Miaka 48 ya Uhuru: Tusake mabadiliko ya kweli tupate uhuru wa kweli-2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 48 ya Uhuru: Tusake mabadiliko ya kweli tupate uhuru wa kweli-2

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by John Mnyika, Dec 20, 2009.

 1. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #1
  Dec 20, 2009
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Nawaletea sehemu ya pili ya makala yangu kuhusu miaka 48 ya Uhuru; tarehe 9 Disemba nilianza kuchambua hali ya kiuchumi na kutoa mwelekeo mbadala. Leo nachambua hali ya kijamii. Makala husika inapatikana hapa: http://mnyika.blogspot.com/2009/12/miaka-48-ya-uhuru-tusake-mabadiliko-ya.html

  Tuendelee na mjadala, sitaweza kuchangia mara kwa mara. Bado tupo katikati ya Operesheni Sangara; tunakwenda vijijini sana kuhamasisha uwajibikaji wa viongozi/serikali, kueneza sera mbadala za CHADEMA na kujenga oganizesheni ya chama.

  Tayari tumeshapita kata za Tanga mjini, Mkinga, Pangani, Muheza, Handeni, Kilindi. Leo tupo lushoto na tutaendelea na wilaya zingine mpaka kieleweke; kwa wanaotoka maeneo haya na wangependa kutoa mchango wa hali na mali kufanikisha Operesheni hii tafadhali tuwasiliane kupitia 0754694553 au 0784222222. Nawatakia heri ya Noeli na Mwaka Mpya

  JJ
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Dec 20, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280

  mmefungua matawi mangapi mapya, mmepata wanachama wapya huko.? na mnaandikisha vijana kwa kiasi gani?
   
 3. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #3
  Dec 20, 2009
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Kaka

  Tutatoa tathmini kamili mara baada ya kumaliza ziara, ila cha msingi ni kuwa tunafungua matawi na kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye DKWK hususani Vijana.

  Bado tunatakribani nusu wiki ya kuendelea na ziara na tuna vikosi mbalimbali. Lazima tufanye tathmini yenye kuunganisha timu zote na vijiji vyote tulivyopita.

  Kwa ujumla ziara hii ni mzigo mzito unaopaswa kuwezeshwa kwa hali na mali na wapenda demokrasia na maendeleo.

  Ni kazi ngumu, mavuno ni mengi lakini watenda kazi ni wachache; nikirejea Dar es salaam nitaandika awamu kwa awamu mang'amuzi yangu kuhusu hali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi katika maeneo ambayo binafsi nimeyatembelea na kuhutubia huku vijijini.

  Nawatakia mjadala mwema

  JJ
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Dec 20, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  tunasubiri kwa hamu sana.. maana feedback ya operesheni Sangara ya kanda ya ziwa hatujasikia na wala mavuno ya kule Kiteto, Tunduru, Busanda, na Biharamulo yalifikia wapi..
   
 5. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #5
  Dec 21, 2009
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Sangara ya Kanda ya Ziwa imewezesha CHADEMA kufanya vizuri kwenye uchaguzi wa mitaa mwaka 2009 tofauti sana na 2004 ukilinganisha na mikoa ambayo Sangara haikupita(isipokuwa Kigoma). Kiteto, Busanda na Biharamulo by elections zimeisaidia CHADEMA kupata viti vingi vya vijiji kwenye majimbo yote matatu ukilinganisha na majimbo jirani na hayo ambayo hakukuwa na by elections. Kumbuka Kiteto hata by election iliyofuatia ya udiwani kata ya matui, CHADEMA ilishinda pamoja na CCM kuweka nguvu kubwa. Ukiondoa Kiteto, majimbo ya Busanda na Biharamulo CHADEMA haikuwa na nguvu kabisa mwaka 2005, ilikuwa chama cha tatu na pengine cha nne, lakini 2009 pamoja na hujuma zote imekuwa ya pili ikishindana kwa karibu na CCM. Kwa hali niliyopita huku Tanga, majimbo mengi CHADEMA imepanda kisiasa kutokana na Sangara. Kila kata tuliyopita matawi yamefunguliwa, hata maeneo ambayo awali CHADEMA haikuwa na wanachama kabisa. Pia kwa ujumla, zipo kata ambazo zilikuwa ni CCM peke yao, kuanzia sasa ni CCM na CHADEMA. Kama nilivyoahidi, nikitulia nitaandika kuhusu kata nilizopita

  JJ
   
Loading...