Miaka 4 baadaye: Kikwete vunja bodi ya Mikopo!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Habari Leo

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, imekataa taarifa iliyowasilishwa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa kuitaka menejimenti ikutane nayo mwezi ujao Dodoma kujadili namna ya kuiendesha kwa tija na ufanisi.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Estheria Kilasi, alisema jana Dar es Salaam kuwa kamati haikukubaliana na maelezo ya uongozi wa Bodi hiyo kuhusu utekelezaji wa maelekezo waliopewa katika kikao kilichopita.

Kilasi, ambaye ni Mbunge wa Mbarali, alisema Bodi imeshindwa kutoa maelezo ya kuridhisha kuhusu matumizi, ukusanyaji usioridhisha wa mapato, na kushindwa kutoa taarifa iliyokamilika.

Kwa mujibu wa Kilasi, matumizi ya jumla na kiwango cha fedha kilichotumika kwa ajili ya posho ni kikubwa. Kasoro nyingine zilizoainishwa na kamati ni pamoja na Bodi hiyo kushindwa kukusanya madeni kutoka kwa watu waliopata mkopo kutoka kwenye Bodi hiyo.

Kamati pia ilieleza kushangazwa na kitendo cha Bodi kushindwa kutoa maelezo kuhusu namna mkopo wa Sh bilioni 58 kutoka Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) unavyolipwa.

Jambo lingine lililofanya kamati ikatae ripoti ni kutokana na kile ambacho Kilasi alisema HESLB imeshindwa katika ripoti yake kutoa maelezo ya namna ambavyo watatumia Sh bilioni 21 zilizoahidiwa kutolewa na Wizara ya Fedha na Uchumi.

Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti huyo, wakati wa Mkutano wa Bunge ujao, watakaa na viongozi wa Bodi katika kikao kitakachomshirikisha pia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na Waziri wa Fedha na Uchumi.

Lengo la kikao hicho ni kujadili namna ya kusaidia bodi hiyo kufanya kazi kwa ufanisi na tija.

Wakati huo huo, Kamati imeitaka Bodi kumthibitisha Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Yusuf Kisare katika nafasi hiyo baada ya kubaini kwamba tangu Januari 2007 amekuwa akikaimu.

Mkurugenzi wa HESLB, George Nyantega aliieleza kamati kwamba walishawasilisha majina Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa ajili ya kupata mhusika, lakini hadi sasa hawajapata jibu.

My Take:
Hivi uzembe unatakiwa uvumiliwe hadi miaka mingapi? Kweli mnafikiria watu wale wale watabadilika na mara moja kuwa watendaji kazi wazuri mkiwapa fedha zaidi!? Please Mr. President, just sack this stupid board, would you?
 
bodi ya mkopo ni chombo muhimu sana katika kuwezesha watanzania wa hali ya chini kumdu elimu ya juu. pamoja na matatizo yake, si busara kushauri ivunjwe bila kuleta wazo mbadala litakaloondoa mapungufu yanayoonekana katika bodi kwa sasa. kumbuka kuwa kama majukumu ya utoaji mikopo yatarudishwa wizarani, basi tunaweza kushuhudia madudu mengi zaidi ya tunayoyaona sasa.

hayo yaliyoripotiwa ni baadhi tu, ukiangalia ripoti nyingine unawza kusema kuwa angalau hayo yana nafuu na ufanisi wake unaoneana.
 
Najua uozo wa bodi hii kwa undani; ninaposema aivunje manake iundwe nyingine ya muda ili hatimaye tuunde Mamlaka ya Mikopo ya Elimu (Education Loans Authority) ambayo itafanya kazi tofauti na uozo huu!
 
nafikiri unazungumzia masuala ya kimuundo tu. kwani bodi na mamlaka bado kimsingi ni vyomba mahsusi vya utekelezaji japo vinatofautiana kwa misingi ya sheria za uundwaji wake. tunaweza kuchagua kubadili muundo wa bodi hii au hata kufanya mabadiliko ya sheria kuiimarisha na ikafanikiwa kupunguza madudud iliyonayo sasa.

pia unaweza kukuta mamlaka imeanzishwa lakini watuwakawa walewale ama tofauti lakini kutoka kada ileile. hapo uwezekano wa tofauti unaweza kuwa mdogo sana.

muhimu mi naona kila mhusika atekeleze wajibu wake na tuanza kujenga utamaduni wa kuwajibishana bila koneana haya. katika taasisi yoyote ya umma ukikuta pasho zimekuwa nyingi hadi zinaleta shaka, basi ujue tatizo namba moja pale ni maadili ya uongozi
 
Please Mr. President, just sack this stupid board, would you?
. Mzee Mwanakijiji, stupid are the people on that board, not the body. Bodi ni mzuri na malengo yake ni mazuri ila haijapata watu.

Hii kamati nayo!. Haukuridhishwa na madudu ya bodi kutokana na maroroso ya fedha, halafu inapiga chapuo kinara wa fedha athibitishwe kazini!. Kukaimu kwa mujibu wa sheria mwisho ni miezi 9 baada ya hapo au unathibitishw au unapigwa chini. Hivi hiyo kamati si ingeuliza baada ya kutothibitishwa kwa zaidi ya miaka 2 kwanini hajapigwa chini, leo inataka athibitishwe aendeleze maroroso.

Naisikitikia hii bodi, haina uwezo kutrack down madeni ya nyuma, eti wanatoa majina ya wadaiwa sugu magazetini ili iweje?!.

Hii bodi ni ya kuimarishwa kila Mtanzania alipiwe elimu kama haki yake na sio favour kama ilivyo sasa. Wako watoto wa wenye uwezo wanalipiwa shule nchi za neeme, huku watoto wa masikini wakinyimwa mikopo na wengine kutelekezwa kama wale vijana wa Urusi.

Usiendelee kumuomba mkulu aivunje, tuimarishe mapambano ili aje mtu mwenye guts kusafisha uozo wote huuu uliopo, na sio bodi tuu, infact ni kuclear nyumba nzima maana saa hizi ni jalala!.
 
nafikiri unazungumzia masuala ya kimuundo tu. kwani bodi na mamlaka bado kimsingi ni vyomba mahsusi vya utekelezaji japo vinatofautiana kwa misingi ya sheria za uundwaji wake. tunaweza kuchagua kubadili muundo wa bodi hii au hata kufanya mabadiliko ya sheria kuiimarisha na ikafanikiwa kupunguza madudud iliyonayo sasa.

pia unaweza kukuta mamlaka imeanzishwa lakini watuwakawa walewale ama tofauti lakini kutoka kada ileile. hapo uwezekano wa tofauti unaweza kuwa mdogo sana.

muhimu mi naona kila mhusika atekeleze wajibu wake na tuanza kujenga utamaduni wa kuwajibishana bila koneana haya. katika taasisi yoyote ya umma ukikuta pasho zimekuwa nyingi hadi zinaleta shaka, basi ujue tatizo namba moja pale ni maadili ya uongozi

sizungumzii mabadiliko ya muundo tu, nazungumzia kuwatimua wanabodi wote, na ikiwezekana kuwatupa kwenye genge! Halafu kuwaweka watu ambao wanajua nini maana ya kutoa mikopo ya elimu!!
 
. Mzee Mwanakijiji, stupid are the people on that board, not the body. Bodi ni mzuri na malengo yake ni mazuri ila haijapata watu.

the board is stupid kwa sababu walioandika sheria yake waliandika kama wamelewa ugimbi! Umeshasoma sheria ya bodi ya mikopo?

Naisikitikia hii bodi, haina uwezo kutrack down madeni ya nyuma, eti wanatoa majina ya wadaiwa sugu magazetini ili iweje?!.

you didn't know.. it was pre-emptying the committee.

Hii bodi ni ya kuimarishwa kila Mtanzania alipiwe elimu kama haki yake na sio favour kama ilivyo sasa. Wako watoto wa wenye uwezo wanalipiwa shule nchi za neeme, huku watoto wa masikini wakinyimwa mikopo na wengine kutelekezwa kama wale vijana wa Urusi.

Nope ni ya kuvunjwa na sheria yake kubadilishwa.. believe me.. naweza kuandika sheria ya mikopo ya elimu ambayo itampa utu na heshima kila kijana na mtanzania yoyote anayetaka elimu ya juu!

Usiendelee kumuomba mkulu aivunje, tuimarishe mapambano ili aje mtu mwenye guts kusafisha uozo wote huuu uliopo, na sio bodi tuu, infact ni kuclear nyumba nzima maana saa hizi ni jalala!.

I'm very serious.. leo nimerudia tu! They know why..
 
Mara nyingi wanaoharibu mambo ni hawa "wateule" wetu. Jeshini wanaitwa special forces( RED BERRET), maana kuna watu wako pale, kwasababu ya connection zao, wamejisahau kabisa kama wanawatumikia watanzania.
Siku tutakapoanza kufunga wafujaji wa mali ya umma ndio tunaweza kuona mabadiliko. Deal siku hizi ni kufuja ili mradi una God Father basi mambo hayatasumbua.
 
the board is stupid kwa sababu walioandika sheria yake waliandika kama wamelewa ugimbi! Umeshasoma sheria ya bodi ya mikopo?

you didn't know.. it was pre-emptying the committee.

Nope ni ya kuvunjwa na sheria yake kubadilishwa.. believe me.. naweza kuandika sheria ya mikopo ya elimu ambayo itampa utu na heshima kila kijana na mtanzania yoyote anayetaka elimu ya juu!

I'm very serious.. leo nimerudia tu! They know why..

Huwezi kuandika sheria ya mikopo MMKJ haya unayasema tu hapa, hii bodi inajitahidi sana wakati huo mikopo ilipokuwa Chini ya wizara ya Elimu ya Juu madudu yaliyokuwa yanafanyika hapo huwezi kuelezea tulikuwa kila kukicha tuna kwenda pale wizarani aidha jina halipo au umelipwa mara mbili, unaweza kulipwa leo lakini ukienda wizarani na ku claim hujapata unapewa tena cheque walikuwa so dis-organized ukilinganisha na sasa.

Sielewi kama kweli unailewa vizuri bodi na inavyoendeshwa kama unavyodai, tusiilaumu sana bodi kwa mambo ya kiujumla jumla tu kama ni hivyo ni bodi ngapi zilizovurunda zitavunjwa let be realistic kweli wanajitahidi achilia mbali matatizo madogo madogo yanayojitokeza, ina wanafunzi wengi wa kuwahudumia zaidi ya 10,000 ukilinganisha na 2,000 tu mwaka 1992 wakati mikopo ikiwa chini ya wizara, angalia kwanza uzito wa kazi na mahitaji menyewe unaweza kuilaumu bodi kumbe uwezo wa kuiwezesha ifanye kazi ni mdogo mahitaji yanaweza kuwa makubwa kuliko uwezo.
 
nimekusoma vizuri; hii bodi ni ya kuvunjwa tu kuundwa upya, na wote ambao wanafanya kazi hiyo sasa kutafuta ajira mpya, na kuanza upya. Hatuwezi kuendeleza uzembe ule ule tukitarajia mabadiliko. Nyie watafutieni udhuru na maelezo ya kwanini ni wazembe; at the end of the day tungekuwa na kiongozi makini wangekwishatimuliwa siku nyingi.
 
Ana list ndefu sana ya ku-suck huyu jamaa so far inaonekana the whole sector to do with finance and economic advise has to go. Ndio mafisadi wanafungwe lakini hawa jamaa nao wana play a huge role kushinda hao mafisadi in contributing to our poverty. Lastly aitakua mbaya na yeye Mr.President akiamua ku-resign just a thought to think about.
 
Habari Leo

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, imekataa taarifa iliyowasilishwa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa kuitaka menejimenti ikutane nayo mwezi ujao Dodoma kujadili namna ya kuiendesha kwa tija na ufanisi.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Estheria Kilasi, alisema jana Dar es Salaam kuwa kamati haikukubaliana na maelezo ya uongozi wa Bodi hiyo kuhusu utekelezaji wa maelekezo waliopewa katika kikao kilichopita.

Kilasi, ambaye ni Mbunge wa Mbarali, alisema Bodi imeshindwa kutoa maelezo ya kuridhisha kuhusu matumizi, ukusanyaji usioridhisha wa mapato, na kushindwa kutoa taarifa iliyokamilika.

Kwa mujibu wa Kilasi, matumizi ya jumla na kiwango cha fedha kilichotumika kwa ajili ya posho ni kikubwa. Kasoro nyingine zilizoainishwa na kamati ni pamoja na Bodi hiyo kushindwa kukusanya madeni kutoka kwa watu waliopata mkopo kutoka kwenye Bodi hiyo.

Kamati pia ilieleza kushangazwa na kitendo cha Bodi kushindwa kutoa maelezo kuhusu namna mkopo wa Sh bilioni 58 kutoka Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) unavyolipwa.

Jambo lingine lililofanya kamati ikatae ripoti ni kutokana na kile ambacho Kilasi alisema HESLB imeshindwa katika ripoti yake kutoa maelezo ya namna ambavyo watatumia Sh bilioni 21 zilizoahidiwa kutolewa na Wizara ya Fedha na Uchumi.

Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti huyo, wakati wa Mkutano wa Bunge ujao, watakaa na viongozi wa Bodi katika kikao kitakachomshirikisha pia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na Waziri wa Fedha na Uchumi.

Lengo la kikao hicho ni kujadili namna ya kusaidia bodi hiyo kufanya kazi kwa ufanisi na tija.

Wakati huo huo, Kamati imeitaka Bodi kumthibitisha Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Yusuf Kisare katika nafasi hiyo baada ya kubaini kwamba tangu Januari 2007 amekuwa akikaimu.

Mkurugenzi wa HESLB, George Nyantega aliieleza kamati kwamba walishawasilisha majina Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa ajili ya kupata mhusika, lakini hadi sasa hawajapata jibu.

My Take:
Hivi uzembe unatakiwa uvumiliwe hadi miaka mingapi? Kweli mnafikiria watu wale wale watabadilika na mara moja kuwa watendaji kazi wazuri mkiwapa fedha zaidi!? Please Mr. President, just sack this stupid board, would you?

Hapa tupo pamoja kabisa..Na ujinga mkubwa nafikiri ulianza baada ya Waziri aliyepita kujaza ndugu zake na watu wasiokuwa hata na experience na kazi yenyewe.

Tatizo la Tanzania nafikiri bado hatutaki kukubali ukweli kwamba kama watu hawafai jamani hawafaii tuu mbona wapo wengi sana wanaoweza kufanya hizi kazi. Inabidi kubadilika sana bila ya hivyo tutakuwa tunaona uozo kila siku
 
Ndio maana nashangaa jinsi watu wanavyotafutia uzembe maelezo:

a. wamejenga nyumba mbili kwa mabilioni, tunafafanua kuwa "wanastahili"
b. ATCL wamevurunda, tunakubali kuwa tatizo ni kuwa hawana fedha ya kutosha!
c. nikiendelea hapa naweza kuvunja hii screen ..
 
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, imekataa taarifa iliyowasilishwa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa kuitaka menejimenti ikutane nayo mwezi ujao Dodoma kujadili namna ya kuiendesha kwa tija na ufanisi.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Estheria Kilasi, alisema jana Dar es Salaam kuwa kamati haikukubaliana na maelezo ya uongozi wa Bodi hiyo kuhusu utekelezaji wa maelekezo waliopewa katika kikao kilichopita.

Kilasi, ambaye ni Mbunge wa Mbarali, alisema Bodi imeshindwa kutoa maelezo ya kuridhisha kuhusu matumizi, ukusanyaji usioridhisha wa mapato, na kushindwa kutoa taarifa iliyokamilika.

Kwa mujibu wa Kilasi, matumizi ya jumla na kiwango cha fedha kilichotumika kwa ajili ya posho ni kikubwa. Kasoro nyingine zilizoainishwa na kamati ni pamoja na Bodi hiyo kushindwa kukusanya madeni kutoka kwa watu waliopata mkopo kutoka kwenye Bodi hiyo.

Kamati pia ilieleza kushangazwa na kitendo cha Bodi kushindwa kutoa maelezo kuhusu namna mkopo wa Sh bilioni 58 kutoka Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) unavyolipwa.

Jambo lingine lililofanya kamati ikatae ripoti ni kutokana na kile ambacho Kilasi alisema HESLB imeshindwa katika ripoti yake kutoa maelezo ya namna ambavyo watatumia Sh bilioni 21 zilizoahidiwa kutolewa na Wizara ya Fedha na Uchumi.

Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti huyo, wakati wa Mkutano wa Bunge ujao, watakaa na viongozi wa Bodi katika kikao kitakachomshirikisha pia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na Waziri wa Fedha na Uchumi.

Lengo la kikao hicho ni kujadili namna ya kusaidia bodi hiyo kufanya kazi kwa ufanisi na tija.

Wakati huo huo, Kamati imeitaka Bodi kumthibitisha Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Yusuf Kisare katika nafasi hiyo baada ya kubaini kwamba tangu Januari 2007 amekuwa akikaimu.

Mkurugenzi wa HESLB, George Nyantega aliieleza kamati kwamba walishawasilisha majina Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa ajili ya kupata mhusika, lakini hadi sasa hawajapata jibu.
 
Mimi hawa jamaa niliwakopa kweli wakati nikisoma miaka ile lakini kwa kweli siwezi kuwalipa ata waseme nini kwa kuwa sioni uwajibikaji wao wala sionikwa nini niwalipe watu ambao wanalipana perdiem ya laki tatu kwa siku kwa maofisa wa jkawaida wanapoenda kukagua wanafunzi waliowakopesha mikoani.hawas ni genge jipya la wwezi nchini mwetu
 
Back
Top Bottom