Miaka 30 kwa kusalitiwa na msicha walio kubaliana kufanya mapenzi!! Tuendelee kuwaamini wasichana? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 30 kwa kusalitiwa na msicha walio kubaliana kufanya mapenzi!! Tuendelee kuwaamini wasichana?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Alagwa, Jul 12, 2012.

 1. Alagwa

  Alagwa Member

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  “Huyu mimi sikumbaka bali tulikubaliana nae kufanya mapenzi na ndio maana nakiri mbele ya mahakama hii kuwa nilifanya nae mapenzi.” Alisema mshitakiwa.
  Lakini mahakama hai kusikiliza hilo na kuamua kumuhukumu kijana huyu miaka 3o jela . Je hii ni haki kweli ?

  Kijana kasema wazi kuwa walikubaliana na msicha huyo kufanya mapenzi lakini sasa anashangaa kwa kauli ya binti huyo kuwa alimbaka.

  Wakati umefika kwa wanaume nao kupana nafasi katika kutendewa haki maana wameanza kuwanyanyasa kwa kigezo cha KIPAOMBELE KWA WANAWAKE
   
 2. Zanta

  Zanta JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 2,017
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  In court of law "its not what you know" but "its what you can prove". Kwa hiyo kama kijana kashindwa ku-prove kua hajambaka then ishakula kwake.
  Wangapi wamesingiziwa kubaka na wakaachiwa huru
   
 3. Alagwa

  Alagwa Member

  #3
  Jul 12, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Jamaa amekiri kufanya nae mapenzi ila sio kumbaka kwani wamakaa nae room kwake kwa muda wa siku 4 lakini baada ya hapo msichana alipo rudi kwao ndo wakaibuka ma kesi hiyo. Kweli mtu anaweza kubakwa kwa siku nne mfululizo tena kwenye nyumba ya kupanga bila hata ya majirani kusika? Na kama ni kubakwa ange piga hata kelele jamani watu wamsaidie au sio?
   
 4. Buntungwa

  Buntungwa JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 343
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  siku nne chumba kimoja walielewana hao kijana awe huru
   
 5. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Binti ana umri gani? Kama ni chini ya miaka 18, hapo hana ujanja. Ila kama ni juu ya miaka 18, inawezekana walitegemea kulipwa fedha kama watasema hivyo... wachunguze pia uchumi wa binti nyumbani kwake, na kama binti huyo amekuwa akitumiwa na familia kama chanzo cha mapato
   
 6. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ..hata mimi hii hukumu imenisumbua sana. Pamoja na binti kudaiwa kuwa na miaka 16 nadhani ndugu wa kijana wanapaswa kudhibitisha hili ili kijana wao atendewe haki. Taarifa zinasema kuwa binti anamsaidia mama yake ambaye ni mama lishe na alimtuma binti yake chumbani kwa kijana ili kuchukua hela ya makande aliyokuwa akimdai. Hili tu linaanza kunitia waiwasi. Utamtumaje binti yako kwenye kinywa cha Simba? Haya, inadaiwa kuwa baada ya kuingia kwenye chumba cha kijana kwenye nyumba aliyokuwa anapanga kijana alimfungia na kumbaka kwa siku NNE mfululizo, ndipo binti akapata upenyo na kutoroka na kurudi kunyumbani na kuwajulisha yaliyomsibu ambapo familia iliamua kulipeleka suala hilo Polisi na siku tatu baadae Kijana akakamatwa na siku hiyo hiyo kufikishwa Mahakamani na kupewa kichapo cha miaka 30 Jela kwa kosa la Kubaka! Hivi Kesi zote TZ zingekuwa zinaendeshwa haraka hivi si Magereza yetu yangepungua wafungwa wanaosubiri upelelezi kukamilika??
   
Loading...