JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,106
- 3,523
Habari wanajamvi!
Mimi ni mtumishi wa umma, huu ni mwaka wangu wa 27 kazini.Katika kipindi chote hicho nimekuwa nikifanya kazi kwa bidii na maarifa bila kujali mwajiri wangu hatimizi majukumu yake ipasavyo.
Miaka 10 ya mwanzo nilifanya kazi bila kupanda daraja,mpaka ikafikia muda watu walio ajiriwa nyuma yangu wakawa na mikubwa kuliko mimi.
Mwaka 2001 nikapanda daraja kwa mara ya kwanza. Mwaka 2003 nikapanda tena, na mwaka 2007 nikapanda tena. Baada ya hapo sikupanda daraja mpaka hii leo, yaani miaka 10 mingine bila kupanda daraja.Juzijuzi tulipanda madaraja watumishi wengi na mimi nikiwemo, Lakini tulipata mshahara mpya mwezi mmoja tu Rais akasitisha madaraja kwa kisingizio kuhakiki watumishi wa umma. Mpaka leo hii, miezi 7 baada ya uhakiki kwisha mishahara haijarudishwa.
Nimepanga kustaafu at 55. Nimechoka kutumika kama male sheath! Halafu mtu anaomba tumuombee wakati yeye hatutakii mema. Mungu ambariki aendelee kututawala apendavyo ! iko siku Mungu atatulipa na kutufariji.