Miaka 45 ya CCM na uoga wa Katiba Mpya

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
CCM ina miaka 45 toka kuzaliwa kwake ni chama kikongwe ktk siasa
Najiuliza pamoja na ukongwe wake katika siasa kwanini inaogopa mabadiliko ya katiba mpya?

Mchakato wa katiba mpya ulianzishwa na mwenyekiti wa CCM

Na rais mstaafu jakaya kikwete baada ya kuona tuna katiba iliyokaa miaka zaidi ya 50 na mambo mengi yamebadilika na akaunda tume

Chini ya mzee warioba
Wananchi wakachangia maoni yao na kutoa mapendekezo yao .Katika uchaguzi mkuu wa 2015 suala la katiba mpya lilikuwa kwenye ilani ya ccm ya uchaguzi mkuu lakini rais magufuli baada ya kuapishwa

Akadai sio kipau mbele na mchakato ukasimama mpaka leo

Najiuliza ukomavu wa ccm wa miaka 45 kwanini wanaogopa katiba mpya?
Wanaiweka kwenye ilani yao lakini wanaogopa kuitekeleza.

Wananchi tunataka katiba mpya kwani katiba ni ya Wananchi
20211217_073047.jpg
bd9fadcfec3a952bb7beefef291bd5f6.jpg
 
Back
Top Bottom