Miaka 10 baada ya kumaliza chuo bado sina kazi

Sikuhizi ajira haiangalii degree shida ni kaxi chache,pia degree doesn't matter what matters ni connection yako au ikiwa na mtu wa kukushika mkono,Kuna ma Dr, ma nurse kitaa nao ni bad choice?
Tatizo siyo uchache wa kazi. Issue ni uwezo wa makampuni kuajiri umeshuka sana.

Kampuni liko tayari kuishi huku likiwa na upungufu wa watu kuliko kuajiri halafu, lisiweze kuwalipa.
 
Tatizo siyo uchache wa kazi. Issue ni uwezo wa makampuni kuajiri umeshuka sana.

Kampuni liko tayari kuishi huku likiwa na upungufu wa watu kuliko kuajiri halafu, lisiweze kuwalipa.
Uko sahihi ka taifa tinahitaji kuchagua viongozi wenye vision na utu wakuhurumia raia aisee. Inabidi kiongozi kuumiza kichwa kupunguza tatizo la ajira kwa Raia, na kuwa na kiupaumbele na kuijemgea uwezo private sector inayoajiri watu wengi, Ila sasa kiongozi asiye na maono kazi yake kuua tu private sector na mikodi ya hovyo.
 
Nilipata ajira serikalini bila CONNECTION yoyoteee.

Kipindi hicho tuna apply Sekretarieti ya ajira kwa barua za kuandika.

Sikua na connection yoyotee nikatuma maombi nikapata.

Nikaingia kufanya Kazi, nikarudi Shule (masters) na leo ni Afisa mkubwaaa tu.

Siri ni:-
Fanya Kazi kama hakuna KUFA na ombaa sanaa Mungu kama unakufa kesho.

Usiamini sanaa kwenye connection.

#YNWA
Afisa soma tena ile post, nimesema 80% na huo ukweli kila mtu anajua japo wapo 20% ambao wanapata bila connection. Me sitakaa niombe tena Ajira bora niendelee na biashara zngu,yaani nimepoteza muda sana kutafuta kazi ambazo kusema kweli hakuna na walimu na wazee walitupoteza kutuaminisha elimu ya darasani ni kila kitu,simply ni uongo.
 
Bila shaka umesoma Tumaini university Iringa maana mimi pia nimesoma kozi hiyo nilimaliza 2008, kwakweli sijawahi kufanya kazi nilichosomea tokea 2008 napata kazi nje ya field yangu. Nina Zaidi ya miaka 3 sina kazi lakini nimefungua biashara ya chips, mwanzoni wakati naanza niliuza mwenyewe ili kupata uzoefu na kujua faida inapatikanaje pamoja na changamoto.

Kwasasa nimeajiri vijana wa 3 maana nauza na chakula, mwanzoni ilikua changamoto maana nilikuwa naona niko low sana yaani kutoka kuwa na degree mpaka kukaangaa chips yaani nilikuwa sometimes najificha wakija jamaa zangu tuliosoma nao lakini nilipoanza kuona faida kubwa aibu ikanitoka kabisa nikasema nitakomaa humu humu.

Na nilikuja kugundua vijana wengi tunarudi nyuma kwa kuogopa kufanya kazi fulani kisa watu wanaotuzunguka watatuonaje pia hata elimu tunayopewa sio ya kutujenga, mzazi anakwambia soma uje kuwa boss, mwalimu nae anakujaza ujinga ukimaliza chuo unaanza ku face realities una data na kama una moyo flagile unajiua.
Hongera uli think beyond the scope
 
Pole mkuu, vijana wengi wanapitia katika mazingira kama yako awamu hii.
Tuendelee kuomba kipite hiki kipindi cha mpito
 
Nimemaliza shahada ya Utamaduni na Utalii (Cultural Anthropology and Tourism)

Naishi Dar es Salaam.

Ni miaka zaidi ya kumi sasa imepita bado nahangaika na maisha. Nimekuja hapa kuomba msaada wa kazi kwa yoyote atakayeguswa

Uzoefu:
  • Customer Services Represantantive
  • Sales Executive
Baada ya hapo nimejaribu kufanya biashara ila kwa sasa naona mambo ni magumu sana

Kwa yoyote mwenye connection anisaidie mwenzenu.

Nipo tayari kufanya kazi yoyote nje ya taaluma yangu.

Natanguliza shukrani zenu.
Noma kweli
Miaka 10
 
Miaka 10 bado unawaza kuajiriwa? Watu weusi sisi sijui tukoje.
SWALI LAKO LIMENIFANYA NICHEKE MDAU INGAWA NI HUZUNI SANA KWA MTOA MADA. ILA NGOJA NISEME HIVI: KINACHOITWA AJIRA LEO HII NDIYO HAPO AWALI KILIITWA UTUMWA! HILI JAMBO NIMELIWAZA ASUBUHI YA LEO TU.
 
MDAU NGOJA NIKWAMBIE JAMBO, DUNIA INAKULIPA KWA KILE UNACHOFANYA NA SIO KUJUA. ALISEMA HAYA OLIVER NAPOLEON HILL "The world will pay you for what you do, and not for what you know". KASOME KITABU KINACHOITWA SIXTEEN LAWS OF SUCCESS AMEANDIKA HUYU HUYU NAPOLEON, KUNA JAMBO UTALIONA KABLA HAUJAMALIZA KUSOMA KITABU
 
Kuna vitu vingine sio vya kusomea kabisa...unakuta wengine wanasoma B.A Philosophy etc etc...hadi huruma hata kama hauna washauri unatakiwa usomee kitu ambacho ni broad...sijisifii nomesoma LL.B lakini sijawahi waza hata siku moja kufanyia kazi nilichosomea toka nimemaliza chuo miezi 2 tu nilipataga kazi bila connection, nikaachaga nikapigika kitaa nikatafuta ingine bila connection, kazi ikaisha nikarudishi shule kimtindo baadae nikapata ingine bila connection na haina uhusiano na nilichosomea ila wengi wanapendaga sana kufanyia kazi walichosomea...ndo kinachowacheleweshaga
 
The only problem I see is that you are hell bent on getting employed.

You are still keen to waste more time waiting to be employed. Man, that's daft.

Hebu chagua kijiwe, tafuta toroli, nunua matunda ya buku ten na packaging then yaoshe ukate kate fasta uuze kwa wapita njia.

Anza popote just don't remain in the same spot you are.
Kama kuna friji, nunua vifuko vya 1,500, vikaze, weka kwenye freezer vigande haswa jiwe, 200 kila moja, masokoni..mauzo muda wa asubuhi..

Tembeza vitu vya kutuliza joto mjini, maji, soda, juice, kofia, vitaulo vidogo..
Matunda, haswa tikiti maji, apples, zabibu..

Mkaa bado dili mjini...

Achana na ajira, acha uvivu wa kufikiri ndugu..
 
Nyumbani kwangu kuna degree holders wanne na diploma moja. Hakuna ajira !!. Na nyuma yao kuna mabinti zangu wapenzi watatu wako O level . Mpaka navunjika moyo kuwaendeleza mabinti zangu.

Kwa kweli suala la ajira ni shida
Kama uwezo upo wasomeshe to degree level, watakuwa na uwezo wa kuogelea katika bahari ya maisha itakayo kuwa na mawimbi makubwa kuliko tuyaonayo leo, ambamo hata ambaye hakuhitimu msingi anaweza kuogelea(mfano hai tuna wabunge). Msomi ana uwezo mpana wa kuzichambua changamoto kuwa fursa. Tusione mafanikio ya wachache ambao hawakusoma kuwa ndio kipimo na kuwa elimu haina nafasi katika mafanikio.
 
Mr/s. kamwamu sijawakatia tamaa hao mabinti. Nitawafikisha katika uwezo wao wa uelewa. Kati yao atakayeonyesha uwezo atafikishwa ktk matarajio yake, Labda washindwe wenyewe.

Lakini changamoto ya ajira inavunja moyo. Nafasi chache zilizopo wazee wamezikalia.
 
Kiukweli zipo kozi ambazo ajira ni less than 5% kwa wahitimu wake na bado vyuo vinadahili mamia ya wanafunzi.

Uhuni wa vyuo kutunga kozi ili kupata ada na wanafunzi ulipaswa udhibitiwe na Tume ya vyuo vikuu kwa kufanya tathmini ya ajira kwa wahitimu wake ili kama haina soko basi ifutwe au wasomeshe kiasi cha soko.

Poleni. Nadhani ni vyema mkalalamika tume ya vyuo vikuu ili kozi hiyo ifutwe ili wengine wasiendelee kupata hii hasara.

Zipo kozi kuanzia unaanza mpaka unamaliza waliokutangulia hawajapata kazi.
 
Kama kuna friji, nunua vifuko vya 1,500, vikaze, weka kwenye freezer vigande haswa jiwe, 200 kila moja, masokoni..mauzo muda wa asubuhi..

Tembeza vitu vya kutuliza joto mjini, maji, soda, juice, kofia, vitaulo vidogo..
Matunda, haswa tikiti maji, apples, zabibu..

Mkaa bado dili mjini...

Achana na ajira, acha uvivu wa kufikiri ndugu..
Ahsante kwa ushauri
 
Kiukweli zipo kozi ambazo ajira ni less than 5% kwa wahitimu wake na bado vyuo vinadahili mamia ya wanafunzi.

Uhuni wa vyuo kutunga kozi ili kupata ada na wanafunzi ulipaswa udhibitiwe na Tume ya vyuo vikuu kwa kufanya tathmini ya ajira kwa wahitimu wake ili kama haina soko basi ifutwe au wasomeshe kiasi cha soko.

Poleni. Nadhani ni vyema mkalalamika tume ya vyuo vikuu ili kozi hiyo ifutwe ili wengine wasiendelee kupata hii hasara.

Zipo kozi kuanzia unaanza mpaka unamaliza waliokutangulia hawajapata kazi.
Ni kweli
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom