kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 8,990
- 17,869
Mamilioni ya Wairani washiriki maandamano ya kuadhimisha miaka 40 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Feb 11, 2019 08:06 UTC
Mamilioni ya wananchi Waislamu wa Iran wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika maandamano ya kuadhimisha miaka 40 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Licha ya kibaridi, manyunyu na theluji kushuhudiwa nyakati za asubuhi katika baadhi ya miji ukiwemo mji mkuu Tehran, lakini Wairani wamejitokeza kwa wingi katika maandamano hayo, kudhihirisha utiifu wao kwa malengo ya Mwasisi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Khamenei.
Katika mahojiano yaliyochapishwa leo na gazeti la New Yorker la Marekani, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif alitoa ujumbe wake kwa mnasaba wa siku hii inayofahamika hapa nchini kama Siku ya Allah ya Bahman 22 na kusema kuwa, "Mafanikio makubwa ya Mapinduzi ya Kiislamu ni kuwapa sauti wananchi wa Iran kuhusiana na masuala ya ndani na nje ya nchi."
Maandamano ya leo ya maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka huu yanafanyika katika miji zaidi ya elfu moja na vijiji elfu kumi vya Iran ya Kiislamu.
Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalifikia kilele cha ushindi tarehe 11 mwezi Februari mwaka 1979 kwa uongozi wa Imam Khomeini (M.A), Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Februari 11 miaka 40 iliyopita Iran ilikuwa katika siku ya kihistoria itakayokumbukwa siku zote, ambapo wananchi wanamapinduzi wa Iran, wanaume kwa wanawake, vijana kwa wazee na watu wa matabaka yote walisimama kidete wakipambana na mizinga na vifaru vya jeshi la Shah na kujisabilia kwa ajili ya Mapinduzi ya Kiislamu.
Viongozi na maafisa wa ngazi za juu serikalini wanatazamiwa kutoa hotuba mbalimbali kwa mnasaba wa siku hii.
Swali:Jee marekani na israel wameshindwa kuiangusha iran kwa miaka 40 sasa?Maana vikwazo vimefeli na hata kijeshi ni ngumu maana iran wamejiimarisha mno
Sent using Jamii Forums mobile app