Miaka 30 ijayo kabila la kichaga kutoweka kabisa Kilimanjaro

Ishara zote zinaonyesho miaka 30 ijayo kabila maarufu la kichaga litafutika kabisa mkoani Kilimanjaro.

Sababu kuu ni kama zifuatazo:
  • Wachaga wengi wanaoa na kuolewa na makabila tofauti,wengi walio oa kabila tofauti wakifa wake zao ambao ni kabila tofauti wanarithi Mali za mume zao pamoja na shamba LA urithi alilopewa Mme wake.
  • Watoto wengi Wachaga miaka ya sasa hivi wanazaliwa mijini na mikoani na wanakua na tatizo la kutokujua mila na desturi za kichaga sababu hiyo inafanya wawe waswahili.
  • Wanawake wana olewa uchagani wanaleta ndugu zao pindi wenye mji wanapokufa kama kawaida mnajua wanaume wanatangulia kufa. Mfano mzuri ni Jirani yetu mwanamke wa kipare aliolewa kwenye ukoo wetu wa Lema baada ya mume wake kufa na wakwe zake alileta ndugu zake wengine wakaoa na kuolewa huku machame.
  • Wachaga halisi waliorithi Mali na mashamba kutoka kwa wazee wetu hawakuthubutu kuuza ile ardhi kutokana na historian jinsi wazee wetu walivyoteseka kupata ardhi miaka ya 1700 mpaka 1900 mwanzoni.
  • Wanaozaliwa nje ya Kilimanjaro na kurudi uchagani bila kujua historian na wale wanawake wanaoolewa uchagani wanauza na watauza ardhi kwani historian inafutika Wachaga wanajenga mbali na Kilimanjaro na wengine wanafia huko na kuzikwa huko.
  • Ukiwa uchagani sasa hivi kila ukikutana na watu kumi basi watano ni wageni
Ama kweli kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho. Binafsi nasikia uchungu sana nikitafakari mambo haya,hakuna jinsi dunia inabadilika na hakuna wa kuzuia.

Wito kwa wachaga acheni Mara moja kuwadharau wazaramo kwa kuuza mashamba na kuikimbia Dar yaleyale yanakuja kwenu na nashauri mvumilie hakuna jinsi tena ndugu zangu.
Basi ata wachina watatoweka china maana wamesambaa duniani kote...

My take..rudi kalale uote tena hyo ndoto yako then uje na uzi unaosema
WACHAGGA TUNAKARIBIA KUITAWALA DUNIA.
 
Ishara zote zinaonyesho miaka 30 ijayo kabila maarufu la kichaga litafutika kabisa mkoani Kilimanjaro.

Sababu kuu ni kama zifuatazo:
  • Wachaga wengi wanaoa na kuolewa na makabila tofauti,wengi walio oa kabila tofauti wakifa wake zao ambao ni kabila tofauti wanarithi Mali za mume zao pamoja na shamba LA urithi alilopewa Mme wake.
  • Watoto wengi Wachaga miaka ya sasa hivi wanazaliwa mijini na mikoani na wanakua na tatizo la kutokujua mila na desturi za kichaga sababu hiyo inafanya wawe waswahili.
  • Wanawake wana olewa uchagani wanaleta ndugu zao pindi wenye mji wanapokufa kama kawaida mnajua wanaume wanatangulia kufa. Mfano mzuri ni Jirani yetu mwanamke wa kipare aliolewa kwenye ukoo wetu wa Lema baada ya mume wake kufa na wakwe zake alileta ndugu zake wengine wakaoa na kuolewa huku machame.
  • Wachaga halisi waliorithi Mali na mashamba kutoka kwa wazee wetu hawakuthubutu kuuza ile ardhi kutokana na historian jinsi wazee wetu walivyoteseka kupata ardhi miaka ya 1700 mpaka 1900 mwanzoni.
  • Wanaozaliwa nje ya Kilimanjaro na kurudi uchagani bila kujua historian na wale wanawake wanaoolewa uchagani wanauza na watauza ardhi kwani historian inafutika Wachaga wanajenga mbali na Kilimanjaro na wengine wanafia huko na kuzikwa huko.
  • Ukiwa uchagani sasa hivi kila ukikutana na watu kumi basi watano ni wageni
Ama kweli kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho. Binafsi nasikia uchungu sana nikitafakari mambo haya,hakuna jinsi dunia inabadilika na hakuna wa kuzuia.

Wito kwa wachaga acheni Mara moja kuwadharau wazaramo kwa kuuza mashamba na kuikimbia Dar yaleyale yanakuja kwenu na nashauri mvumilie hakuna jinsi tena ndugu zangu.
Wote ni watanzania, na sio wachaga tu hiyo hali inawakumba makabila yote leo hii mmasai anasuka wanawake nywele salooni huko mjini.
 
Kweli uchagani kumezidi sehemu kama rombo wamejaa wasambaa na wanuaturu wanalisha mifugo na wanaoa ukouko na kuzaliana tofauti na mikoa mingne ni nadra sana kukuta makabila tofauti na wazawa vijijini
 
mbona hata ulaya wageni watakua wengi kuliko wenyeji wa asili yaani wazungu. hilo tatizo mbona si kwa wachaga tu ila ni kwa kabila zote au watu wote. inaelekea mtoa mada ana mind sana ukabila. angeangalia tu angeona tatizo hilo liko kwa watani zake wapare na jirani zao wamasai ambao wao tayari wamehama kwao na kusambaa nchi nzima. ni maendeleo huwezi kuzuia kwa mkono. hivi sasa juhudi zianzishwe kuhifadhi lugha za kienyeji. mijini watu waanzishe madarasa kuwafunza watoto lugha za kabila zao kwa vile asilimia kidogo sana ndio wanajua.
Fact.
 
Inauma sana
mwenyewe natafakari nabaki naumia mno
Iruwa mndumi lukabannye mbe lulasasange fo mbe maana
nyindo da baba kwifo namna fo
 
Dunia ya utandawazi hii,lengo la watandawazi ni kuvunja ukabila,udini,ukanda,na rangi ili kufanya watu wote kuwa na mira inayofanana.wachaga watahama na wageni watahamia,mbona wachaga wamejaa huku mlimba kwani huku ni marangu??
 
Ni kweli kuna mabadiliko makubwa ktk jamii ya wachaga licha sikubaliani na hoja na maono ya mleta mada.

Kwanza kila desturi na tamaduni za jamii yoyote huwa zinabadilika, wapende au wasipende.
Ni jukumu la watu wa jamii yao kuhakikisha mabadiliko yanaleta matokeo chanya na siyo hasi.

Pia tamaduni na desturi tulizozikuta ktk jamii zetu ni namna wazee waliotangulia walivyoamua ku define maisha yao au walivyokubali mazingira yatengeneze desturi na tamaduni zao.

Ni jukumu letu kama kizazi kipya kutengeneza tamaduni na desturi zetu badala ya kukumbatia desturi za wazee wetu.
Swala la culture ni pana, tusichukue situations za wazee wetu na kuita culture yetu, hapana ni culture ya wazee wetu. Watu wengine wanaokota mabakuli ya mbao ya wazee wetu na kuita culture yetu, hapana ni culture ya wazee wao, tuna jukumu la ku create yakwetu.

Ktk kipindi hiki cha mageuzi makubwa duniani, jamii ya wachaga ina jukumu la kujipanga na kutafakari weakness yao na strength yao na kutumia strength yao kufunika weakness yao
 
Suala la mtu back kupewa ardhi ya urithi uchagani sijawai ona labda huko kwenu.
 
Ni wachaga tu wanaotoka nje ya mkoa wao? hayo mambo yapo kwa makabila karibu yote, hata wamasai sasahivi wameacha kuchunga wamekuwa walinzi na wauza dawa za kienyeji mijini
Sisi tunasifika kwa hilo tu mkuu?LOOH!
 
Hakuna na hakujawahi kuwa na kitu kama ,,Kabila la Wachaga" Dunia hii bali kilichopo ni makundi mbali mbali ya watu yaliounganishwa na Mzungu na kubatizwa jina Wachaga lkn kabla ya Mzungu kuja hao unaowaita Wachaga hawakujiita hivyo!
Ila walijiita nani? Unajua asili ya wachaga na wametokea wapi?
 
Hii ishu inaathiri makabila yote.. lakin kabila la wachaga ni kubwa.. kuna wamarangu.. machame ..kibosho.. huru, oldmoshi..

Hiyo dhana kuwa kabila la wachaga litapotea.. ni ndoto nyevu...
Haitokaa itokee ng'o.

Long live chagga.... long live kilimanjaro..
 
Back
Top Bottom