Miaka 40! Mtambuzi naelekea uzeeni sasa

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,379
Tarehe kama ya leo, ndio siku ambayo nilizaliwa na kuongeza idadi ya watu hapo Duniani. Si haba, namshukuru muumba kwa kunifikisha hapa nilipo. Pia nawashukuru wazazi wangu, mke wangu mpendwa mama Ngina, na Wanangu Ngina, Ngano na Ngadu, bila kuwasahau wana JF, mahali ambapo pananisaidia kupunguza stress zangu za maisha…………..LOL

Tupo pamoja………………….

Hongera sana...Mungu akujalie nguvu uishi tena miaka mingine zaidi ya hii uliyonayo!
 
hongera sana kwa kusherehekea siku ya kuzaliwa. kwa kuanzia, hebu muulize ngina atafanyeje, kama akipewa chance, kuadhimisha siku muhimu ya dadii kuzaliwa, uone atakavyokupa idea za ajabu. Mungu awajaalie maisha marefu yenye amani
 
Ahsante King'asti. Huyo Ngina ndiye ananipa PRESHA, naogopa hata kumuuliza, maana anaweza kunigeuzia kibao kwa maswali mpaka nitakereka.............
 
hongera mkuu kwa kukimbilia uzeeni kwani pia unakaribia ku-RIP

Yeah! hata hivyo si haba, namshukuru Mungu kwa kuendelea kunipa pumzi yake ya bure..............
 
Tarehe kama ya leo, ndio siku ambayo nilizaliwa na kuongeza idadi ya watu hapo Duniani. Si haba, namshukuru muumba kwa kunifikisha hapa nilipo. Pia nawashukuru wazazi wangu, mke wangu mpendwa mama Ngina, na Wanangu Ngina, Ngano na Ngadu, bila kuwasahau wana JF, mahali ambapo pananisaidia kupunguza stress zangu za maisha…………..LOL

Tupo pamoja………………….

Ebwanaeee hongera sana!!!!!
 
Ahsante King'asti. Huyo Ngina ndiye ananipa PRESHA, naogopa hata kumuuliza, maana anaweza kunigeuzia kibao kwa maswali mpaka nitakereka.............

hapa ndo nafasi pekee ya kumchallenge Ngina ... mwambia akupe plan nzima ya siku na shughuli iweje
 
Hongera sana Baba Ngina! Mungu akupe maisha marefu na yenye mafanikio.
 
Tarehe kama ya leo, ndio siku ambayo nilizaliwa na kuongeza idadi ya watu hapo Duniani. Si haba, namshukuru muumba kwa kunifikisha hapa nilipo. Pia nawashukuru wazazi wangu, mke wangu mpendwa mama Ngina, na Wanangu Ngina, Ngano na Ngadu, bila kuwasahau wana JF, mahali ambapo pananisaidia kupunguza stress zangu za maisha…………..LOL

Tupo pamoja………………….

Binti yako hajambo?
Nina kijana ana mzidi mwanao miaka minne, trully wana tabia zinazo fanana.
Nahisi wanafaana kwa maisha ya baadae.
Happy best day Mtambuzi
 
hongera mkuu,nahisi umejitahidi ku-look after yourself

Yeah, nimeanza kusikia habari za Ukimwi tangu nikiwa Shule ya Msingi, na mpaka sasa zaidi ya miaka 30, tangu kuufahamu Ukimwi, bado nadunda tu........., nimejitahidi kwa kweli maana Balehe ikikujia vibaya unasahaulika mapema........................
 
Wewe ni age-mate, na huenda ninakuzidi kidooogo!
Ila huyo mwanao Ngina fanya kumdhibiti bana!...kawaida masikio hayapiti kichwa!
 
Hongera mkubwa,
Ukipiga 40 nyingine na ukiongeza nyingine tena itakuwa vyema.
OTIS.
 
Yeah, nimeanza kusikia habari za Ukimwi tangu nikiwa Shule ya Msingi, na mpaka sasa zaidi ya miaka 30, tangu kuufahamu Ukimwi, bado nadunda tu........., nimejitahidi kwa kweli maana Balehe ikikujia vibaya unasahaulika mapema........................

Mkuu nakuzidi mwaka mmoja,ebu niambie ulaji wako ukoje,je una kitambi,beer vipi unakunywa sana?nyama choma?mazoezi ya viungo,mastrees yanakusumbua?
 
Haaah! Mtambuzi na hizo threads zako, nikadhani uko over 40 kumbe mpaka jana hata 40 ulikuwa hujaifikisha.....lol! Heheheheheee! Hongera yako mkuu, hata hivo umesogea!
 
Similar Discussions

9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom