Miaka 20 tangu Ubalozi wa Marekani ushambuliwe Tanzania, ipi kumbukumbu yako?

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
5,450
2,000
Wakuu heshima mbele,

Tarehe 7/8/1998 balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya zilishambuliwa kwa wakati mmoja/wakati uliokaribiana na kwa ukanda huu huo ulikuwa ni kama utambulishi wa Al Qaeda katika EA.

Kwa Tanzania nadhani hilo lilikuwa tukio kubwa la ugaidi katika ardhi yetu huku wenzetu Kenya wao walipitia misukosuko kadhaa.

Binafsi sina kumbukumbu yoyote ya tukio hilo wakati linatokea lakini nilibahatika kusoma kitabu kinachoelezea vizuri Al Qaeda tokea kuanza kwake mpaka 2001 na matukio waliowahi kuyafanya kinaitwa "The Looming Tower,Al Qaeda and the road to 9/11".

Pia niliwahi kusoma uzi mmoja mujarabu sana unaitwa https://www.jamiiforums.com/threads...resheni-ya-kukamatwa-osama-bin-laden.1115962/ author alikuwa ni habibu BAnga ambao basically unaonesha nini kilitokea 2001, intelligence na mpaka kuuawa Osama bin Laden.

Mambo ni mengi sana na kwa kuwa JF ipo kila mahala tungependa angalau kujua mbili tatu za tukio lenyewe maana kuna watu walishudia huku tukiendea kuwaombea waliotangulia na faraja kwa majeruhi.

Nawasilisha
 

DrLove69

JF-Expert Member
Jan 20, 2018
3,117
2,000
Naikumbuka siku ya leo miaka 20 iliyopita. Nilikuwa nimerudi likizo nyumbani Tanzania. Nikiwa nimebakiza siku chache kuondoka zangu. Ilikuwa siku ya Ijumaa mida ya saa Nne asubuhi na nilikuwa maeneo ya Oysterbay Hotel (wa zamani mmenielewa). Nilitoka hapo Ubalozini jana yake kwa shughuli za kuweka mambo yangu sawa ya kurudi zangu nilikotoka...kwa sababu Ubalozi wa Marekani walikuwa hawafanyi kazi siku ya Ijumaa. Yaani huduma zilikuwa kuanzia Jumatatu mpaka Alhamisi. Siwezi kuisahau hii siku kwa sababu kama wale magaidi wangeichagua siku ya Alhamisi kufanya mashambulizi yale, kwa hakika ningekuwa mmoja wa wahanga au leo hii nisingekuwepo hapa. Namshukuru sana Mungu kwa yote...maana tarehe 6 August 1998 saa nne asubuhi nilikuwa Ubalozini.
Hii ni kumbukumbu yangu ya siku ile BLACK FRIDAY.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom