Miaka 125 ya Jumba la Maajabu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 125 ya Jumba la Maajabu...

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Kibunango, Sep 20, 2008.

 1. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Leo ni miaka 125 ya Jumba la Maajabu huko Zenj... Karibuni katika sherehe hii adhimu! Bonyeza hapa kwa detail. sherehe hizi zitadumu kwa mwezi mmoja..
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Sep 20, 2008
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kinachofanya hilo jumba kuwa la maajabu ni nini mkuu?
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kamanda tembelea hapa kwa majibu ya swali lako...
   
 4. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu Kibunango; Asante kwa taarifa.
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Sep 21, 2008
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Nimetembelea blog yako na kukutana na maneno haya yafuatayo:

  Nanukuu... Wataalamu wa histori ya Zenj wanasema umarufu wa jengo hilo umejengwa kwa sifa zifuatazo;-
  1. Ni jumba la kwanza Afrika ya Mashariki kuwa na Umeme.
  2. Ni jumba la kwanza Afrika ya Mashariki kuwa na lifti( elevator)
  3. Ni jumba la kwanza Afrika ya Mashariki kuwa na mfereji ndani ya nyumba( Bomba la maji)...
  mwisho wakunukuu.

  Je hayo ndo kweli yamesababisha kuwa jumba hilo kuwa la maajabu mpaka hivi leo?

  Hivi unamchukuwa mtoto wako aliye zaliwa karne hii na kumpekeleka hapo kisha unamfahamisha kuwa hili ni jumba la maajabu, atakuelewa kweli? Kisa ni jumba la kwanza Afrka mashariki (wengine wanasema in Sub-Sahara Africa)kuwa na umeme, lift na bomba la maji ndani.

  Kwani haitoshi tu kuelezea kuwa ni Jumba la kwanza Afrika mashariki kuwa na vitu hivyo mpaka tuongeze neno maajabu? Labda nashindwa kuelewa neno maajabu katika karne hii tulikuwa nayo sasa...!

  Anyway ahsante mkuu kwa taarifa yako...! Nikipata nafasi nitatembelea tena Jumba hilo linaloitwa Beit al Ajaib...!
   
Loading...