Miaka 100 ya Baba wa Taifa Mwalimu JK Nyerere: Tumkumbuke pamoja baadhi ya aliokuwa nao

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,906
30,248
Nimekaa toka asubuhi na mapema nafikiria vipi tutamkumbuka Mwalimu Nyerere katika karne moja lakini pamoja na yeye tuwakumbuke wenzake ambao baadhi yao hawajulikani kabisa.

Nikaingia shambani kwangu kuangalia labda ninaweza kuchimba shina moja la muhugo nikachemsha ninywee chai.

Shamba langu ni hii Maktaba yangu.

Nikaona picha ya safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere anakwenda UNO Februari, 1955.

Picha hii ikanilletea katika kichwa changu kumbukumbu za wazee wangu wawili wote wametangulia mble ya haki - Ally Sykes na Jim Bailey.

Ally Sykes ndiye aliyenitambulisha kwa Jim Bailey na Jim Bailey akanipa kitabu chake cha picha kuhusu Nyerere nifanye uhariri wa makala na maelezo ya picha na nimtafutie mchapaji, yaani publisher.

Picha hii nimeipata katika ya safari ya Nyerere UNO nimeikuta katika mswada huu.

Bailey amenikumbusha Zuberi Mtemvu ambae Bailey katika mazungumzo yetu aliniambia alikuja Dar es Salaam kutoka Afrika Kusini kuhudhuria uhuru wa Tanganyika tarehe 9 Desemba, 1961.

Bailey akaniambia kuwa Mtemvu alikuwa rafiki yake sana na alimwazima gari yake atembelee alipokuja kuhudhuria sherehe za uhuru.

Zuberi Mtemvu ananikumbusha Uchaguzi wa Kura Tatu na ugomvi wake na Nyerere hadi kupelekea yeye kujitoa TANU na kuunda chama chake cha African National Congress.

Zuberi Mtemvu na Nyerere walitoka mbali sana.

Mzee Mtemvu alikuwa mzungumzaji wangu sana.

Ameniambia kuwa yeye alijuana na Nyerere kipidi kilekile Mwalimu alipofahamiana na akina Sykes yeye akiishi Mtaa wa Somali (sasa Mtaa wa Omari Londo).

Mwalimu ndiye aliyemshawishi aache kazi ili aitumikie TANU na ilibidi Mwalimu azungumze na baba yake Mtemvu, Mzee Mwinshehe Mmanga kwani Zuberi alikuwa kijana mdogo sana.

Mwangalie kwenye picha hiyo ya mwaka wa 1955 akiwa na Nyerere uwanja wa ndege wa Dar es Salaam.

Zuberi Mtemvu ni huyo wa tatu kutoka kushoto.

Nilikuwa kila nikizungumza na Mzee Mtemvu katika majlis yetu nyumbani kwa mama yetu Bi. Siti Kilungo hakosi kuwataja watu wawili kwa sifa tofauti - Julius Nyerere na Robert Makange.

Mzee Mtemvu akimpenda sana Robert Makange aliyekuwa mmoja wa wahariri wa gazeti la Mwafrika.

Mtemvu ndiye aliyemwingiza Ali Mwinyi Tambwe Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika TANU mwezi August 1954.

Makange ni huyo aliyesimama kuliani kwake Mtemvu.

Waingereza walimfunga Robert Makange na Rashid Kheri Bagdelleh kwa ajili ya kalamu zao katika gazeti la Mwafrika.

Baada ya Makange ni Rashid Sisso rafiki mkubwa wa Mwalimu.

Sisso kashika kikapu cha ukili.

Mwalimu alimpa lakabu akimwita, ''Afisa.''
Rashid Sisso alikuwa akisimama nyuma ya Mwalimu katika mikutano.

Basi Mwalimu atazungumza, atazungumza, atazungumza kisha atasimama kidogo atageuza shingo atamuuliza Sisso, ''Unasemaje Afisa?''

Hapo Sisso atapiga ukelele na Uwanja wa Mnazi Mmoja utalipuka.

Nyerere na Sisso hao.

Bi. Hawa bint Maftah na Bi. Titi watapokea kwa nyimbo ya, ''Mweshimiwa nakupenda sana Wallahi sina mwenginewe In Shaa Allah Mungu yupo Tanganyika tutajitawala.''

Mtu alikuwa habaki nyumbani siku ya mkutano wa TANU labda kama mgonjwa. Mwalimu ndiye huyo hapo katikati ya Iddi Faiz Mafungo na John RupiaM

Mzee Rupia maarufu nani asiyemjua?
Makamu wa Rais wa TANU na mfadhili mkubwa wa TANU.

Iddi Faiz Mafungo si kwa bahati mbaya kuwa pembeni ya Mwalimu.

Iddi Faiz alikuwa Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na pia Mweka Hazina wa TANU na ndiye aliyekabidhiwa kazi ya kukuanya fedha za safari ya Nyerere UNO.

Iddi Faiz alihudhuria mkutano wa uzinduzi wa TANU katika Ukumbi wa Arnautoglu.

Haifahamiki kwa hakika hasa ni lini Iddi Faiz alijiunga na TANU kwa sababu kadi yake ya kwanza ya uanachama ilipotea na akapewa kadi nyingine iliyokuwa na namba 915 iliyotolewa tarehe 28 Agosti, 1954.

Lakini kwa kukisia tu kutokana na kadi ambayo Idd Faiz mwenyewe alimwandikia kaka yake Iddi Tosiri no. 25 na yenye saini yake inaweza kuchukuliwa kwa uhakika kuwa Iddi Faiz alikuwa miongoni mwa wale watu wa mwanzo kabisa kuingia TANU na huenda akawa miongoni mwa wanachama 20 wa mwanzo.

Nimeona katika kumkumbuka Baba wa Taifa itapendeza sana tukawakumbuka pamoja na yeye hawa wazalendo wengine waliofanya makubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika lakini historia imewasahau.

1648464955187.png
 
Asante kutukumbusha. Kumuenzi Baba wa Taifa:CCM, Serikali, Viongozi na Watanzania kwa Ujumla, Je Tunamuenzi Baba wa Taifa kwa Mawazo, Maneno na kwa Vitendo?, Tunamuishi?.
Nawatakia maadhimisho mema na mapumziko mema ya Nyerere Day.

P
 
Mzee Mujengi Josephat Gwao - Nyerere ktk harakati za kupigania uhuru na ujenzi wa taifa, alishirikisha jamii

Mzee Mujengi Josephat Gwao (88) amepitia na kuona mengi kwa nafasi zake ktk kutumikia jamii, alishiriki siasa kama katibu mkuu msaidizi CCM, katibu mkuu msaidizi TANU, katibu wa TANU wa wilaya na District Commissioner, makamu wa rais Tanganyika Labour Federation, executive officer wa Nyaturu halmashauri (Council)

1955 Mzee Makongoro na nyimbo zake , Bibi Titi Mohamed na hotuba zake motomoto , Saadani Abdul Kandoro wa jimbo la kati karani wa mahakama, Rajab Kundya mfasiri wa mahakama (court interpreter ..

Uamuzi wa Sahihi wa Tabora 1958 wa kura 3 ulioafikiwa na TANU katika uchaguzi wa vyama vingi Tanganyika. Ahadi kuu ya mwana CCM /TANU ya Nitasema Ukweli Daima Haipo ....
Source : Dar24 Media,
 
Back
Top Bottom