Miaka 45 ya CCM: Wanachama na Viongozi wa CHADEMA ndio wanaongoza kwa kujiunga CCM ukilinganisha na wapinzani wengine

Kwa hiyo unataka kumaanisha chadema Safi lazima azaliwe humohumo akitokea ccm ni kirusi?

Utakuwaje CHADEMA Safi umezaliwa CCM. Wengi wanaosumbua ni wale waliokuwa CCM wakahamia CHADEMA. Mtu aliyezaliwa CHADEMA Kama Mimi , siijui CCM sijawahi Hama mpaka Leo Nina miaka 17 Sasa na sioni chama bora Kama chadema. Lakini wahamiaji ndio virusi vibaya ndani ya CHADEMA.

Angalia Esther Bulaya na akina kaboyoka kina Waitara walichofanya CHADEMA leo. Virusi Ni wahamiaji ambao wameingizwa CHADEMA kwa maslahi. Nakiomba chama changu kianze kuinvest kwa die hard supporters na kuachana na wageni wanaokuja kuchukua vyeo na kuharibu chama maslahi yanapoondoka.
 
Wakati tarehe 05/02/2022 CCM itasherehekea miaka 45 tangu kuasisiwa pia kitawashukuru wanachama wa Chadema waliouona mwanga na kuamua kujiunga na chama tawala.

Takwimu zinaonyesha kuwa wanachama na viongozi wa Chadema ndio wanaongoza kwa kuunga mkono juhudi za CCM katika kuwaletea wananchi maendeleo ukilinganisha na vyama vingine vya upinzani.

Mfano wa viongozi wa juu wa Chadema waliovutiwa zaidi na CCM ni pamoja na Amani Kabirou rip, Dr Slaa, Tambwe Hiza, Dr Mashinji, Mwita Waitara, Cecil Mwambe, Dr Gekui, Patrobas Katambi, Juliana Shonza, Dr Mollel, Dr Lijualikali, Dr Joshua Nassari, David Silinde nk...nk.

Viko vyama makini vya upinzani ambavyo vinaiunga mkono CCM bila wanachama wake kuhamia Lumumba kwa sababu ya kuendekeza njaa, vyama hivyo ni pamoja na TLP, NCCR, Cuf na ACT wazalendo.

Mungu wa mbinguni awabariki CCM.

Mungu wa mbinguni akibariki Chama Tawala.

Maendeleo hayana vyama!

Sasa mbona mnauwa watu ,mnawatia vilema watu kwa kutumia vyombo vya dola kulazimisha ushindi badala ya kuwaachia Hao wananchi wakaichagua hiyo CCM wanayoipenda ?
 
......... It's very simple. Ndio wanaongoza kununuliwa na ccm kuliko vyama vingine kwa sababu wao ndio ccm wanawalenga kwa sababu vyama vingine vile wamevipandikiza wao.
 
Back
Top Bottom