Miaka 30 ya Mfumo wa Demokrasia na Vyama Vingi Tanzania: Mjadala wa Mafanikio na Changamoto za Kidemokrasia, Utawala wa Sheria na Ushiriki wa Umma

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,877
Kongamano la kujadili Mafanikio na Changamoto za Kidemokrasia, Utawala wa Sheria na Ushiriki wa Umma, Dar es Salaam.

GEOPHREY PINDA (NAIBU WAZIRI KATIBA NA SHERIA): Tanzania hakuna Sheria mbovu, bali tuna Sheria zilizopitwa na wakati, zinazohitaji kufanyiwa marekebisho ili kuendana na wakati tuliopo

KAIZA BUBERWA: Miaka ya zamani Vyama vya siasa vilipoteza dira baada ya kuweka nguvu nyingi kwenye kutaka kuiondoa CCM madarakani. Wakati huo huo wanufaika wa CCM wakizuia kwa nguvu kutoondolewa Madarakani

JENERALI ULIMWENGU: Miaka mitano ya Magufuli ilijaa ukandamizaji uliopitiliza. Tulishuhudia utawala wa mtu mmoja ukibadili sheria na katiba. Hakujali Katiba ilisema nini. Uzuri alikua mkweli, alisema waziwazi hataki vyama vingi

Magufuli aliamua Wabunge watakao ingia Bungeni yeye mwenyewe, Takwimu zilikuwa ni haramu kama hazikutolewa na Serikali, Azaki zilishindwa kufanya kazi, katika awamu yake wajinga waliibuka kwa wingi na kujiona bora

Lazima tukubali kuwa bado tupo pabaya na tunahitaji kujitafakari tumefikaje hapa, tuangalie kama kuna mtu tuliyemuumiza katika kupotea kwetu. Tujue namna gani ya kuponya mioyo iliyoumia la si hivyo maridhiano hayatakuwa na tija

Rais Samia ameonyesha nia ya kuleta maridhiano. Nasi tuunge Mkono juhudi hizo lakini tunapaswa kufanya hivyo kwa umakinifu ili tusirudi tulipotoka

HAMAD RASHID MOHAMED (ADC): Wanasiasa wa Upinzani kukosa ushirikiano wenyewe kwa wenyewe ni chanzo kikuu cha kukosekana kwa Upinzani imara nchini

Udhaifu wetu mkubwa ni kukosa umoja

JOHN MNYIKA (CHADEMA): Kuingia kwenye mfumo wa Vyama vingi kulipaswa kutanguliwa na mfumo unaoruhusu uwepo wa vyama vingi.

Sasa ni miaka 30 ya Vyama vingi lakini bado hakuna katiba inayoruhusu mfumo wa vyama vingi nchini

Ukosefu wa Katiba Mpya ni Mzizi wa Matatizo. Vyama vya Siasa havina ruhusa ya kufanya mikutano ya Hadhara pamoja na kuwa na Sheria zinaruhusu hili. Pamoja na mabadiliko ya kiutawala bado katazo hili linaendelea

HAMAD RASHID MOHAMED (ADC): Katiba sio mwarobaini bali utashi ndio unatakiwa, nilimwambia Mnyika 'hamuwezi kuandamana kama tulivyokuwa tunafanya sisi'

Nilikuwa tayari kukaa ndani kutetea wenzangu, lakini wao wakisikia kuna kukamatwa watakimbia watajificha uvunguni

FATMA KARUME: Uchaguzi wa 2020 ulikuwa wa hovyo kuliko chaguzi zote zilizopita. Hakujawahi kutokea chaguzi yoyote tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe kusiwe na kesi Mahakamani isipokua wa 2020, na hii ni kwa sababu watu hawana imani na Mahakama

Tumetengeneza Mhimili wa Mahakama usioweza kufanya kazi yake, Rais kuwa na Uwezo wa Kumteua na Kumuondoa Jaji Mkuu kunaondoa Uhuru wa Mahakama

Pia Mahakama kutegemea bajeti ya Serikali kufanya shughuli zake hudunisha uhuru wa Mahakama

JAJI MSTAAFU ROBERT MAKARAMBA: Wale ambao hawapaswi kutunga Sheria ndio wanatunga Sheria, ambao hawapaswi kutafsiri ndio wanatafsiri Sheria

Ndio maana mnasikia mtu anasema ‘Nitakuweka ndani’, yaani anakuwa Sheria, Mahakama na Polisi kitu ambacho tulipiga marufuku

Lazima kuwe na usawa, mfano neno gender lilikuwemo kwenye Katiba yetu likaondoshwa, Wanasiasa wanashindwa kutofautisha kati ya sex na gender

Sex ni biological, gender ni social concern, sasa hivi limebaki neno sex peke yake

Kudhibiti matumizi mabaya ya madaraka, hii inaanzia ngazi ya familia, kinachotoka kwenye familia ndicho kinachoakisi jamii yetu

Mfano Mkuu wa Wilaya au Mkoa anamuweka mtu ndani akiwa hajui umefanya kosa gani

Uvunjani na ukiukwaji wa Haki za Binadamu ngazi ya binafsi ndani ya jamii zetu ni mkubwa sana, hilo tuliangalie

Umoja wa Mataifa umeshaandaa Kanuni za kuongoza biashara katika kuheshimu Haki za Binadamu

ADO SHAIBU (ACT WAZALENDO): Vyama vya Siasa viwajibike kutengeneza mazingira bora ya Ushiriki wa Wanawake

Demokrasia isipoimairishwa, Siasa zikiendelea kuwa za piga ua, za baruti, za mabomu za kukimbizana itawafanya Wanawake washindwe kushiriki Kisiasa
 
Huyo mpuuzi Hamad Rashid anataka ushirikiano upi wa wapinzani? Ushirikiano na akina nani? Yeye? Au na akina Lipumba ambao pamoja na uprofesa bado ni mlafi hata wa sambusa?

Huwezi fanya ushirika na watu wa hovyo kama kina Zitto, Hamad, Lipumba et al, watu wapuuzi na hovyo ambao hata ubwabwa kwao huwachukulia akili yao na hulka za uroho na tamaa. Huyo Lipumba ulimi wake muda wote ansupepesa kama mamba leo ushirikiane nae si ndio atakuuza mbele ya sinia ya pilau?
 
Huyo mpuuzi Hamad Rashid anataka ushirikiano upi wa wapinzani? Ushirikiano na akina nani? Yeye? Au na akina Lipumba ambao pamoja na uprofesa bado ni mlafi hata wa sambusa?
Kila mpinzani ni mlafi. Mpinzani hujinasibu kama mpinzani pale mrija wake binafsi unapominywa.
 
Jenerali anaposema Magufuli hakujali katiba mbona anatofautiana na chadema wanaosema katiba hii iliyopo mbovu ndio ilimpa Magu madaraka makubwa.?
Mkuu ndio raha ya debate!,mnapotofautiana kihoja ndio Safi maana more facts zinatolewa, mjadala wa upande mmoja unapoteza Ile vavumaaa ya topic
 
Kila mpinzani ni mlafi. Mpinzani hujinasibu kama mpinzani pale mrija wake binafsi unapominywa.
Sio wote walafi, na hata ulafi pia hutofautiana. Unafikiri Samia anaweza mshawishi Mbowe kwa sinia ya Sambusa kama afanyavyo kwa Lipumba?

Magufuli alitaka mnunua Mnyika kwa sh. Ngapi na kijana alikataa?
 
Jenerali Ulimwengu ni babu anayewapa wakati mgumu wajukuu zake kutafuta busara kutoka kwake. Ni moja ya wazee ambao nchi hii imepata hasara.

Busara na hekima ilitakiwa kumsukuma mzee wetu aone kwamba hatupo katika vita na mtu mmoja ila vita yetu kuu ni kwa maadui watatu ujinga, umasikini na maradhi
 
Amshawishi mara ngapi?!!
 
Siyo raia
 
Jenerali anaposema Magufuli hakujali katiba mbona anatofautiana na chadema wanaosema katiba hii iliyopo mbovu ndio ilimpa Magu madaraka makubwa.?

..hapana.

..Jenerali anamaanisha Magufuli alizidisha unovu wa katiba yetu.

.Matendo ya Magufuli yalikuwa ya kidikteta na kikatili kuzidi katiba ilivyomruhusu.
 
..Hsmad Rashid hasemi ukweli.

..vyama mbalimbali vinashirikiana.

..kwa mfano, 2015 kulikuwa na ukawa.

..2020 Cdm na Act walikuwa na mashirikiano.

..kuhusu kufungwa sio Hamad Rashid peke yake aliyefungwa.
 
Natamani kuona mjadala huru wenye kuchambua mada kwa upana wake kwa maslahi ya nchi sio misingi au itikadi za mtu au kikundi cha watu.
 
Jenerali ulimwengu na Magufuli 🤔 aisee,Huyu Mzee kuna kitu Magufuli alimfanyia
Kumbuka ile fungiafungia magazeti ilimkumba huyo mzee. Aidha, ni mkosoaji wa siku n
Kongamano la kujadili Mafanikio na Changamoto za Kidemokrasia, Utawala wa Sheria na Ushiriki wa Umma, Dar es Salaam.

GEOPHREY PINDA (NAIBU WAZIRI KATIBA NA SHERIA): Tanzania hakuna Sheria mbovu, bali tuna Sheria zilizopitwa na wakati, zinazohitaji kufanyiwa marekebisho ili kuendana na wakati tuliopo

KAIZA BUBERWA: Miaka ya zamani Vyama vya siasa vilipoteza dira baada ya kuweka nguvu nyingi kwenye kutaka kuiondoa CCM madarakani. Wakati huo huo wanufaika wa CCM wakizuia kwa nguvu kutoondolewa Madarakani

JENERALI ULIMWENGU: Miaka mitano ya Magufuli ilijaa ukandamizaji uliopitiliza. Tulishuhudia utawala wa mtu mmoja ukibadili sheria na katiba. Hakujali Katiba ilisema nini. Uzuri alikua mkweli, alisema waziwazi hataki vyama vingi

Magufuli aliamua Wabunge watakao ingia Bungeni yeye mwenyewe, Takwimu zilikuwa ni haramu kama hazikutolewa na Serikali, Azaki zilishindwa kufanya kazi, katika awamu yake wajinga waliibuka kwa wingi na kujiona bora

Lazima tukubali kuwa bado tupo pabaya na tunahitaji kujitafakari tumefikaje hapa, tuangalie kama kuna mtu tuliyemuumiza katika kupotea kwetu. Tujue namna gani ya kuponya mioyo iliyoumia la si hivyo maridhiano hayatakuwa na tija

Rais Samia ameonyesha nia ya kuleta maridhiano. Nasi tuunge Mkono juhudi hizo lakini tunapaswa kufanya hivyo kwa umakinifu ili tusirudi tulipotoka

HAMAD RASHID MOHAMED (ADC): Wanasiasa wa Upinzani kukosa ushirikiano wenyewe kwa wenyewe ni chanzo kikuu cha kukosekana kwa Upinzani imara nchini

Udhaifu wetu mkubwa ni kukosa umoja

JOHN MNYIKA (CHADEMA): Kuingia kwenye mfumo wa Vyama vingi kulipaswa kutanguliwa na mfumo unaoruhusu uwepo wa vyama vingi.

Sasa ni miaka 30 ya Vyama vingi lakini bado hakuna katiba inayoruhusu mfumo wa vyama vingi nchini

Ukosefu wa Katiba Mpya ni Mzizi wa Matatizo. Vyama vya Siasa havina ruhusa ya kufanya mikutano ya Hadhara pamoja na kuwa na Sheria zinaruhusu hili. Pamoja na mabadiliko ya kiutawala bado katazo hili linaendelea

HAMAD RASHID MOHAMED (ADC): Katiba sio mwarobaini bali utashi ndio unatakiwa, nilimwambia Mnyika 'hamuwezi kuandamana kama tulivyokuwa tunafanya sisi'

Nilikuwa tayari kukaa ndani kutetea wenzangu, lakini wao wakisikia kuna kukamatwa watakimbia watajificha uvunguni

FATMA KARUME: Uchaguzi wa 2020 ulikuwa wa hovyo kuliko chaguzi zote zilizopita. Hakujawahi kutokea chaguzi yoyote tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe kusiwe na kesi Mahakamani isipokua wa 2020, na hii ni kwa sababu watu hawana imani na Mahakama

Tumetengeneza Mhimili wa Mahakama usioweza kufanya kazi yake, Rais kuwa na Uwezo wa Kumteua na Kumuondoa Jaji Mkuu kunaondoa Uhuru wa Mahakama

Pia Mahakama kutegemea bajeti ya Serikali kufanya shughuli zake hudunisha uhuru wa Mahakama

JAJI MSTAAFU ROBERT MAKARAMBA: Wale ambao hawapaswi kutunga Sheria ndio wanatunga Sheria, ambao hawapaswi kutafsiri ndio wanatafsiri Sheria

Ndio maana mnasikia mtu anasema ‘Nitakuweka ndani’, yaani anakuwa Sheria, Mahakama na Polisi kitu ambacho tulipiga marufuku

Lazima kuwe na usawa, mfano neno gender lilikuwemo kwenye Katiba yetu likaondoshwa, Wanasiasa wanashindwa kutofautisha kati ya sex na gender

Sex ni biological, gender ni social concern, sasa hivi limebaki neno sex peke yake

Kudhibiti matumizi mabaya ya madaraka, hii inaanzia ngazi ya familia, kinachotoka kwenye familia ndicho kinachoakisi jamii yetu

Mfano Mkuu wa Wilaya au Mkoa anamuweka mtu ndani akiwa hajui umefanya kosa gani

Uvunjani na ukiukwaji wa Haki za Binadamu ngazi ya binafsi ndani ya jamii zetu ni mkubwa sana, hilo tuliangalie

Umoja wa Mataifa umeshaandaa Kanuni za kuongoza biashara katika kuheshimu Haki za Binadamu

ADO SHAIBU (ACT WAZALENDO): Vyama vya Siasa viwajibike kutengeneza mazingira bora ya Ushiriki wa Wanawake

Demokrasia isipoimairishwa, Siasa zikiendelea kuwa za piga ua, za baruti, za mabomu za kukimbizana itawafanya Wanawake washindwe kushiriki Kisiasa

Watu mnajua kugeuzageuza maneno. Sasa hapo si mbovu tu,ndiyo umekanusha nini.

Labda tufasili upya neno ubovu.
 
Bora mnyika na huyo jaji wameongea point, ila huyo ulimwengu ye vita yake na Magufuli hawezi kushinda maana mshindani hayupo!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom