Mhitimu wa shahada ya usimamizi wa biashara katika ujasiriamali. Nianzie wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhitimu wa shahada ya usimamizi wa biashara katika ujasiriamali. Nianzie wapi?

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Damson88, Sep 30, 2012.

 1. Damson88

  Damson88 JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2012
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu wana JF, mimi ni mhitimu wa chuo kimoja hapa nchini,nimesomea mambo ya ujasiriamali haswa hivyo inabidi nijiajiri mara baada ya kuhitimu na muda wenyewe ndiyo huu. Ubunifu ninao tena mkubwa sana bila kusahau kuwajari wateja au wanaohitaji huduma zangu. Mfano-na design website, fundi computer n.k. Sasa swali linakuja hivi:- nikiajiriwa(kama ajira zipo) ntafanya kitengo gani? maana mimi ni mtu anayepaswa kujiajiri. Je, mtaji wa kuanzisha biashara ntaupataje? Au niende jeshini TPDF? naomba mwongozo na mawazo yenu nayaheshimu sana. Ahsante!
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Sep 30, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mkuun unafurahisha sana, Bila shaka Utakuwa Umesoma MZUMBE UNIVESITY kitengo cha BBA-ED, Mkuu ni kweli kabisa hiyo Kozi ni mahususi kwa ajili ya Kujiajiri mwenyewe, Tatizo lina kuja kwamba Spirit ya Mtu kujiajiri inatakiwa ujengwe tangia mwanzo na si Chuoni, Hii inatokana na kuwa na mentality ya kuajiriwa tangu akiwa CHEKECHEA, SHULE YA MSINGI, SECONDARY NA HATA CHUO

  Walio kuwa wamekuzunguka kuanzia Majirani, Marafiki na hata Wazazi wote wana weza kuwa ni Wafanya kazi sasa shughuli ndo inaanzia hapo,

  Mkuu mimi sikushauri uajiriwe, na kwa sababu wewe umedai ni mtalamu wa Komputa unaweza tumia elimu ya Ujasirinali uliyo pata kutafuta Mtaji,

  Na Mkuu UNAPO KUWA NA MAWAZO YA KUJIAJIRI HUKU UKITAMANI AJIRA ZA KUAJIRIWA HUTAKAA UFANIKIWE KAMWE NA UTAKUWA UNAJIDANGANYA BURE, Mkuu kama Umedhamiria kujiajiri inabidi uweke Pamba masikioni na Uvae Miwani ya Mbao,

  Na unatakiwa kufanya haya

  1. Ikibidi Ondoa namba za Rafiki zako wote ambao unazania watakufanya ndoto zako za kijiajiri zisifanikiwe

  2. Badilisha namba ya simu ikibidi

  3. Badilisha Marafiki ikibidi, anza kutafuta marafiki wajasirimali, na sio wafanya kazi

  4. Epuka kuomba ushauri kwa ndugu jamaa na marafiki kuhusu kujiajiri labda tu unao waomba Ushauri ni Wafanya Biashara
   
 3. Damson88

  Damson88 JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2012
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu nakushukuru sana kwani hata hizi idea ndogo ndogo sikuwa nazo kabisa kumbe sasa hivi ndiyo macho yanaanza kufunguka. Ni kweli hujakosea kabisaa kuwa nimesoma Mzumbe BBA-ED, vipi nawe ulikuwepo au unajua waliokuwepo na sasa hivi wapo wapi haswa kwenye kozi hii?
   
 4. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #4
  Sep 30, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Ya walio soma Kozi ya Entreprenership wengi wao wako kwenye Mabenki na Tasisi nyingine na wapo walio Jiajiri, Ila nakushauri Ujiajiri mkuu ila ukisema Uingia kwenye Kazi kutafuta Mtaji hutakaa utoke huko kamwe,Vipi uko Dar?
   
 5. Dafo

  Dafo Member

  #5
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 1, 2012
  Messages: 70
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  mkuu ujasiriamali ni kama dini vile unapoamini kuwa kitu fulani ukifanya ndio kitakufikisha kwenye nchi ya asali na maziwa inabidi ujitoe kweli.kama alivyokushauri mkuu hapo juu,kuwa tayari kwa vikwazo kuanzia ngazi ya familia,jamii na marafiki kwa ujumla.unaweza kuwa umemaliza na wenzako chuo wamepata ofisi halafu unapishana nao njiani wakosmart na tai zao wewe ndo uko mtaani kwenye harakati zako za ujasiriamali na wakati mwingine unakuwa bado haujakaa sawa kifedha.inaweza ikakuumiza na kukurudisha nyuma lkn ndio changamoto hzo.
  Na pia tambua kwenye ujasiriamali huku uwe hardworking na creative kwa sababu unaanzisha system yako ya kufanya kazi na usimazi tofauti na unapoajiriwa unakuta system tayari ipo wewe unafuata procedures.
  Pia kuwa tayari kuanza chini hata kama nikidogo namna gani lakini kwa maono ya kukifanya kuwa kikubwa zaidi na kila siku uwe mtu wa kujifunza na usikate tamaa.
   
 6. Damson88

  Damson88 JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nashukuru tena mkuu, nia kweli ninayo na mara ntakapokuwa nimeanza ku practice huu ujasiriamali lazima nitakujuza. Ulichosema ni kweli ata bado naona wahitim wenzangu wanasema wanaanza kuajiriwa ili kutafuta mtaji na hapa mimi napaona pagumu na parefu, usiombe ikukute kama mtu anayetegemewa ili kusaidia familia kama mim hapa ndo maana najikuta nkiumiza kichwa sana..ushauri wako umenifaa sana. Nipo dar ndiyo mkuu
   
 7. Damson88

  Damson88 JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ahsante mkuu, hili jambo nina imani sikumbani nalo mim peke yangu bali ata wajasiriamali waliopo mtaani. Sera zetu bado zipo nyuma sana hadi tufikie hatua ya kuwezesha na kuboresha mazao/products za wajasiriamali bila kusahau inputs/rasilimali.
  Creativity najua lazima viwepo pamoja na mwenzake innovation.
  Mh. Dafo nashukhuru tena kwa ushauri
   
 8. Madiba

  Madiba JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2013
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 386
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 60
  Damson88, kwanza hongera kwa kusomea ujasiliamali. Nakubaliana kabisa na wadau wengine ambao wamekushauri hapo juu. Achana na kuajiriwa, go into practice ufanye huo ujasiliamali. Mwanzo utakuwa mgumu, na watu ambao wamekuzunguka watakusema sana, na kukubeza, kukuambia tafuta kazi n.k. Experience ya ujasiliamali utaipata ukiufanya... Ji-associate na watu ambao wanafanya ujasiliamali, wakupe mbinu... Kafanye biashara ya kulima vitunguu kule Ruaha Iringa, inalipa........
   
 9. lucky sabasaba

  lucky sabasaba JF-Expert Member

  #9
  Mar 27, 2013
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 1,672
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 145
  Kuna muhindi mmoja alikuwa mhasibu mkubwa sana kwenye hotel(burj al arab)baada ya kujua vizuri operations za hotel aliacha kazi,watu wengi walishangaa !!!lakini yeye alikuwa anajua alichokuwa anafanya...alielewa hotels zinaitaji vitu gani e.g bedsheets..curtains..bathrobes..slippers..notebook..pens..yaani vitu vingi sana ambavyo siwezikuviandika vyote..alichofanya akaenda kiwandani na kuchukua samples..ofisi yake ilikuwa gari lake(kwa kuanzia)alikuwa anatafuta tender hotelini hiyo ilikuwa 2005 akabahatika kupata tenda kwenye hoteli mbili ku supply linen...sasa hivi jamaa yupo juu sana hoteli nyingi sana hapa dubai huyu jamaa ndiye supplier mkuu wa mambo mengi..na kama ujuavyo dubai ni mji wa kibiashara hivyo hoteli ni nyingi sana...pia sasa anamiliki chain ya hoteli ndogondogo..pia bado anaendelea kuwa supplier wa vitu vya hoteli..anatembea na sample na vingine vipo kwenye picha ndani ya ipad(kumbuka yeye hamiliki hivi vitu..ila ukiangalia sample ukapenda atakupatia)huu ni ujanja ambao ata hizi website nyingi zinazouza vifaa online wanautumia..wengi wao hawana vitu wanakuwekea sample tu kwenye website zao ila utakapoitaji kitu ndani ya mda mchache watakutumia..na vitu vyao vinakuwa cheaper kuliko vya dukani maana dukani utalipa pango la duka..utalipa ushuru..utamlipa staff nk...hii nakwambia kwa mazingira ya dubai ambapo hoteli zinafunguliwa kila baada ya mda mchache...sasa homework kwako angalia kwenye mazingira uliyopo kitu gani kipo kwenye high demand..lakini kumbuka huwezikuiona good opportunity kwa macho bali uwa inaonekana kwa mind...hivyo tumia ubongo... kazi kwako kaka
   
 10. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #10
  Mar 27, 2013
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Sisi inatakiwa tuje kwako utushauri sio wewe unakuja kwetu kuomba ushauri.

  Inakuwaje mwarabu atoke kwao aje hapa kwetu Tanzania kutafuta Tende?
   
Loading...