Miaka 20 kumbukumbu ya kifo cha Mzee Moses Nnauye na kilio cha kupewa mtaa

Miguna Chiwenga

New Member
Jan 4, 2022
1
0
MIAKA 20 KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MZEE MOSES NNAUYE NA KILIO CHA KUPEWA MTAA

Tumeshuhudia mambo mengi sana katika Mwaka uliomalizika wa 2021 yapo mambo mengi lakini yaliyotikisa ni mambo ya Kisiasa, Tulishuhudia katika Tasnia ya siasa za (Chama Tawala, chama cha Mapinduzi) na za baadhi ya viongozi wake wa zamani wa chama na serikarili ambapo tuliweza kuona Kumbukumbu ya miaka 20 ya Kifo kwa Mtumishi mstaafu wa ngazi ya juu wa Jeshi letu la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mzee Moses Nnauye. Sio utamaduni au utaratibu wa kawaida kwa chama cha Mapinduzi kuwaenzi makada na viongozi wastaafu wa chama cha mapinduzi waliochangia chama kwa hali na mali na ambao wametangulia mbele za haki; pengine aliye pekee katika hili ni Hayati Baba wa Taifa ambae kifo chake uadhimishwa tarehe 14 October ya kila Mwaka, lakini pamoja na hayo kama ni utaratibu rasmi na utaendelea kwa wengine, ni jambo jema hasa kwa vile inatoa fursa kwa vijana au kizazi cha sasa kujifunza juu ya historia ya chama cha mapinduzi pamoja na waasisi waliojitolea kukijenga na kukiimarisha kwa hali na mali. Ni ukweli kwamba Historia ya chama haikuanza na vita vya Kagera na badae urafiki singidani.

Katika maadhimisho hayo ya kumbukumbu ya Kifo cha Mzee Nnauye Mwamba wa siasa za ccm akiwa mwanzilishi wa Chipukizi, greengurds na mengine makubwa, Tumesikia historia yake japo kwa uchache jinsi alivyoweza kushiriki katika kukijenga chama na kukitumikia kwa nafasi mbalimbali na hasa pale alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida aliweza kusaidia makada wenzake akiwemo Mzee Yusuf Makamba ambae alikuwa Katibu Tarafa katika moja ya Wilaya mkoani humo, Mzee Makamba alieleza jinsi Mzee Nnauye alivyokuwa mtu wa kujitoa na kusaidia wenzake kwa kuweza kuwasemea maeneo mbalimbali pale anapopata nafasi hiyo, na kupitia yeye watu wengi waliweza kupanda kwa kupata nafasi kubwa za uteuzi kupitia Mgongo wa Mzee Nnauye.

Haya yote tumeyasikia kutoka kwa Mzee Makamba alipokuwa akielezea historia hiyo, lakini pamoja na yote hayo Mzee Nnauye kwa mujibu wa mzee Makamba analalamika anaona kutoheshimiwa tangu alipofariki, kwamba viongozi wanaonekana kushindwa kumuenzi katika namna ya kupewa hata Mtaa ili kumuenzi. Sasa mm najiuliza kama kweli mzee Makamba siyo mnafiki, tunaomba atuambie yafuatayo, Kwamba amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa mkoa katika Maeneo mengi na badae DSM na Katibu mkuu wa ccm tena vyeo vingine vikiambatana kwa pamoja, nafasi hizi tunaamini ni kubwa sana hazishindwi kumfanya Makamba kufanya maamuzi au kupendekeza kama kweli angetaka kumjengea heshima mzee Nnauye asingeshindwa kumpa moja kati ya Mtaaa, Soko, Uwanja, Madaraja. Anafanya yote haya ni mwendelezo wa unafiki wake na kutaka kujionyesha mwema kwa Watoto wa Mzee Nnauye, Najua kuna kitu wanakitaka ntakisema badae. Bado haitoshi Rais wa Awamu ya Nne nae alikuwepo kwenye maadhimisho hayo na ni sehemu ya rafiki mkubwa wa Mzee Nnauye nae bado alishindwa kuona umuhimu wa kumpa mzee Nnauye hata Mtaa mpaka katoka Madarakani baada ya kukaa miaka 10, hakuona umuhimu wa mzee Nnauye lakini wote walijumuika pale kulilia Mzee Nnauye amepuuzwa, haheshimiki kiasi cha kushindwa kupewa hata Mtaa, huu ni Unafiki, kama kweli nyie mlimpenda kwa Dhati msingeshindwa kumpa mtaa mnaoulilia hadharani tena kwnye camera bila aibu, mnaonyesha ni kiasi gani mmemtumia Mzee wa watu Marehemu Mzee Moses Nnauye kwa maslahi yenu, mlimtumia kupanda mabega yake kujinufaisha wenyewe na familia zenu na matokeo yake mzee huyo kafa masikini na bado mkamsema kwamba alishindwa kuandaa maisha yake kwa sababu ya Ulevi huku nyinyi aliowasaidia mkishindwa kutambua umuhimu na mchango wake.

Familia ya Mzee Makamba bado inaendeleza staili ile ile iliyotumia kumtumia Mzee Moses Nnauye kujinufaisha yenyewe, tunashuhudia Mwanae Nape Moses Nnauye akiendelea kutumika kisaisa katika familia ya mzee Makamba, Wanajua ushawshi wa Nape aliowahi kuupata huko nyuma ndio wanaulekeza kuutumia huo huo kumbeba January Makamba, sasa hivi Nape kajikabidhi kama ndio kiranja mkuu wa mbio za urais za Januray, wanamtumia kwa staili ile ile waliyomtumia babake Mzee Moses, Nape ndio anatumika kushawishi Makada na watu mashuhuri wamuunge mkono January kwny mbio za Urais, Nape amewekwa kama Punching bag ndie anaenunua ugomvi wowote unaohusu siasa za January kuelekea 2025.

Mimi napenda nitumie nafasi hii kumuonya, kumshauri na kumsaidia Nape kwamba ifike mahala Nape usiwe Punda, usiwe mpumbavu wa kiasi hicho cha kutumiwa na hiyo familia kama vile umekatwa kichwa, Ni familia hiyo hiyo ndio iliyosimamia wewe ufukuzwe ccm chini ya Makamba akiwa Katibu Mkuu wa CCM alikufukuza ccm na akasema umefungiwa Duniani na Mbinguni, Ni familia hii hii ndio iliyosimamia matangazo ya ndg zako kwa kutambulisha watoto wa mzee Nanauye kwenye gazeti na kuhakikisha jina lako wewe halitambuliki na haliwi sehemu ya familia ya mzee Nnauye, haya yote walikufanyia wewe bila huruma na kulenga kukudhalilisha, baada ya kujeruhiwa hivyo kisiasa ulienda mbali zaidi kwakutafuta mbadala mpaka kufikia kiasi cha kujichafulia Historia yako kwa kuwa mmoja wa Waanzilishi wa chama cha CCJ hiyo ni baada ya kujiridhisha kwamba Makamba na wenzake walishaamua kwamba hauhitajiki CCM unapokonywa Kadi. Bila ya huruma ya Rais Kikwete mpaka leo usingekuwa Mwana ccm. Na kumbuka wakati ccm inahakiki mali za chama, gari lako lilifatwa kijijini na likarudishwa kama sehemu ya mali za chama zilizoibiwa, wala January hakuwahi kurudisha gari hilo mpaka leo na bado hujiulizi kwanini?.

Ushauri wangu acha kutumika na hiyo familia, Usidhani kama wanakupenda, wala Wanampenda Marehemu Babako , hawakupendi ww wala Babako… , wangekuwa Wanampenda huo Mtaaa wanaoupigania leo wangeshampa tena zaidi ya Mtaa, Wanakukumbatia wakijua ww unahimili matusi na mikiki kwajili ya kumlinda Mtoto wao Mpendwa katika safari ya Urais jambo ambalo nauhakika huo urais hata kaa aupateee, Kwa yeyote mwenye uelewa wa Siasa za CCM hasa 2015 na kuendelea, January kuwa Rais ni Ndoto…haiwezekani; ni haki yake kikatiba lakini ni juhudi ambazo mazingira hayatampa nafasi. zinduka acha upumbavu wa kuendelea kutumika jifunze kupitia marehemu babako alivyotumika na hao hao ambao leo ni wastaafu na wanapata kila kitu hawana Deni na mtu, Ww bado ni kijana tafuta maisha yako ya kisiasa mwenyewe, tafuta pesa urudishe heshima ya familia ya mzee Nnauye achana na ujinga wa kuililia Mtaa.
 

Attachments

  • Mtaa.docx
    18.3 KB · Views: 20
Back
Top Bottom