Miaka 33 baadae, Huyu ndiye Jenny wa Arnold Schwazenegger

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,713
45,090
Miaka 33 baada ya kuekti movie ya Commando, huyu ndiye Alyssa Milano maarufu kama Jenny aliyeekti kama mtoto wa Arnold, ambapo alitekwa na ikabidi Arnold atumie maarifa yake ya kikomando ili kwenda kumkomboa kutoka kwa maadui.
alyssa-milano.jpg


Alyssa-Milano-appelle-les-victimes-de-violences-sexuelles-a-parler-avec-le-hashtag-MeToo_news_full.jpg


Hapa chini ni picha yake akiwa katika sehemu ya movie hiyo, akiwa kabebwa na baba yake.
aba333625ed3161eb75aa1455be0b64f.jpg


Wahenga mpo? unakumbuka wapi kuhusu movie ya Commando?
 
Nakumbuka tulikua tunaambiwa tukaoge ndio turuhusiwe kwenda kuangalia movie hii kwa tajiri wa kijiji wakati huo...tajiri wa kijiji alikua na movie kali sana

Commando(Arnold)
Solo
The bridge of dragon(dolph)
Delta force(norris)
Predator (arnold)
Ghost dog(forest Whitaker)
The silencers (jack skalia)
Lucky seven
Londolozi(picha ya wanyama)
 
Nakumbuka tulikua tunaambiwa tukaoge ndio turuhusiwe kwenda kuangalia movie hii kwa tajiri wa kijiji wakati huo...tajiri wa kijiji alikua na movie kali sana

Commando(Arnold)
Solo
The bridge of dragon(dolph)
Delta force(norris)
Predator (arnold)
Ghost dog(forest Whitaker)
The silencers (jack skalia)
Lucky seven
Londolozi(picha ya wanyama)
The hard way
 
Steven Seagal anapewa sifa asizostahili.
Chuck Norris ni mwamba wa ukweli.

Lakini wote ni wataalam wa judo.

Chuck Norris ni Kodokan judo yaani kukamatana na kuangushana chini na Ukiangalia movie nyingi za Norris awafanyia maadui wake mchezo huu wa kuwaangusha chini na kuwamaliza.

Steven Seagal ni Aikido dojo mtindo ambao mtu unakuwa unajilinda dhidi ya adui lakini wakati huohuo unahakikisha pia humdhuru sana adui yako ila unamwadhibu.

Ndio maana Steven Seagal mara nyingi anakuwa anapenda kuwazaba makofi maadui zake au anajaribu kuwadhibiti kwa namna ya kujikoa yeye zaidi bila kumvamia adui na kumshambulia kama afanyavyo Chuck Norris.

Ila hawa wawili kwa maisha halisi ni wataalam wa judo na Steven Seagal ni rafiki mkubwa na Vladimir Putin mpaka Ptutin amemteua kuwa balozi maalum wa Russia nchini Marekani.

Vladimir Putin nae ni mtaalam wa judo 8th Degree Black Belt na pia Taekwondo na ana mkanda mweusi wa daraja la 9 au "9th Degree Black Belt".

NB:

Kipimo cha ufanisi wa kucheza judo kinaitwa Dan na kina ngazi 1 hadi 10

Vladmir Putin ana hiyo ngazi ya 9, akifuatiwa na Chuck Norris ngazi ya 8 au "8th Degree Black Belt" na Steven Seagal ngazi ya 7 au "7the Black Belt".
 
Back
Top Bottom