia 2% hadi kufikia 79% Afrika.

Ulipokuwa ukienda Kenya wanachi walivaa mavazi ya jina lako na Afrika nzima waandishi walikuandika kwenye vitabu na makala kama kiongozi bora Afrika, ila sahivi nani kenya au Afrika ataomba uwe raisi wao hata kwa nepe la usingizi.

Magufuli oyee🇺🇸
Kabla ya kuapishwa na kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania picha zako zote zilikuwa nyeusi ila sahivi zote unazopigwa zinakuonesha mweupe hakika madaraka sio sabuni ya roho hata moyo unabadilika rangi.

Ni huyu huyu wewe ambaye ulisema utalinda katiba ya Tanzania!
Ni huyu huyu wewe ambaye ulisema utalinda amani ya Tanzania!
Ni huyu huyu wewe ambaye ulisema utalinda uhuru na haki za binadamu!
Ni huyu huyu wewe ambaye ulisema utalinda ajira za vijana!

Magufuli oyee🇺🇸
Sasa ni mwaka wa tano toka uingie madarakani katiba unaitumia utakavyo tulivyo wajinga sisi tunakusifia na kusema kazia hapo hapo baba.

Sasa ni mwaka wa tano toka uingie madarakani tumepata msamiati wa neno watu wasiojulikana ila ni watumishi wako wanavunja amani za wananchi tukiogopa kusema tusije kupotezwa.

Sasa ni mwaka wa tano toka uingie madarakani watanzania hatuna haki ya kuikosoa na kupendekeza maoni tukiogopa risasi kama zile za Tundu Lissu kitupasua utumbo kama Aquiline.

Sasa ni mwaka wa tano vijana tupo vijiweni hatuna ajira wala fungu la kuanzisha biashara tukiomba mkopo unaambiwa uwe na biashara nitaanzisha vipi biashara bila mkopo au mtaji.

Sasa ni mwaka wa tano toka uingie madarakani umesema hutaki kushauriwa jamani mwogope hata Mungu wenda akufanye kuwa malaika wa nuru.

Magufuli oyee🇺🇸
Magufuli umeleta uwoga serikalini ila sio kupambana na ufisadi sahivi aliyemgongoni mwako ndiye anye kula kwa urefu wa kamba yake na wengi wanalipua majengo na mahoteli ndio maana wanakusifia vibaya wanasahau wengine wanakufa kwa utapia mlo.

Magufuli toka angalau kwa dakika moja njoo utazame maisha yanavyozidi kuwa magumu mitaani, lengo lako na nia yako ni kuifikisha Tanzania mbali ila toka usingizini pokea ushauri huku vijana wataanza kuuza vyuma vya daraja unayojenga na mipango itaharibika.

Magufuli toka utazame lini nyumba ya nyasi na tope inawekewa umeme zaidi ya hiyo ghalama tungemboreshea kwa kumpunguza vifaa vya ujenzi na mabati tusiangalie sera ya kufurahisha ila tukumbuke usalama zaidi.

Magufuli toka utazame hakuna dawa wala matibabu ya bure kama ulivyosema 2015, watu wanakufa kwa kukosa tiba na madawa tumeletewa mfumo mpya hadi uwe na bima ya afya ndio unatibiwa ghalama zake ukizisikia duh utamfanya mama angu kijijini anywe mitishamba mpaka akumbuke mizimu ya mababu.

Magufuli toka utazame viongozi wako wanatuchezea vichwa kila kukikucha wanakuja na filamu halijatoka hili limeibuka jipya kwani wao ndio wanaweza kuingiza tu hata sisi tunaweza sema njaa inauma tumbo baba tupo kutazama tu.

Magufuli oyee🇺🇸
Watanzania tuungane ni mdaa wa kurejesha umoja wetu, umoja ni nguvu utengano ni udhaifu anayofanya Magufuli sio yote ni mabaya ila kuna mengine tusimame kama taifa kusema bila uwoga tunahitaji serikali ya Magufuli ifanye mabadiliko mtatutesa na kuwapoteza wachache ila mtawaibua wengine wapya ujumbe wameshare ili uwafikie nyinyi viongozi.
 

ngwanduu

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2018
Messages
321
Points
250

ngwanduu

JF-Expert Member
Joined Sep 20, 2018
321 250
beberu wewe mwacheni magufuli tulio na akili timamu tunaona yaliofanyika awamu hii haijawahi kutokea kuanzia awamu ya pili hadi yanne, reli ya dar moshi ilikufa tangu miaka 90+ leo magufuli kaifufua ,nenda pale wami daraja kubwa linajengwa ,kafufua shirika la ndege na kununua ndege mpya, angalia kinachofanyika hapo Dar es saalam ubungo, reli ya kisasa dar to mwanza ,elimu bure, vituo vya afya kajenga miaa tatu na sitini , bwawa la kufua umeme , ,.
Mungu endelea kumpa makufuli moyo wakizalendo katika kuwaletea watanzania maendeleo,

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics

Threads 1,390,268
Members 528,139
Posts 34,047,866
Top