Miaka 179 Baadaye Siku Kama ya Leo: Fikra Zake Zinaishi

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,742
40,873
160377-004-ECB7BCBD.jpg

Na. M. M. Mwanakijiji

Mwaka 1743 Siku ya Jumatano tarehe 13 Aprili alizaliwa Thomas Jefferson. Alizaliwa wakati Marekani ikiwa ni koloni la Waingereza. Thomas Jefferson alikuwa ni Rais wa tatu wa Marekani baada ya George Washington na John Adams. Alikuwa pia ndiye Waziri wa kwanza wa Mambo ya Nje wa Marekani (Secretary of State) chini ya Rais George Washington. Historia inamtambua kama mtunzi mkuu wa Azimio la Uhuru (Declaration of Independence) ambamo ndani yake maneno yale maarufu ya kuwa “Binadamu wote wameumbwa sawa, na wote wamejaliwa na Muumba wao haki kabisa zisizoondosheka ambapo miongoni mwao ni haki ya uhai, uhuru na kutafuta furaha”.

Jefferson alikuwa ni mwanafalsafa, mwanasayansi na mwananadharia za kisiasa ambaye msimamo wake umeacha msingi mkubwa wa maisha ya kisiasa katika Marekani. Yeye pamoja na kina Washington na wenzake wanatambulika kama “Mababa Waasisi” (Founding Fathers) wa Marekani. Pamoja na utunzi wake wa Azimio la Uhuru ambalo lilianisha sababu ya Wamarekani kukataa kuwa chini ya himaya ya Waingereza Thomas Jefferson aliandika maandishi mengine mengi na wakati mwingine alipingana hata na waasisi wenzie. Mchango wake katika fikra na maisha ya Wamarekani ni mkubwa sana.

Pamoja na hayo yote Jefferson alikuwa binadamu. Alikuwa na matatizo yake na mapungufu ambayo historia inayatambua; licha ya kwamba alitunga yale maneno kuwa “binadamu wote wameumbwa sawa” yeye mwenyewe alikuwa na watumwa takriban 150; usawa wao ulikuwa wapi? Alikuwa hapendi mahusiano ya mapenzi ya watu wa rangi tofauti (interracial relationships) lakini yeye mwenyewe inaamini kuwa alikuwa na mpenzi hadi kuzaa naye mtumwa wake mmoja mweusi – Sally Hemingway.

Ukweli huo wote na mapungufu yake yote hayaondoi ukweli wa mchango wake kwa taifa lake na kwa Jimbo lake la Virgnia ambako alionesha jinsi alivyothamini elimu kwa kuanzisha Chuo Kikuu cha Virginia na maktaba na vitu vingine vingi – ikiwemo mfumo wa elimu wa utatu (tertiary education system). Jefferson hakumaliza yote yaliyoikabili nchi yake, miaka hamsini tangu kuandikwa kwa maneno yale ya Azimio Jefferson alifariki akiwa na miaka 83 – siku hiyo hiyo Rais aliyemtantulia John Adams naye alifariki huko Boston (siku ya Julai 4, 1826). Ilikuwa ni Sikukuu ya Uhuru wa Marekani.

Miaka 179 baadaye, mbali kabisa kutoka Marekani katika iliyokuwa koloni la uangalizi la Waingereza la Tanganyika. Siku ya Alhamisi tarehe 13 Aprili, 1922 alizaliwa Julius Kambarage Nyerere. Alizaliwa chini ya utawala wa Waingereza. Julius Nyerere naye alipoingia kwenye siasa alijikuta anatambua jambo ambalo Jefferson naye alishalitambua; Nyerere aliweka mawazo yake katika Azimio la Arusha ambalo mtunzi wake mkubwa alikuwa yeye mwenyewe na sehemu yake ya kwanza inatangaza kuwa “binadamu wote ni sawa”.

Tofauti na Jefferson, Nyerere aliona usawa huu siyo suala la kuumbwa tu ni usawa unaotokana na utu wao. Kwamba, bila kujali rangi, kabila, dini n.k binadamu wote wana utu sawa. Nyerere yeye alienda mbali zaidi na kuhakikisha kuwa – tena kama kanuni – kwamba “kila mtu anastahili heshima”. Wakati Jefferson alifungwa na mazingira ya wakati wake ambapo utumwa ulikuwa unakubalika nay eye mwenyewe akiwa na watumwa Nyerere alikataa mapema kabisa ubaguzi wa rangi kwani unapingana na msingi huo wa kwanza kuwa binadamu wote ni sawa. Ni kwa sababu hiyo aliweka kama madhumuni ya TANU ya wakati ule kuwa mojawapo ya malengo ya TANU kama chama cha kupigani Uhuru ilikuwa ni “Kuona kwamba Serikali inatoa nafasi zilizo sawa kwa wote, wake kwa waume, bila kujali rangi, kabila, dini au hali;” na “Kuona kwamba Serikali inaondoa kila namna ya dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa na upotofu” (Neno “upotofu” lilivyotumika hapa wakati huo ndivyo tunavyomaanisha leo tunaposema “ufisadi”).

Viongozi hawa wawili wote wanapaswa kuangaliwa kwa zama zao. Wakati mwingine unaweza kukuta unahukumu vikali bila kujali maudhui ya kihistoria (historical context) ya viongozi hawa. Mojawapo ya mambo ambayo nimekuwa nikiyaangalia sana ni jinsi gani vijana au hata watu ambao hawajachukua muda kusoma na kumwelewa Nyerere wanakuwa wepesi sana kuhukumu kwa ukali. Ni sawasawa na mtu kusema kuwa Jefferson alifeli uongozi wake kwa sababu hadi anakufa utumwa ulikuwepo! Au kusema kuwa alifeli kwa sababu hakuweza kuondoa matatizo yote ya Wamarekani; hakuweka misingi yote ya utawala na kuhakikisha viongozi wanaokuja hawafanyi lolote jingine kwani lote lililohitajika kufanywa lilifanywa na Jefferson. Hii siyo haki kwa historian a hata kwa mtu mwenyewe.

Kuna watu ambao wangependa kuwa Nyerere angekuwa amemaliza kutengeneza mifumo yote, kuandaa viongozi wote (kwa miaka mia ijayo) na kutatua matatizo yote ambayo alikutana nayo. Kwamba, kila mtu angekuw ana nyumba nzuri, barabara zingekuwepo, umeme hadi wa kumwaga n.k Kwamba kwa vile alipokufa Tanzania bado ilikuwa ni nchi maskini basi ndugu zetu hawa wanasema tu kuwa “alifeli”.

Leo hii inawezekana anazaliwa Mtanzania mwingine, mtu mwingine ambaye anaweza kuja kutoa mchango mkubwa sana katika maisha ya Taifa letu huko mbeleni. Changamoto ambazo leo zipo zinaweza kumalizwa na sisi; lakini haina maana hakuna changamoto nyingine zinazoweza kuja huko mbeleni. Anayedhani Magufuli – pamoja na jitihada zote anazofanya – atamaliza matatizo yetu yote naye huyo ni muota ndoto. Magufuli atafanya kwa kadiri ya uwezo wake na kwa kadiri ya zamu yake. Na yeye kama ilivyokuwa kwa Jefferson na Nyerere – naye ana mapungufu yake. Mapungufu haya hata hivyo hayamfanyi apoteze mwelekeo au aone hafai kufanya lolote.

Hivyo, kwa sisi mashabiki na wanafunzi wazuri wa Mwalimu leo ni siku ya kutafakari mchango wetu wa kifikra kwa taifa letu. Tunamshukuru Mungu kwa kutupa mtu ambaye ameacha alama ambazo leo zinakumbukwa katika taifa letu.

#TunakukumbukaMwalimu
 
Mwalimu Nyerere alikuwa ni dikteta lakini udikteta wake ulizaa taifa lenye umoja na mshikamano.

Udikteta wa Mwl. Nyerere ndio umefanya Tanzania kuwa ni nchi ambayo MwanaJamiiforums aitwaye Goliath mfalamagoha amesema;

3.Tz ni nchi ambayo haijawahi kupata majanga makubwa kama matetemeko ya ardhi, magonjwa ya mlipuko kama ebola, mafuriko na vimbunga au ukame.

4.Tz ni nchi ambayo imekuwa na kitu ambacho nchi za Afrika zimekikosa. Kitu hicho ni AMANI. Kwa miaka yote 54 ya uhuru haijawahi kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe.

5.Tz ina ukubwa wa 945,000 km za mraba yani sawa na uchukuwe Denmark, France, United Kingdom, Netherland, Ireland ujumlishe zote kwa pamoja.

6.Tz ina eneo la bahari lenye ukubwa wa 1,424 km. Bahari inaleta fursa za usafirishaji, uvuvi, utalii na nyinginezo.

7.Tz ni nchi ambayo imepakana na nchi za (Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi, D. R. Congo) ambazo zinategemea bahari yetu kwa usafirishaji wa mizigo na ni fursa nzuri ya kuzipelekea bidhaa za viwanda vyetu.

8. Tz ina maziwa makubwa manne na mengine madogo mengi.

Maziwa matatu makubwa yako kwenye kumi bora za ukubwa duniani na Maziwa makubwa matatu yote yapo Tanzania. Ziwa Victoria ni la tatu kwa ukubwa duniani (la kwanza Afrika) na ziwa Tanganyika ni la sita kwa ukubwa (la pili Afrika) na la kwanza kwa kuwa na kina kirefu duniani. Ziwa Nyasa ni la tisa kwa ukubwa duniani (ni la tatu Afrika).

9.Tz ina mito mikubwa kumi ambayo ni mto Kagera, mto Ruvuma, mto Rufiji, mto Wami, mto Malagarasi, mto Mara, mto Pangani, mto Ruaha, mto Gombe, mto Mweupe wa Nile na ina mito midogo mengi kama mto Kilombero, mto Mbemkuru n.k

10.Tz ndiyo nchi ya kwanza Afrika kuwa na maji mengi yasio na chumvi yaliyokuwa kwenye uso wa dunia (fresh surface water) kutokana na kuwana mito na maziwa mengi na kupitiwa na bonde la ufa.

11.Tz ni nchi ya nne kwa uzalishaji dhahabu Afrika baada ya Afrika Kusini, Ghana na Mali na ipo TOP 20 duniani. Kuna migodi nane inayochimbwa dhahabu na miwili imefungwa. Migodi inayochimbwa ni Buzwagi gold mine- (Shinyanga), Geita gold mine-(Geita), Golden pride gold mine-Nzega (Tabora), Bulyanhulu gold mine- (Shinyanga). New leuka Gold mine- (Mbeya),

Tulawaka gold mine-(Kagera), North mara gold mine-(Mara). Iliyofungwa ni Korandoto gold mine (Shinyanga), Senkenke gold mine-(Shinyanga???).

12.Tz ina madini ya almasi yanayopatikana Mwadui Shinyanga. Mgodi huo ulianza kuchimbwa tangu mwaku 1940. Mpaka leo bado unachimbwa, unamilikiwa na kampuni ya Waingereza.

13.Tz ni nchi ya kwanza na ni nchi pekee inayozalisha madini ya tanzanite duniani. Mkufu wa kuvaa shingoni unatengenezwa na tanzanite na almasi unauzwa hadi shilingi milioni 25 za Kitanzania.

14.Tz ina madini ya chuma yanayopatikana Mchuchuma, Ludewa- Njombe mgodi unamilikiwa na Wachina. Mgodi huo una hifadhi ya madini ya chuma tani milioni 122 ambayo yanawezwa kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 100.

15.Tz ina madini ya makaa ya mawe (Coal) yanayochimbwa Kiwira Mbeya, Mchuchuma na Liganga Njombe. Unamilikiwa na Wachina. Pia mgodi wa Ngaka kule Mbinga-Ruvuma unamilikiwa na kampuni ya Tancoal ya Australia. Hifadhi ya madini ya makaa ya mawe iliyopo ni tani bilioni 2. Makaa ya mawe ndio chanzo cha pili cha umeme wa bei nafuu duniani baada ya maji.

16.Tz ina hifadhi ya madini ya Uranium kule Dodoma (Bahi) na ni mgodi ambao unamilikiwa na Warusi. Pia madini haya yanapatikana Namtumbo (Mkuju), Galapo, Minjingu, Mbulu, Simanjiro, Lake Natron, Manyoni, Songea, Tunduru, Madaba and Nachingwea.

17.Tz ni moja ya nchi tatu Afrika zikiwemo Zimbabwe na Madagascar kwa kuwa na madini mengi ya graphite. Madini haya yapo Tanga, Mahenge-Morogoro, Mererani- Manyara. Madini ya graphite ndiyo yanayotumika

kutengenezea betri za simu, kwenye injini na brake za magari na kwenye karamu za risasi (pencili).

18.Tz ina madini ya nickel yanayopatikana kule Kabanga Kagera, milima ya Uluguru-Morogoro, North Mara, Ngasoma-Mwanza.

19.Tz ni nchi ya tatu duniani kwa kuwa na hifadhi kubwa ya magadi soda duniani baada ya Marekani na Uturuki. Magadi soda hutumika kutengeneza vioo vya aina zote. Vioo vya nyumbani hadi magari pia kutengeneza sabuni na dawa mbalimbali za usafi.

20.Tz ina hifadhi na mgodi wa madini ya niobium uliopo Panda hill Mbeya ambao ndio utakuwa mgodi mkubwa wa kwanza Afrika na wa nne duniani. Mgodi huu unamilikiwa na kampuni ya Australia. Madini ya niobium ni magumu sana hutumika kutengeneza mabomba pamoja na madini chuma pia hutumika kutengeneza baadhi ya sehemu za injini za ndege na vyombo vinavyoenda nje ya uso wa dunia (mfano Apollo 15 CSM), vioo vya computer na lenzi za camera.

21.Tz ni nchi ya kwanza Afrika na ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii. Ya kwanza ni Brazil. Nchi zilizokuwa kwenye tano bora kwa utalii Afrika ni Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Kenya na Zambia.

22.Tz ina mbuga zipatazo 16 na ile mbuga maarufu kuliko zote duniani Serengeti ipo Tanzania, mbuga iliyopakana na bahari iitwayo Saadani ipo Tanzania na mlima mrefu kuliko wote Africa Kilimanjaro upo Tanzania.

24. Tz ina ardhi kubwa yenye rutuba na inayofaa kwa kilimo cha mazao mengi tofauti tofauti. Mashamba makubwa ya mpunga kwa mfano yaliyokuwa chini ya Shirika la NAFCO yalitoa mazao ya kulisha Tanzania na pia nchi nyingine.

24.Tz ina gesi ya asili ya Carbon Dioxide (CO2) inayovunwa kule Kyejo, Rungwe-Mbeya na kampuni ya TOL. Gesi ya asili ya cardon dioxide inatumika sana kutengenezea vinywaji laini kama soda, bia na pia kutengenezea madawa, makaratasi na kutibia maji (water treatment).

25.Tz ina gesi ya asili inayopatikana katika kisiwa cha Songo songo mkoa wa Lindi. Gesi hii imekuwa ikichimbwa na kusafirishwa hadi Dar es salaam tangu mwaka 2004. Inamilikiwa na kampuni ya Songas ya Uingereza.

26.Tz imengundua gesi ya asili yenye zaidi ya meta za ujazo trilioni 55.3 iliyongunguliwa katika maeneo ya bahari ya Hindi na Mtwara.

Pamoja na sifa zote hizi lakini Tz ni nchi iliyo kwenye kundi la nchi maskini duniani ambayo asilimia kubwa ya raia wake wanaishi chini ya Dola moja za Marekani na hali ya huduma za kijamii ikiwa duni.
 
Mkuu@ Mwanakijiji, kwanza nikupongeze kwa bandiko kama hili. Maudhui ya bandiko lako yanafikirisha sana.

Hata hivyo, inatufundisha kila mtu kufanya kwa nafasi yake na wakat wake yale yanayompasa kutenda bila kuhukumu watu wengine wanaojitahidi kuonyesha njia kwa kutumia mapungufu yao.

Kama tunavyohubiriwa makanisani na misikitini, tusiangalie matendo ya viongozi wetu ila tusikilize wanachohubiri. Ni dhahiri kuwa anenacho mtu ndicho kilichojaa moyoni mwake.
 
Maendeleo sio jambo la kuamka asubuhi na kukuta kila kitu kipo sawa,bali huchukuwa miaka kadhaa,awamu na awamu,raisi na raisi.Hamna aliye kamili bali dhamira njema iliyopo kwa kiongozi juu ya taifa lake ni msingi mzuri kwa maendeleo ya dhati.
 
Anayedhani Magufuli – pamoja na jitihada zote anazofanya – atamaliza matatizo yetu yote naye huyo ni muota ndoto. Magufuli naye ana mapungufu yake. Mapungufu haya hata hivyo hayamfanyi apoteze mwelekeo au aone hafai kufanya lolote.
Mkuu Mzee Mwanakijiji, kwanza asante kwa bandiko hili, mimi ni muumini wa life after life, na mambo ya reincarnation, hivyo waumini wa nadharia hizi, kwao hakuna kitu kinachoitwa a coincidence, kuwa limetokea jambo fulani tarehe fulani na siku hiyo hiyo, tarehe hiyo hiyo likatokea jambo jingine mahali pengine, as just a coincidence, it is not, hakuna coicidence hayo yote ni pre meditated moves, thanks for this!.

Nimefarijika zaidi baada ya kuona Mkuu Mwanakijiji unaanza kurejea back to your senses na kwa kuanza kuondoka kwa "jikombaring Mwanakijiji, na kurejea kwa "the objective Mwanakijiji" we used to know ambaye alikuwa akiandika with much objectivity ya kutanguliza mbele maslahi ya taifa no matter what!. Welcome back Mkuu Mzee Mwanakijiji!.

Nimeguswa rna huu ukweli wako bayana kumhusu Magufuli kuwa na yeye ni binadamu kama binadamu wengine, na sii malaika!, ana strengths na weakness zake kama binadamu wengine wote. Miongoni mwa mapungufu hayo ambayo wengi wanaiona kama ni streghth, ni suala zima la udikiteta uliopitiliza kiasi cha kukiuka haki za msingi za binaadamu ikiwemo ile ya "no body is condemned unheard", anawahukumu watu bila kuwapa fursa ya kusikilizwa!!.

Madikiteta wengine wote maarufu duniani, nao mwanzo walianza hivi hivi kwa kuwa ni populist leaders wakishangiliwa sana na umati wa watu!, lakini mwishowe yaliwakuta ya kuwakuta, hivyo akina sisi tunaoupigia kelele huu udikiteta wa Magufuli, hatumaanishi kumfanya apoteze mwelekeo, wala hatumaanishi hafai kwa lolote, bali tunamkumbusha tuu kuwa na yeye ni binadamu, mwenye madaifu fulani, hivyo wakati akiconcentrate kutumia strengths zake kuijenga Tanzania tuitakayo, asipuuze weaknesses zake, if hazitakuwa counter checked at early stages, no one can stop them huko mbele ya safari, akiachwa tuu kuendelea hivi hivi alivyo kwa kuwasikiliza tuu waimba shangwe za sifa na mapambio, by the time muda huo ukifika, it might be too little too late!.

Magufuli ni rais wetu, ni kiongozi wetu, tumuunge mkono kwa nguvu zetu zote kwa kumsaidia kufanikisha malengo mazuri aliyonayo kwa taifa letu, na msaada mkubwa zaidi kwake kwa sisi baadhi yetu, ni kumuonyesha mapungufu yake with constructive criticisim za kumkosoa ili kumsaidia kwa kumjenga zaidi na sio tuu kumsifia kwa kudhani ndio tunamsaidia kumbe ndio tunambomoa!, ndio maana kamwe hutatusikia baadhi yetu kama akina sisi tukiyazungumzia yale mapungufu yake mengine ya kibinaadamu ya yale mambo yetu yaleee!, kwa sababu na yeye pia ni binadamu kama binadamu wengine wote!.

Pasco.
 
MsemajiUkweli, umenifanya nipatwe na donge; kama nataka kulia hivi...
Ndio urudi kuwa critic kama ulivyokuwa. Magufuli hahitaji waimba pambio na wapiga makofi. Anahitaji watu wakumpush (kumkosoa, kumkumbusha) ili aweze kufanya hata zaidi. Sasa mkikaa kimya anapoharibu, kumtetea wanapomkosoa wengine na kumsifia anapotimiza wajibu wake unakuwa hauna tofauti na lumumba buku seven. Campaign iliisha na uchaguzi vile vile, hivyo chukua nafasi yako ya kukemea na kuzungumzia mapungufu. Kusifu waachie wao. Ikifika 2019 anza tena kampeni.
 
MsemajiUkweli yaani Kuna vitu vingine hapo nilikuwa sifahamu tunavyo.

Kwa nini tu Tanzania bado ni nchi masikini?
Kwa nini Tanzania ni nchi inayopata misaada?
 
Big up sana, pamoja na mchango mkubwa wa mawazo wa mwalimu katika azimio la arusha lakini lilikuwa azimio lenye kujicontradict, kwa mfano utatangazaje kuwa maadui wakubwa wa nchi ni maradhi, ujinga na umasikini, halafu wakati huohuo uwazuie viongozi kuwa na nyumba za kupangisha? ( kwa mujibu wa TANU enzi hizo hata kiongozi wa nyumba kumi kumi naye sharti hili lilimkumba), sasa unazuia watu kutumia rasilimali walizonazo kujiondolea umasikini halafu unasema adui mmojawapo wa taifa ni umasikini?

Utazungumziaje usawa wakati mshahara wa raisi ulikuwa shilingi 4000( hii ni baada ya kuupunguza kwa asilimia 20 kufuatia maandamano ya wanafunzi wa chuo) ambapo yeye mwenyewe alikiri kuwa mshahara wa awali wa shilingi 5000 kwa mwezi ingemchukua mkulima wa kawaida miaka 12 kuufikia, hata hizo shilingi 4000 bado zilikuwa ni fedha nyingi sana hapo kuna usawa gani?

Utazungumziaje usawa wakati hutoi uwanja mpana wa kuleta " political alternative" kwa kulazimisha tuwe na mfumo wa chama kimoja, huku fikra za mwenyekiti zikiwa ndiyo dira?

Again contradictions za mwalimu zilikuwa in principles na wala si mazingira yaliyoinfluence, angeweza kutimiza ndoto yake ya " usawa" kwa kuruhusu uhuru mpana wa umma, na si kuwapeleka kwa mtindo wa Zidumu fikra za Mwenyekiti!

Tukija kwa Magufuli ni heri tukamkosoa kwelikweli kuliko kuimba pambio la kumsifu, kwa maana akifanya vizuri twanufaika, hilo ni jambo jema, ila tukikaa kimya au kuimba pambio kwenye altare yake huo ni uwoga "cowardice", Fikra zisizoona tatizo, au zinazoona tatizo kisha mahaba yakafunika maamuzi hizo wala hazina maana.
Hata mwalimu Nyerere alikuwa na waimba mapambio lakini je hali ilipokuwa ngumu mwaka 1980 -1985 mapambio yao yalilifaa nini Taifa?
 
Swali kubwa (million $ question) Magu anajua kuwa yeye ni binadamu tuu na anamapungufu yake?
Je anashaurika au anaajiona yeye ni alpha na omega?
 
Kiongozi anakuwa na maono na kuwaelekeza/kuwahamasisha wananchi wake kushiriki kwenye maono hayo, kama wananchi hawapo tayari kwa namna yoyote ile kuyafikia maono hayo ni Ngumu.
 
Ndio urudi kuwa critic kama ulivyokuwa. Magufuli hahitaji waimba pambio na wapiga makofi. Anahitaji watu wakumpush (kumkosoa, kumkumbusha) ili aweze kufanya hata zaidi. Sasa mkikaa kimya anapoharibu, kumtetea wanapomkosoa wengine na kumsifia anapotimiza wajibu wake unakuwa hauna tofauti na lumumba buku seven. Campaign iliisha na uchaguzi vile vile, hivyo chukua nafasi yako ya kukemea na kuzungumzia mapungufu. Kusifu waachie wao. Ikifika 2019 anza tena kampeni.
Message sent
 
Mkuu Mwanakijiji ahsante sana, pamoja na yote naomba nitie neno kidogo;
Pamoja na mapungufu ya kibinadamu ya viongozi hao wawili, kosa kubwa linalotendwa na jamii kubwa hasa hii yakwetu(watu weusi)

Ni kujaribu ku downplay personal weaknesses katika uongozi, kama ilivokuwa kwa Nyerere, weakness zake zilitudumaza na kuturudisha nyuma zaidi.

Kwa upande wa Magufuli, ana miss strong and smart advisers, watu makini waku amplify strengths yake na ku materialize intentions zake....hilo kwa hakika amekosa, ndio maana watu kama kina Pasco &Co wanamuona kama dicteta hivi.........

Tumsaidie Magufuli atatufikisha mbali...
 
Vizuri. Ila kalamu na karamu ni vitu tofauti kabisa. Tuanze kuithamini lugha yetu ndipo tutathamini vingine tulivyo navyo. Kuthamini lugha ni kuthamini utamaduni, kuthamini utamaduni ndiyo kujithamini wewe mwenyewe. Ndiyo, ina uhusiano mkubwa na maendeleo. Samahani, labda nasema haya kwa lugha kali, ni kwa sababu naona mtu Mswahili anafanya makosa ambayo hawezi kufanya katika Kiingereza kwa mfano. hii inamaanisha nini? Sijaona Mswahili akaandika solly, badala ya sorry! Tena tunamcheka sana mtu anayefanya kosa dogo tu katika Kiingereza....rejea Magufuli!
Tazama, umetaja mali nyingi inamilikiwa na wageni. Tujiulize kwa nini? Miaka 60 ya uhuru hatukuweza kuwatoa wataalamu hata 10 wa kuchimba madini yetu? Hivi serikali nzima inashindwa kununua mitambo ya kuchimbia graphite kwa mfano?
No. Nadhani tatizo kubwa ni kutojiamini. Mtu mweusi, na si Mtanzania tu, ana tatizo kubwa la kinafsi, hata sijui kwa nini. Mara nyingi huwaangalia watu weusi wanapokutana kwa mfano na Mhindi, au Mzungu.....wee angalia tu anavyojichukua mbele ya watu hawa. Na hiyo inapokuja kwa viongozi ndiyo inakuwa hatari kubwa. Matokeo yake serikali zetu ziko tayari kumlipa Mzungu mamilioni ya fedha kufanya kitu ambacho Mtanzania anakiweza. Na hata akimwajiri huyo Mtanzania, hamlipi hayo mamilioni.
Tangu miaka ya 60 tunapeleka watoto kusoma uhandisi Urusi, Yugoslavia, Uingereza nk. na wamesoma na hao hao Wazungu na Wahindi na hata kuwashinda darasani. Lakini hadi leo Barabara zetu, majumba yetu yajengwa na Mchina! Ninapofikiri hivi, nikichanganya na tabia zetu za kuuzana ( si ni ajabu kuwa hakuna race nyingine imeuza watu wake en mass kwa race nyingine tofauti isipokuwa Waafrika? Na mpaka leo twauzana)......naona tuna walakin!
 
Kweli Magufuli kama binadamu ana mapungufu yake. Kweli ni vema kukosoa anapokosea lakini kusifia anapofanya vyema. Mwisho wa siku tujue hatuna Rais Malaika. Kuna miaka kadhaa taifa limevurugwa kila sector ikiwemo siasa zetu. Uongozi bora unatokana na siasa safi lakini tumeshuhudia uozo wa kutisha CCM uliotikisa taifa. Uozo huo ukasambaa na kuharibu hadi oppositions. Siasa kwa ujumla zimejaa fitna na unafiki zilizoanzia CCM. Hivyo tukubali mvurugano huu ndio unaotoa mawazo tuliyonayo leo. Hoja nyingi zimekaa kisiasa zile zilizotufikisha hapa. Critics wengi wamevurugwa na upepo mzima wa siasa chafu. Hii inapelekea ukosoaji mwingi kwa JPM ukose objective critics zaidi ya upambe kwa kisiasa. Wengine tunaweza kufikiriwa tunamtetea tu JPM lakini hatutetei mtu bali hoja zinazoibuliwa ambazo bado zimejaa uchafu ule wa mvurugano wa kisiasa uliodumu kwa zaidi ya miaka 15. Tunahitaji ukosoaji wenye mantiki na si kujipanga kupinga tu kila juhudi inayofanywa.
 
Kiongozi anakuwa na maono na kuwaelekeza/kuwahamasisha wananchi wake kushiriki kwenye maono hayo, kama wananchi hawapo tayari kwa namna yoyote ile kuyafikia maono hayo ni Ngumu.
je atawaunganishaje wapinzani wanoamini hakushinda alibebwa na tume, bado ana kazi kubwa , kukubalika kwa makundi yote
 
Back
Top Bottom