Mhusika MKUU wa Msiba wa KANUMBA ni Wasanii wenzake au Familia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhusika MKUU wa Msiba wa KANUMBA ni Wasanii wenzake au Familia?

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by mzee wa njaa, Apr 9, 2012.

 1. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Muhusika wa Msiba wa KANUMBA ni Wasanii wenzake au Familia?

  Najiuliza sana hili swali pasipo kupata jibu lililotimia, kwani kila chombo cha Habari kinasema au kinataja Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ya KANUMBA ni Wasanii wenzake na hapo ndipo ninapopata Mashaka.

  Kwa Mtazamo wangu Mazishi ya KANUMBA yanatekwa au kuporwa na Wasanii wa Filamu. Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi la leo. Rais wa Tanzania JK ametoa angalizo ya kwamba: Waache wana familia ya Kanumba washughulikie na waamue ni sehemu gani ya Kuzikwa kijana wao. Kwani alishaona dalili ya Wanafamilia kuingiliwa kwenye Maamuzi ya Maziko.

  Tunafahamu Watanzania wana majonzi kwa hili ila kwenye ukweli hatutoacha kusema.

  Tupo pamoja katika majonzi ya kijana Wetu kanumba na Nawatakia pole wana familia nzima ya Kanumba na Mungu awalinde na awafariji katika kipindi hiki Kigumu.

  R.I.P Kanumba.

  Ni Maoni na Mtazamo tu.

  Asante.
   
Loading...