Mhubiri wa injili kitaani achezea kichapo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhubiri wa injili kitaani achezea kichapo!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by vukani, Jul 9, 2012.

 1. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2012
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Tukio hilo nililishuhudia hivi karibuni katika viunga vya Mwenge hapa jiji Dar wakati naenda Hospitali. Nilikuwa nimesimama kwenye duka moja la kuuza Dawa kuulizia dawa fulani ambayo niliandikiwa hospitalini. Upande wa pili wa barabara kutoka katika duka hilo kulikuwa na jamaa mmoja aliyejitambulisha kama Mtumishi wa Mungu, alikuwa akimwaga neno la Mungu, kuwaasa watu waache matendo ya Dhambi, na kumrejea Mungu.

  Jasho lilikuwa likimtoka kwelikweli na alikuwa akiongea kwa jazba kama vile anagombana, lakini katika mahubiri yake alikuwa akiwananga wapita njia hususan wanawake ambao walivaa vimini au suruali za kike.Ilikuwa kila akipita mwanamke mwenye kimini au suruali ya kike alikuwa akimwambia…….. ngoja nimnukuu hapa. ‘wewe mwanamke mwenye suruali acha dhambi, hayo mavazi uliyovaa hayampendezi mungu kamwe na ninakuhakikishia utakwenda motoni, na wewe mwanamke mwenye kimini na hakika hutauona uzima wa milele, utaishia motoni' mwisho wa kunukuu.

  Kibaya zaidi alikuwa akitumia kipaza sauti na alikuwa akiwafuata nyuma (hao wanawake) huku akiwamwagia maneno makali na ya kudhalilishaWakati akiendelea na mahubiri yake akapita dada mmoja ambaye alikuwa amefuatana na mvulana, sikuweza kujua kama walikuwa na uhusiano wa kimapenzi au walikuwa ni ndugu, yule mhubiri kama kawaida yake akaendelea kumwaga maneno ya kuwakashifu wanawake wenye kuvaa suruali.

  Kutahamaki nikamuona mhubiri kakunjwa shati na yule kijana, aliyekuwa na yule binti, mara ghafla yule kijana akaanza kumchapa makonde yule mhubiri mara kichwa, hajakaa sawa akalambwa mtama, mhubiri chali……………..Kisha yule kijana akamshika mkono yule dada, wakaondoka wakimuacha mhubiri akijizoa zoa pale chini. Niliondoka katika eneo lile maana umati wa watu ulianza kusogea katika eneo hilo ili kujua kulikoni.

  Kilichojiri nyuma yangu sijui.
   
 2. ummu kulthum

  ummu kulthum JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 2,791
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  saaafi sana,huwa wanakera anahukumu kama yy ndio anaenda peponi
   
 3. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Hahahahaaa
  Mi sisemi... Bado wale wanaokaa pale manzese wanaosema dini za wengine badala ya kuhubiri waumini wao maneno y SAW.
   
Loading...