Miaka 42 ya kuzaliwa CCM na mzimu wa Tundu Lissu

Mromboo

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,928
6,467
Wasalaam wana jukwaa.
Leo ni siku muhimu sana kwa wanaCCM kote nchini katika kuelekea Kilele cha miaka 42 ya kuzaliwa chama hiki kikongwe kabisa barani Africa na duniani kwa ujumla. Katika hekaheka zangu kwenye mitandao ya kijamii na mikusanyiko tofauti ya uzinduzi wa sherehe hizi hii leo, nimegundua kuwa CCM kama chama tawala na Chama kongwe wametumia muda wao karibia 90% kumnanga mnadhimu mkuu wa upinzani na Mwanasheria wa CHADEMA na pia Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kama ndiye Chanzo cha CCM kushindwa kutekeleza majukumu yao.

Jambo hili limefikia kiwango cha viongozi wa CCM Kuanzia katibu Mkuu mpaka kiongozi wa shina kupandikiza chuki kubwa sana kwa WanaCCM na Watanzania kwa ujumla kuwa adui mkubwa wa nchi hii ni Tundu Lissu. CCM wanatumia nguvu kubwa sana kuuelezea Umma kuwa matatizo yote kuanzia maji, afya, elimu na uchumi yana/yameletwa na Tundu Lissu. Wanajitahidi kuuonyesha Umma kuwa ni kosa kubwa sana kwa Tundu Lissu kuvuta hii hewa ambayo tumepewa Bure na Mwenyezi Mungu.
Kiongozi yeyote mwenye kaliba na CCM kuanzia serikalini mpaka michezoni asipomnanga Lissu katika hotuba yake anaonekana bado kama hajaongea kitu.

Naomba Watanzania na wanaCCM kwa ujumla tufike mahali tuone hii nchi ni yetu sote. Na maendeleo ya hii nchi yataletwa na sisi watanzania wote bila kujali itikadi zetu zakisiasa. Kama tumeukubali mfumo wa vyama vingi pia tukubali kutofautiana kwa mawazo ili tuweze kujenga nchi yetu. Kumnyooshea kidole Tundu Lissu hakutapunguza tatizo la maji, wala hakutaongeza madawa katika hosipitali zetu wala hakutaongeza ufaulu katika shule zetu bali tunaendeleza chuki na hasira kati ya watanzania sisi kwa sisi na kuongeza wigo wa kumegua umoja na Utanzania wetu.

Wasalaamu Jumapili njema.
 
Pengo la akina kinana na akina Nape bado litaendelea kuonekana!

ccm ile ya wajenga hoja hata kama zilikua za uongo imekufa kabisa!

Yaani chama + vyombo vya dola bado kwa ujengaji hoja lissu amewazidi mbaaaali
 
Tatizo ni Kiburi ndo kinaiua CCM. Tuliwambia mapema Polepole hana mapafu ya kukimbizana na akina Lissu wakabisha. Saiv CCM kila mtu analia Lissu Lissu Lissu....kuanzia mwenyekiti, katibu hadi TFF nakati ilikua ni kaz ndogo sana kwa kada kama Nape

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni
Wasalaam wana jukwaa.
Leo ni siku muhimu sana kwa wanaCCM kote nchini katika kuelekea Kilele cha miaka 42 ya kuzaliwa chama hiki kikongwe kabisa barani Africa na duniani kwa ujumla. Katika hekaheka zangu kwenye mitandao ya kijamii na mikusanyiko tofauti ya uzinduzi wa sherehe hizi hii leo, nimegundua kuwa CCM kama chama tawala na Chama kongwe wametumia muda wao karibia 90% kumnanga mnadhimu mkuu wa upinzani na Mwanasheria wa CHADEMA na pia Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kama ndiye Chanzo cha CCM kushindwa kutekeleza majukumu yao.

Jambo hili limefikia kiwango cha viongozi wa CCM Kuanzia katibu Mkuu mpaka kiongozi wa shina kupandikiza chuki kubwa sana kwa WanaCCM na Watanzania kwa ujumla kuwa adui mkubwa wa nchi hii ni Tundu Lissu. CCM wanatumia nguvu kubwa sana kuuelezea Umma kuwa matatizo yote kuanzia maji, afya, elimu na uchumi yana/yameletwa na Tundu Lissu. Wanajitahidi kuuonyesha Umma kuwa ni kosa kubwa sana kwa Tundu Lissu kuvuta hii hewa ambayo tumepewa Bure na Mwenyezi Mungu.
Kiongozi yeyote mwenye kaliba na CCM kuanzia serikalini mpaka michezoni asipomnanga Lissu katika hotuba yake anaonekana bado kama hajaongea kitu.

Naomba Watanzania na wanaCCM kwa ujumla tufike mahali tuone hii nchi ni yetu sote. Na maendeleo ya hii nchi yataletwa na sisi watanzania wote bila kujali itikadi zetu zakisiasa. Kama tumeukubali mfumo wa vyama vingi pia tukubali kutofautiana kwa mawazo ili tuweze kujenga nchi yetu. Kumnyooshea kidole Tundu Lissu hakutapunguza tatizo la maji, wala hakutaongeza madawa katika hosipitali zetu wala hakutaongeza ufaulu katika shule zetu bali tunaendeleza chuki na hasira kati ya watanzania sisi kwa sisi na kuongeza wigo wa kumegua umoja na Utanzania wetu.

Wasalaamu Jumapili njema.

Nimemsikiliza Bashiru Allƴ ƴule katibu mkuu wa CCM, hana hoja analilia majeshi ƴanusuru chama chake!

Majeshi yajitenge na CCM! Yanachafuka yanapoɓeɓa uchafu wa CCM! CCM iachwe ipambane na hali ƴake!
 
Ndomaana nikasema sasa hivi siasa za hoja naona kama zimepitwa na wakati hapa nchini. Nashangaa leo mtandaoni kuna juhudi kubwa sana za kuhakikisha kuwa Lissu ndiye mbeba madhambi ya hii nchi. Napenda kuwaambia CCM kwa siasa hizi hatutafika kama taifa.
 
Vp fomu ya urais atachukua au ndio naye ameshanunuliwa!?...
Lisemwalo lipo kama.... 👇 👇 👇
images (4).jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom