Miaka 10 ya Utumishi: Kumbukizi mbaya ya matumizi ya pesa isiyofutika katika historia ya maisha yangu

Mkuu pole sana ila bado una nafasi umeshtuka mapema.

Me nilichokigundua mpaka leo kwa wa tz wengi wanapopata kazi huwaga hawana vision tena Baada ya pale,ndio maana tz mpaka leo watu wake bado wanaangaika kila siku wachache watakao jitambua kama wewe wanatoboa.

Sio kwamba uku pata washauri mkuu ,wewe kama wewe unatakiwa uwe na vision ya maisha yako kama ulivyoweza kutoboa mpaka umepata kazi umefika hapo ulipo,ulivyofika hapo ulikuwa na washauri?

Usipende sana kujilinganisha na wengine hao unaweza ukakata tamaa focus na maisha yako huku ukiwa unapanga malengo yako tu,na jifunze kuwa mbahili saizi kwenye kutafuta.

Hali uliyokutana nayo iko kwa wantanzania wengi ndio akili zetu hizo ,ndio maana mpaka leo raia tupo busy kutafuta halafu bado maskini.

Mkuu nakushauri hiyo kazi usiache mpaka mwenyewe waseme wewe basi kuendelea baada ya hapo amia kwenye biashara zako.

Maisha yana kuwa easy sana kama unakuwa unajiwekea malengo kwa kila hela utakayo ipata,ndio maana wazungu wanatuzidi,wazungu wengi wakipata kazi tu wanajua tayari vitu gani wanahitaji muhimu kuwa navyo kwenye maisha yao,kitu kama mke ,nyumba,kiwanja biashara za kufanya.sio sisi ,sisi tunatumia kinaisha kesho tunaanza upya.

Hongera pia mkuu umejitambua mapema,wengine mpaka anastafu ndio anaanza kujilaumu nilikuwa nachezea hela kumbe.

Vijana wengi wakipata kazi wanaangaika kwanza na simu za milioni 2,3. Mpaka unashangaa huyu hela yake hana matumizi mengine hizo simu za gharama utanunua tu fanya mambo ya msingi kwanza jipange kimaisha kwanza ,ukimshauri hakuelewi na hela anazo utamwambia nini?

Kwa sababu usipo fanya vitu vya muhimu saizi kwenye maisha unakuwa unajichelewesha wewe mwenyewe maana baadae utatakiwa uwenavyo na wewe wakati huo huna hela,utabaki tu kujilaumu.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mimi na mwaka huu natimiza miaka 21 ya utumishi nina umri wa miaka 37 tu nimeajiriwa nikiwa mdogo mno umri wa miaka 17 tuu nikabahatia....aisee yangu mm makubwa mno nimepitia mengi mno nimeona mengi mno tena ya kutisha sana, maisha ni safari ndefu naweza sema nita staafu nikiwa bado nguvu ninazo za kutosha nina miaka 10 tuu mbele ya kustaafu hii kazi...Labda waniongezee mkataba wakiniongezeea nakataa sitaki mana nisije kufa bure......
 
kazi gani hiyo uliyoajiriwa ukiwa na umri wa miaka 17 mkuu?
 
Maisha haya! Ila imekua safi sana kujishtukia mapema mkuu bado una umri wa kufika unapotaka. Ila Mungu huwa hakupi wala hakunyimi vyote yani wakati unasema umechoma hiyo hela kwa kukosa mshauri au msimamizi ye amekubariki na huyo mwanamke makini, ni vema kushukuru kwa hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kosa sikufanya kosa, kosa ni kurudia kosa! Bora umejitambua muda haujaenda sana. Nakutakia la kheri kwenye maisha yako baada ya kujipanga upya!

Dah nimeipenda sana hii waswahili usema maji yakimwagika hayazoleki lkn hapana tunatakiwa tuanguke mpk mavumbini kabisa ili tunyanyuke na kuanza upya.

Maisha hayawezi kunyooka tu hata unayemuona anamafanikio fulani kuna changamoto amezipitia hakuna maisha Yaliyo smoth kwa binadaam yoyote yule

Chamsingi una mikono na miguu na mwenyezi Mungu kakupa afya njema na akiri mafanikio yatakuja tu ukipambana changamoto ni sehem ya maisha kwa mwanaadam yoyote yule
 
Nina washkaji waliofanya hayo makosa mimi sijafanya ... nilipata ajira soon tu nilivyomaliza chuo mwaka 2017 mwezi wa 11 nilifanya interview ya kwanza mwaka huohuo Mungu sio Paskali mayalla nikapata ...kama unajua kazi zetu hizi za majitoleo ( Mwalimu ) mshahara sio mkubwa yani hizo posho zako tu umeuzidi mshahara wangu wote 😂 ( life’s not fair) ukiangalia walimu wako wengi mtaani lol salaale unajikuta umesema ndio nimekubali hata kabla hajamaliza kutaja kiasi atakachokulipa ...

To cut the story short nilikutana na manguli wa Taasisi watu wana miaka takribani 10 mpka 15 ila hakuna hata mmoja aliyefanikiwa kujenga... wanaomiliki ndinga ni kama hizi za kutangazia matangazo ya dawa za asili sokoni ( mikweche haswaa ) ... na stori ikawa ni hiyo kwamba kumiliki nyumba ( kibanda) ni sawa na Ngamia kupita kwenye tundu la sindano ( haiwezekani ) mzee wa mlengo wa kulia ikabidi ni pige hesabu bila kutumia mshahara wangu kwa mwaka napata mil 7 hivi ina mana kwa miaka miwili mil 14 ...

kweli bwana nikawa nakula kwa mwezi 90000 tu ndio tisini elfu hujakosea ( kula katikati ya wiki unakula shule asubuhi na mchana ) kodi unalipiwa na shule ikawa ndio utaratibu wangu baada ya kipindi cha mwaka nikapiga msingi na nikaacha na tofari mwaka huu nimeipandisha mpka renta jumla kama mil 8 hivi ... ninapofanya kazi hakuna anaejua wala kuhisi mana hata picha nikipiga na save iCloud ...

Bila ya hii KORONA ningepauwa tena na Roman versatile basi tu ... usiache kazi mzee biashara mueke mkeo mana umesema amekuzidi maarifa
 
Hongereni wakuu kwa kila hatua mnazopiga tupo pamoja na poleni kwa maswaibu mbali mbali yanayojitokeza ktk maisha kutokana na kujisahau.
Binafsi ningependa kutoa ushauri,kitu starehe,yaani pombe + mademu ni adui mkubwa sana wa maendeleo.ukitaka mafanikio ipende pesa na uieshimu na rafiki wa kweli ni pesa yako ,tunza pesa ,tunza pesa kamwe haitakutupa.

Anasa ni mbaya sana kwenye maisha,tuwape elimu walio chini yetu wasije situka kumekucha
 
Kuna mda huwa tunafanya makosa mengi sana katika maisha tena mengine ya kujitakia kabisa ambayo ukiyakumbuka baadae unayajutia sana. Binafsi kama ningetumia mda vizuri ningekuwa mbali sana sana kimafanikio kuliko nilivo sasa.

Kipindi namaliza O' level baada ya matokeo kutoka nikapangwa Moshi Technical kwa elimu ya Advance, nikabadili kwenda Dar Es Salaam Institute of Technology (DIT) kusoma FTC kwa miaka 3, nilipomaliza tu nikaunganisha degree MIST, nikiwa semister ya kwanza na umri wangu wa 21yrs naelekea 22 mungu akawa upande wangu nikaajiriwa nikiwa kijana mdogo kabisa nikiwa na 21 kama technician katika moja ya taasisi inayolipa vizuri sana hapa nchini ikabidi niahirishe chuo kwa mda niingie kwenye ajira hii ilikuwa 2009 mwishoni, kwa kipindi hicho kwa hiyo level yangu nilikuwa nalipwa 840k kama mshahara kwa mwezi, bado kulikuwa na housing Allowance 240k,Transport allowance 200k, posho ya mawasiliano 60k, Lunch 150k na Extra duty ambayo hii tulikuwa tunaingiziwa wafanyakazi wote sawa kila mwisho wa mwezi 350k kwa kipindi hicho.

Ofisi ilikuwa inatoa mikopo kwa wafanyakazi wake wapya ya bila riba za kujengea nyumba, kwa level yangu kipindi hicho nilikopeshwa 48m na zikawa zinakatwa kwenye posho na sio kwenye mshahara. Kiukweli kitu ambacho ninakijutia mpaka leo nikikumbuka naumia sana basi ni miaka yangu 4 ya mwanzo kwenye ajira (2009-2012) nilipoteza pesa nyingi sana kwenye mambo ya kijinga kabisa na badala yake nikawa mtu wa hovyo sana kuliko kipindi chochote katika maisha yangu, nadhani umri na kutopata washauri wazuri pia kulichangia hili.

Nilipopangiwa kituo changu cha kazi nilipewa 3+m za kujikimu, karibia robo tatu za hizi pesa nilitumia kujivinjari na wasichana wa CBE waliokuwa wananitolea nje kipindi cha zamani na hata nilipopewa pesa ya mkopo wa ofisi sikuweza kufanya la maana kubwa la kuweza kujivunia japokuwa kiasi cha pesa katika huo mkopo nilitumia kuwajengea na kukarabati nyumba ya zamani ya wazazi na mwaka uliofuata nikakopa CRDB tena 15m kupitia mshahara wangu, kipindi nakopa hii pesa nilikuwa nakaribia kwenda likizo yangu ya mwaka na asilimia 80 ya hizi pesa niliitumia kwenye starehe na wanawake kwenye hoteli tofauti tofauti, Sasa nikawa nakatwa kwenye mshahara na posho zinakatwa kulipia madeni ya mkopo nikawa napata kiasi kidogo tu japo kwa matumizi ya kawaida kilikuwa kinatosha kwa kujibana ikizingatiwa wazazi nao tayari nilikuwa tegemeo lao, Nikaanza kuishi kwa kutegemea zaidi per diem za safari za kikazi.

Mwaka 2011 nilimpa mdada mmoja mimba alikuwa anamalizia diploma yake TPSC ikabidi nikae nae kama mke wangu hata hatukufanya harusi mwenyewe hakutaka kabisa japo wazazi wa pande zote walitaka tufunge harusi kanisani na sherehe ifanyike na kiukweli hata uchumi wangu ulikuwa hauruhusu hili nadhani wife alisoma upepo mapema , Nilimshirikisha Mkurugenzi wangu tulichoafikiana na mwenzangu kuhusu ndoa yetu na jinsi ya kupata cheti cha ndoa ili aweze kupata bima ya afya kupitia kazi yangu kama mke wangu halali, Wakubwa wanajuana bhana, usiku wa siku hiyohiyo ananipigia simu akinitaarifu tujiandae kesho yake anakuja kutuchukua tukasaini cheti cha ndoa nadhani ilikuwa ni RITA pale kama kumbukumbu zangu ziko sawa, lilikuwa ni jengo la ofisi za mkuu wa wilaya na mle ndani ndo kulikuwa na hizo ofisi za RITA sikujua hata kimelipiwa bei gani hicho cheti tulisaini tu na mashahidi zetu wawili wa pale ofisini akiwemo mkurugenzi then tukachukua vyeti tukamrudisha wife nyumbani mimi nikaingia kazini kuendelea na majukumu na hapa ndipo maisha mapya yalipoanza.

Mwaka 2012 nikahamishiwa Arusha na kupewa ruhusa ya kuendelea na masomo yangu ya shahada ATC kwa kujilipia mwenyewe, hapa pia ndipo nilipoanza kufeel ule ugumu wa maisha na kuona utofauti kati ya akili ya kikubwa na kitoto.Posho zina madeni, mshahara una madeni, safari zimepungua kwa sababu niko shule nina mke,mtoto wote wananiangalia mimi , maisha yalikuwa magumu sana kwangu kwa kipindi hicho huku nikiona wenzangu tulioajiriwa nao waliokuwa na umri mkubwa kidogo wao wakiwa mbali sana kimaendeleo na wakawa wananishangaa mimi kuona Inawezekanaje kuishi maisha yale ninayoishi na kwa namna ile tunayolipwa huku nikiwa sina majukumu mengi.

Baada ya kumaliza chuo 2015, ikabidi nijipange upya na mkopo ukawa umemalizikia na hata biashara sikuwa nayo pamoja na kukopa pesa zote hizo na kuugulia maumivu ya mkopo kwa miaka 5 na dogo nae anatakiwa aanze kindergarten na tayari ana mdogo wake mwingine:D:D MAISHA HAYA. nikaanza kusuka mipango upya utafikiri ndio nimeanza ajira rasmi, Kibaya zaidi kipindi hicho wenzangu nilioajiriwa nao baadhi wako mbali sana, wana familia, wana nyumba nzuri, wana gari na biashara zao wakati mimi nimepanga chumba kimoja tu wakati huo mpaka namaliza masomo yangu ATC:cool:

Yale maisha na nikiwaangalia wenzangu itabaki kuwa kumbukumbu mbaya kichwani mwangu, uzuri nilitambua baadhi ya makosa yangu mapema nikajipanga upya nikiwa na akili ya kikubwa zaidi kuliko wakati ule, Japo sio sana ila somehow nime - win kidogo, lakini sio kama hatua walizo nazo wenzangu, ningekuwa na akili ya kikubwa kipindi kile ningekuwa mbali, mwaka jana nimetimiza miaka 10 ya utumishi wa umma nikiwa mwajiriwa na naelekea miaka 32 kiumri miezi michache ijayo bado ile kumbukumbu inagoma kabisa kufutika katika fikra zangu.unaweza kudhani natania lakini huu ndio ukweli kiasi ambacho nikikumbuka inaniuma sana hata kuandika hapa nakuwa kama napunguza mzigo wa maumivu wa ujinga wangu niliobeba moyoni

Pamoja na yote, mungu alinionesha mwanamke bora sana kwenye maisha yangu ambae hata sikuwahi kufikiria kumuoa ilitokea kama emergency tu hakuwa kati ya wasichana niliodumu nao kimahusiano kwa mda mrefu wala sikuwahi kumpenda, moyo wangu ulipenda kwingine kabisa na hata kwenye mipango yangu hakuwepo kabisa. Lakini kadri nilivoishi nae nimefahamu KWELI MKE BORA ANATOKA KWA MUNGU, mawazo yake yamebadili KABISA maisha yetu , kuna mda naona kabisa huyu kanizidi uwezo wa kufikiri hapa namzidi pesa tu, ni zaidi ya spiritual woman na mrembo haswa ni kivile tu wanaume huwa haturidhiki lazma tukaonje radha zingine nje.

Nashehekea miaka yangu 10 ya utumishi nikiwa na mtazamo mpya kabisa wa kuacha kazi ndani ya miaka 5 ijayo nijikite zaidi kuendesha miradi na biashara zangu niliyofungua ili kufikia malengo yangu niliyojiwekea. Kwa sasa ni baba wa familia, nina watoto kadhaa na mwanagu wa kwanza nimempata nikiwa na miaka 23 tu kwa sasa ana 8yrs anaelekea 9 miezi michache ijayo
Kama nakufahamu mdomo wangu..
 
Mwenzako mi mpaka leo najuta kwanini sikuenda kusoma Diploma vyuo vya ufundi nikaenda Form 5. Mkuu, hili ntajilaumu maisha yangu yote.

Anyway, maji yameshamwagika. Fresh tu.
 
Back
Top Bottom