Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 1,740
- 4,230
Mwanahabari Jean Bigirimana wa Burundi alipotea tangu Julai 22 mwaka 2016 na hadi leo hajapatikana wala habari kuhusu yeye kusikika popote.
Bigirimana alikuwa mwandishi wa gazeti la kila wiki la Iwacu na alipotea mchana wa Julai 22, 2016 baada ya kupokea simu kutoka kwa kinachodaiwa kuwa chanzo chake katika Usalama wa Taifa wa nchi hiyo.
Mke wa Bigirimana, Bi. Godeberthe Hakizimana aliiambia Associated Press kuwa mumewe alienda Bugaramana, Muramvya lakini hakurudi licha ya kuahidi kurudi kwa ajili ya chakula cha usiku.
Bigirimana alipotea ikiwa ni wiki chache tu tangu atoke kwenye mafunzo ya uandishi nchini Rwanda na gazeti la Iwacu linaamini amechukuliwa na Usalama wa Taifa kwa sababu aliandika makala akiwa Rwanda kuhusu maisha ya mwandishi aliye uhamishoni.
Haijawahi kuthibitishwa kama alikamatwa au amefariki lakini Taasisi ya uangalizi wa Haki za Binadamu umeona matukio ya utekaji, ukamataji, utesaji na mauaji ya wanaharakati wa kijamii, wanahabari na wengine kutoka kwa Serikali, waasi wenye silaha na watu wasiojulikana tangu Aprili 2015 maandamano yalipoanza kufuatia uamuzi wa Nkurunziza wa kugombea kwa kipindi cha 3.
Hii habari inaendana sana na ya Mwandishi wa Mwananchi, Azory Gwanda aliyepotea tangu Desemba 2017.
Je, tuache kumlilia na kusubiri maana hatarudi tena?
Je, Gwanda aliandika makala yeyote 'hatarishi'?
Wizara imejitoa katika hili na tumekatazwa kuihusisha. Tukaombe msaada nje ya nchi kwa jambo lililo ndani ya uwezo wa vyombo vyetu vya dola?