Mhubiri wa Kiislamu Indonesia adaiwa kueneza picha za utupu

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Polisi nchini Indonesia wamesema mmoja wa wahubiri wa Kiislamu wenye msimamo mkali nchini humo ni mshukiwa katika kisa cha usambazaji wa ujumbe na picha chafu za ngono.

Rizieq Shihab anatuhumiwa kutuma ujumbe wenye maneno mazito ya mahaba na pia picha za utupu alipokuwa anawasiliana na mwanamke mmoja.

Mhubiri huyo, ambaye kwa sasa yupo nchini Saudi Arabia, amekanusha madai hayo.

Bw Rizieq ni kiongozi wa kundi la Islamic Defenders Front (FPI), ambalo liliongoza maandamano makubwa dhidi ya gavana wa zamani wa mji mkuu wa Jakarta Basuki Tjahaja Purnama ambaye alifungwa jela kwa kosa la kuitusi dini ya Kiislamu mwezi uliopita.

Mhubiri huyo ambaye anafahamika sana kwa hotuba na mahubiri yake yenye ujumbe wenye kuzua utata, tayari amefungwa jela mara mbili awali kwa kuzua fujo na kuvuruga amani.

Katika kisa cha sasa, Bw Rizieq anadaiwa kukiuka sheria kali za kukabiliana na uenezaji wa ujumbe, picha au video chafu kwa kutuma ujumbe na picha kwa mwanaharakati Firza Husein, ambaye pia ametajwa kama mshukiwa.

Nakala za zilizodaiwa kuwa mawasiliano ya maandishi ya picha kati ya wawili hao kwa njia ya simu zilianza kusambaa sana mtandaoni mapema mwaka huu.

Polisi wamemwita Bw Rizieq mara kadha kwa mahojiano tangu Aprili lakini bado hajatii agizo la kufika kwa maafisa hao.

Mhubiri huyo amekuwa nchini Saudi Arabia na familia yake tangu mwishoni mwa mwezi Aprili.

Msemaji wa FPI ameambia Reuters kwamba madai hayo dhidi yake hayana msingi wowote na lengo lake ni kumhujumu mhubiri huyo.

Wakili wa Bw Rizieq amesema madai hayo yalibuniwa na wafuasi wa Bw Purnama, anayefahamika pia kama Ahok.

Bw Rizieq ni mpinzani mkubwa wa Bw Purnama.

Yeye na maafisa wengine wa FPI waliendesha kampeni mwishoni mwa mwaka jana dhidi ya Bw Purnama, ambaye ni Mkristo na raia wa asili ya China, na kudai kwamba hawezi kuongoza jiji la Kiislamu.

Bw Purnama alipogusia madai haya kwenye hotuba wakati wa kampeni za umeya Jakarta, alidaiwa kutusi dini ya Kiislamu, na maandamano yakazidi.

Alishtakiwa na kupatikana na hatia na kufungwa jela miaka miwili.
 
Back
Top Bottom