Miaka 13 ya ndoa lakini hajazoea familia ya mumewe/wakwe, inakuaje?

Kalaudi

Senior Member
Apr 16, 2017
112
100
Vipi mambo wakuu,

Eti inakuaaje mke wako hana mapenzi ya kutosha katika family ya mume? Na family inampenda sana mke hata akienda kwa wakwe anajifanya kama mgeni vile hazoei kabisa pale home ni miaka kama 13 hivi.

Ushauri please.
 
Kuzoea ukimaanisha nini?

Mama yangu hadi leo hana mazoea na bibi!!! Bibi akija nyumbani mama anajisikia kama ndo siku ya kwanza kukutana na wakwe! Anafanya kila kitu kwa umakini ili asimkwaze bibi. Sio kwamba hampendi bibi ila mambo ya mila yanamfanya awe mdogo akiwa kwa wakwe.
 
Jaribu kumdadisi mkeo. ..inawezekana kuna kitu walimuudhi, na familia yako hawajui wamemkosea pia wewe hujalitambua hilo. ..
Pengine hawezi kuweka wazi kwako akihofia kuweka chuki kati yako na nduguzo.....Muulize mkeo utapata jibu.
 
Mke anatakiwa akuzoee wewe mume n.a. watoto kama mumejaliwa FULL STOP

Unataka awazoee ndugu zako kwani wamemuoa?
Mnaenda kusalimu mnasepa pia kwa wewe usiwazoee wakwezo unaenda kuwasalim unasepa
 
Jaribu kumdadisi mkeo. ..inawezekana kuna kitu walimuudhi, na familia yako hawajui wamemkosea pia wewe hujalitambua hilo. ..
Pengine hawezi kuweka wazi kwako akihofia kuweka chuki kati yako na nduguzo.....Muulize mkeo utapata jibu.
Sikumbuki hata siku moja kama kulikua na Issue in between
 
Kuzoea na mapenzi nadhani Ni vitu viwil tofauti.

Kama mtu anamapenz hata siku ya kwanza tuu inajulikana.

Sometimes Huwa Ni hulka tu ya wanawake juu... Jaribu kumzoea na ndugu wajaribu kumzoea.....
 
Sikumbuki hata siku moja kama kulikua na Issue in between
Mwanamke mtu wa ajabu sana....jaribu kumuuliza.... kwa akili lakini. Usionyeshe kuchukizwa bali kuwa upande wake zaidi. ...atafunguka.
 
Kuzoea ukimaanisha nini?

Mama yangu hadi leo hana mazoea na bibi!!! Bibi akija nyumbani mama anajisikia kama ndo siku ya kwanza kukutana na wakwe! Anafanya kila kitu kwa umakini ili asimkwaze bibi. Sio kwamba hampendi bibi ila mambo ya mila yanamfanya awe mdogo akiwa kwa wakwe.
Uige tabia ya Mama ndoa yako itadumu
 
Kawaida mkuu, kujali na kuzoe vitu viwili tofauti. Labda shida iwe hataki hata kuwajulia hali, lakini kama anaulizia maendeleo yao basi anajali sio mbaya.
 
una mke mzuri na mwangalifu sana ,, akiwazoea tu jiandae kusukuhisha na kuwekwa kati uchague mke au mama..

uliza wanaume wenzio katika ndoa sehemu inayowapa tabu pale wakwe wagombane na mkeo aisee upo kati unaweza ona dunia chungu usimbe ufike hapo you will go crazy .. hongera kwa kuwa na mke mzuri
 
Unataka mazoea ya nn as long anawapa heshima wanayostahili inatosha,

Kuzoea zoea mtakuja kuzoea.......................................
 
Back
Top Bottom