Miaka 49 ya uhuru:-kukithiri kwa umaskini, ujinga na maradhi ni umwagaji damu pia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 49 ya uhuru:-kukithiri kwa umaskini, ujinga na maradhi ni umwagaji damu pia

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Jatropha, Oct 11, 2010.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  [FONT=&quot]Mara tu baada ya Tanganyika kupata uhuru wake Mwalimu Nyerere aliwatangaza maadui watatu wa taifa hili kuwa ni Umaskini, Ujinga na Maradhi, na kaanzisha rasmi mapambano dhidi ya maadui hao. Licha ya kutambua kuwa Tanzania ina utajiri mkubwa wa maliasili kama vile madini ya aina mbali mbali, alichelea kuanza uchimbaji mkubwa wa madini hayo mpaka Tanzania itakapokuwa imeweza kusomesha wataalamu wake wa fani mbali mbali ikiwemo Sheria, Uhandisi, Uchumi n.k ili kulinda maslahi ya taifa katika uchimbaji madini. Hivyo Mwalimu Nyerere alilazimika kutumia raslimali kidogo zilizopakuwepo kuwapatia watoto wa wakulima na wafanyakazi elimu na huduma ya afya ya bure kwa nia ya kujenga taifa lenye umoja, usawa,uzalendo na kutokuwa na matabaka.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Matazamio ya Mwalimu Nyerere kuwa watoto wa wakulima na wafanyakazi aliowasomesha bure na kuwarithisha uongozi wa CCM na Tanzania yanazidi kufifia mwaka hata mwaka. Hii ni kutokanana Ubinafsi, Choyo, na Tamaa ya kujilimbikizia mali kuwakumba wanasiasa ndani ya chama kikongwe cha siasa cha CCM baada ya kifo cha Mwalimu Nyerere. Hivyo badala ya raslimali za Tanzania kutumika kutokomeza Umaskini, Ujinga na Maradhi; wanasiasa hao walafi ndani ya CCM wamejijengea mitandao na Mafisadi na Vibaka Uchumi kupora raslimali za Tanzania huku wakiendeleza kutumia ulaghai, ghiliba na vitisho dhidi ya wananchi ambao wanaonekana kukerwa na na kukithiri kwa maadui Umaskini, Ujinga na Maradhi vinavyopelekea kuwepo ongezeko kubwa la vifo vya watanzania kutokana na sababu zinazoepukika. [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Mfumo wa vyama vingi vya siasa ambao ulirejeshwa hapa nchini mwaka 1992 ndio kwa sasa unaonekana kutaka kuleta ukombozi wa pili wa Tanzania dhidi ya Mafisadi na Vibaka Uchumi ndani ya CCM. Licha ya uchache wao katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya mwaka 2005 -2010, wabunge wa upinzani hususan kutoka chama cha CHADEMA walijitoa mhanga kupaza sauti dhidi ya Mafisadi na Vibaka Uchumi hao. Hivi sasa mmoja wa wabunge hao shupavu Dr Wilbroad Slaa amejitokeza kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kwa nia kuwakomboa watanzania kutoka katika makucha ya Mafisadi na Vibaka Uchumi hao. [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kama ilivyotokea mwaka 1995 wakati watanzania walipoonyesha kwa vitendo kuwa wanataka mabadiliko, CCM ilitumia hja za umwagaji wa damu katika nchi za jirani kuwatisha wananchi ili wasichague vyama vya upinzani. Kituo kimoja cha runinga kilitumika kuonyesha picha za mauaji ya Kimabari ya Rwanda kama sehemu ya mkakati wa kuwatisha wananchi.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Katika kuelekea ukingoni mwa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, CCM imeamua kuzusha upya madai ya umwagaji damu za watanzania dhidi ya wagombea wa vyama vya upinzani kwa nia ya kuwatisha wananchi. Mgombea Urais wa CCM, ambaye ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayemaliza kipindi chake cha kwanza Dr Jakaya Kikwete amenukuliwa akidai katika mikutano ya kampeni za CCM kuwa baadhi ya washindani wake wapo tayari kumwaga damu za watanzania katika harakati za kusaka tiketi ya kuingia Ikulu. Aidha CCM inadaiwa kutumia kampeni chafu kupitia mitandao ya simu zikimchafua mgombea urais wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa kuwa yuko tayari kumwaga damu za watanzania ili kuingia Ikulu”.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Katika hali ya kutaka kuwajenga watanzania hofu zaidi, vyombo vya ulinzi na usalama navyo kwa upande wake vimeibuka kuingilia shughuli za Tume ya Uchaguzi kwa madai ya kuwepo madai ya umwagaji damu za watanzania katika kipindi hiki cha uchaguzi. [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Neno “umwagaji damu” lina maana gani? Na kwanini hutumika wakati wa uchaguzi tu, ilihali watanzania kwa maelfu hupoteza maisha kila siku kutokana na sababu mbali mbali zinazoepukika? Kwa kiwango linashiria kikubwa kuibuka kwa vurugu kufuatia vyama vya siasa kutokukubali matokeo ya uchaguzi. Hivyo wanasiasa wa CCM wanaolitumia neno hilo kwa kiwango ikubwa hivi sasa wanataka kutuambia kuwa ni halali kwa maelfu ya watanzania kupoteza maisha wakati mwingine wote wanapokuwa madarakani, isipokuwa wanapokabiliwa na ushindani kutoka vyama vya upoinzania nyakati za uchaguzi tu. Mbona wakati mwingine wote hatuaoni wakichukua hatua zozote kuzuia watanzania kupoteza maisha kutokana na sababu zinazozuilika? Katika hali hiyo ni chama kipi ni chinja chinja na mumiani, kama sio CCM ambayo hufurahia kutuma rambi rambi kila kukicha, pasipo kuchukua hatua kukomesha mauaji ya watanzania. [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Sheria ya 1984, Kifungu cha 14 (Haki ya Kuishi) kinatamka kuwa Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria. Kwa mujibu wa kifungu hiki ni wajibu wa Serikali na viongozi wa Serikali kumhakikishia kila raia wa nchi hii haki ya kuishi wakati wote na sio katika kipindi cha uchaguzi tu.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Hivyo sio sahihi hata kidogo viongozi wan chi kuwa wanafiki na kujidai kuwa wanajali sana maisha ya watanzania katika kipindi hiki cha uchaguzi , ilihali katika uongozi wao wa miaka mitano wameshindwa kutimiza matakwa mbali mbali ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hali iliyosababisha wananchi kwa maelfu kupoteza maisha (kumwaga damu).[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kifungu cha 8[FONT=&quot] cha Katiba kinatamka kuwa -(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo -[/FONT][/FONT]
  [FONT=&quot](a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;[/FONT]
  [FONT=&quot](b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;[/FONT]
  [FONT=&quot](c) Serikali itawajibika kwa wananchi;[/FONT]
  [FONT=&quot](d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Aidha kifungu cha 9 pamoja na mambo mengine kinatamka kuwa “…..Kwa hiyo, Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha-[/FONT]
  [FONT=&quot](a) kwamba utu na haki nyinginezo zote za binadamu zinaheshimiwa na kuthaminiwa;[/FONT]
  [FONT=&quot](b) kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa;[/FONT]
  [FONT=&quot](c) kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumyonya mtu mwingine;[/FONT]
  [FONT=&quot](d) kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa na kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja;[/FONT]
  [FONT=&quot](e) kwamba kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi, na kazi maana yake ni shughuli yoyote ya halali inayompatia mtu riziki yake;[/FONT]
  [FONT=&quot](f) kwamba heshima ya binadamu inahifadhiwa na kudumishwa kwa kufuata Kanuni za Tangazo la Dunia kuhusu Haki za Binadamu;[/FONT]
  [FONT=&quot](g) kwamba Serikali na vyombo vyake vyote vya umma vinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia wote, wake kwa waume, bila ya kujali rangi, kabila, dini au hali yamtu;[/FONT]
  [FONT=&quot](h) kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini;[/FONT]
  [FONT=&quot](i) kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha[/FONT]
  [FONT=&quot] umaskini, ujinga na maradhi;[/FONT]
  [FONT=&quot](j) kwamba shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia zinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi;[/FONT]
  [FONT=&quot](k) kwamba nchi inatawaliwa kwa kufuata misingi ya demokrasia na ujamaa.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kwa kuwa Katiba ndiyo sheria mama, na kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara tu baada ya kutangazwa mshindi hutalkiwa kuapa kuilinda na kuitetea Katiba hiyo, ikiwemp vifungu vilivyotajwa hapo juu.
  [/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Inapojitokeza kuwa idadi kubwa ya watanzania wanapoteza maisha kutokana na watawala yaani Raisa na chama tawala kushindwa kutekeleza kikamilifu Kifungu 9 a,b,c,i na j hapo juu; basi huo ni ukiukwaji wa Kifungu cha 14 cha Katiba na kuwavunjia wananchi wanaopoteza masiha haki yao ya Kuishi. Hali hiyo haina tofauti na umwagaji damu mwingine wowote kama vile ujambazi, mauaji n.k.[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Hebu tutazame vyanzo mbali mbali vinavyosababisha upotevu wa idadi kubwa a miasha ya watanzania. Inakadiriwa kuwa hapa nchini akinamama 8000 hupoteza maisha kila mwaka wakati wa kujifungua kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kukosa huduma za kujifungua salama, ukosefu wa madakatari, manesi, wauguzi na madawa, zahanati, vito vya afya na hospitali. Hivyo katika miaka mitano ya utawala wa CCM na JK ni akinamama 40,000 wamepoteza maisha ilihali Serikali ya JK ikitumia utajiri wa nchi hii kununua magari ya kifahari, kila wizara ikitengewa kati ya Bilioni 20 hadi 30 kama fedha za chao na vitafunwa kinyume na Kifungu cha 9 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Inakadiriwa kuwa kati watanzania milioni 14 hadi 18 huugua ugonjwa wa malaria kila mwaka na kati yao 60,000 hupoteza maisha kwa kukosa huduma za afya kwa wakati kutokana na ukosefu wa madakatari, manesi, wauguzi, madawa, vifaa vya tiba, zahanati, vituo vya afya na hospitali. Ndio kusema kuwa katika miaka jmitano ya utwala wa Kikwete zaid ya watanzania Laki Tatu walipoteza maisha kutokana na ugonjwa wa malaria ilihali Serikali ya CCM ikifanya matumizi makubwa ya fedha na raslimali za taifa katika ahali isiyoelekeza kuokoa maisha ya watu hawa.
  [/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Hebu tujiulize ni watanzania wangapi wanapoteza maisha kutokana maradhi yatokanayo na kunywa maji yasiyo salama k.m magonjwa ya Kipindipindu, Kuhara n.k wakati ambapo viongozi wa CCM na Serikali yake wakitumia utajiri wa nchi hii kulipatia kundi dogo la viongozi wake na Serikali maji safi kwa ajili ya kuoshea magari, kunyweshea bustani za maua na majani, na kujaza mabwawa ya kuogelea kinyume ya Kifungu cha 9 (i) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinachotamka kuwa “matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha umaskini, ujinga na maradhi”[/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Kwa kipindi cha miaka mitano ya JK maelfu ya watanzania wamepoteza maisha kutokana na ajali za barabarani ambazo zingeweza kuepukika kama kiongozi huyo angekuwa makini zaidi katika uendeshaji wa nchi. Kwani si siri tena kuwa ajali hizi husababishwa na madereva waliopatiwa leseni za udereva na serikali za CCM kwa njia za rushwa pasipo kupata mafunzo na kufaulu mitihani ya udereva wa magari, pikipiki, bajaj, malori na mabasi ya abiria n.k. Je huku sio kwa ishara ya viongozi wa CCM kushindwa kuongoza nchi. Wanataka mpaka watanzania wangapi wapoteze maisha, kugeuka vilema na mayatima ndipo wakubali kuwa CCM imeshindwa kuongoza Tanzania kutokana na kutafunwa na mchwa rushwa na ufisadi?[FONT=&quot]

  CCM na serikali zake zinahusika moja kwa moja na umwagaji wa damu za wakulima na wafugaji waliohusika katika mapigano katika sehemu mbali mbali za nchi yetu kama vile Kilosa na kwingineko; kufuatia vitendo vya rushwa vya baadhi ya viongozi wake kuwamilikisha wawekezaji uchwara ardhi ya wafugaji wa maeneo ya Loliondo, Ngorongoro n.k na wafugaji hao kulazimika kuhama na mifugo yao na kuhamia maeneo ya wakulima.

  Hata hivi sasa idadi kubwa ya watanzania wanaendelea kupoteza maisha (umwagaji damu za watanzania) katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu wa 2010 kwa sababu zilizotajwa hapo juu kwa madai kwamba serikali ya CCM haina fedha kuwapatia wananchi madawa, huduma za madakatari, manesi na wauguzi pamoja na na vifaa vya tiba ilhali ccm ikitumia bilioni 50 katika kampeni zake kugombea viti 237 tu ilihali chama cha conserrvative cha uingereza kilitumia bilioni 42 tu kugombea viti 639. Na nchi ni mmoja wa wafadhili wetu wakuu na bajeti ya 2010/11 imetupatia bilioni 240. Iweje CCM iwe na matumizi makubwa ya fedha kuliko vyama vya siasa vinavyoongoza katika nchi wafadhili wa Tanzania? Hapo moja kwa moja ni ukiukwaji wa Kifungu cha 9 cha Katiba na hivyo kusababisha umwagaji wa damu endelevu za watanzania.[/FONT]
  [/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Kutokana na Dr Slaa na CHADEMA kutaka kusimamia upangaji upya wa mgawanyo wa raslimali za Tanzania kwa mujibu wa Kifungu cha 9 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutunga Katiba mpya ambayo itaondosha ukiritimba wa kikundi kidogo cha wanaCCM kwenye raslimali za Tanzania na kuwashughulikia Mafisadi na Vinaka Uchumi wote wanaoongozwa na CCM ndio maana Jakaya Kikwete anawaghilibu watanzania maskini na wasiokuwa na ufahamu wa kutosha kuwa ni umwagaji damu za watanzania.
  [/FONT]

  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Laiti kama mgawanyo sawa wa raslimali za Taifa ungefanyika kutokea mwaka 1995 ni watanzania wangapi waliopoteza maisha wangeokolewa kutokana na bajeti ya afya, elimu na kuondoa umaskini kuongezwa maradufu? Hivyo propaganda za CCM kuhusu umwagaji damu ni za kuogopwa kama ukoma kwani husababisha maelfu kupoteza maisha kila mwaka. [/FONT]
   
 2. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
Loading...