Mhitimu Shahada ya Usimamizi wa Biashara katika Ujasiriamali. Nianzie wapi kujiajiri? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhitimu Shahada ya Usimamizi wa Biashara katika Ujasiriamali. Nianzie wapi kujiajiri?

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Damson88, Sep 30, 2012.

 1. Damson88

  Damson88 JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2012
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu wana JF, mimi ni mhitimu wa chuo kimoja hapa nchini,nimesomea mambo ya ujasiriamali haswa hivyo inabidi nijiajiri mara baada ya kuhitimu na muda wenyewe ndiyo huu. Ubunifu ninao tena mkubwa sana bila kusahau kuwajari wateja au wanaohitaji huduma zangu. Mfano-na design website, fundi computer n.k. Sasa swali linakuja hivi:- nikiajiriwa(kama ajira zipo) ntafanya kitengo gani? maana mimi ni mtu anayepaswa kujiajiri. Je, mtaji wa kuanzisha biashara ntaupataje? Au niende jeshini TPDF? naomba mwongozo na mawazo yenu nayaheshimu sana. Ahsante!
   
 2. N

  Nndu wa Selote JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 341
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Ndugu yangu, kama wewe uliyesomea ujasiriamali na una shahada kabisa unashindwa pa kuanzia kujiajiri, je wale ambao ni fresh from school ambao hawakubahatika kupata utaalamu kama wa kwako itakuwaje??? Nilitegemea kwa utaalamu wako utawaalika wana JF ambao hawajui mbinu za kujiajiri waje wapate ushauri kwako kile wanachopaswa kufanya kukabiliana na tatizo kubwa la ajira lililopo nchini kwa sasa.
   
 3. Zanta

  Zanta JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 2,017
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kweli wabongo tunasoma ili tupate cheti. Yaani umesomea ujasiariamali then unakuja hapa kuuliza mtaji utapata wapi?
   
 4. Damson88

  Damson88 JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu hili ni jambo la kufikirika kidogo kwa upande wangu, au kama vipi jiweke upande wangu na unipe mawazo yako juu ya hili.
   
 5. Damson88

  Damson88 JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hivi umeelewa nilichoandika kweli? Wewe ulichoona tu hapa ni kwamba natafta mtaji... Nasikia mshua/mjomba anauwezo. Kama unajipya changia. Kumbuka mtu anaomba ushauri pale ambapo hayakubali majibu ya maswali aliyonayo kichwani. Nahis umenielewa.
   
 6. Voice of Wisdom

  Voice of Wisdom JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 541
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  mi naona point yako ya msingi hapa ingekuwa ni namna gani unaweza kupata mtaji. Kuhusu ujiajiri vp wakati umejinadi umesoma ujasiriamali huo ni uchuro,na inaelekea utakuwa na vyeti wala si elimu, but no wonders kwani ni drs na prof wangapi wapo wanafundisha ujasiriamali vyuoni na hawana hata mradi wa genge. Hyo ndiye elimu yetu tanzania inatujenga kufaulu mitihani, ila haitusaidia tukishafaulu tusipoajiriwa tunafanyaje, btw sikulaumu wewe ni mfumo labda umekuathiri.
   
 7. b

  bagain JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60
  hichi alichokileta mwenye uzi ndiyo taswira halisi ya elimu inayotolewa na vyuo vyetu.

  Vyuo vyetu ni wanajisifu sana kwa maneno lakini uhalisia ndio huu ya kuwa elimu inayotolewa siyo inayohitajika.

  Mfano: kuna vijana wengi sana wanaingiza nyimbo kwenye simu na kuburn cd kkoo na maeneo mengine lakini wengi hawajasomea hata computer, waliosomea wanatembea na bahasha kutafuta kazi. Hapo mtaji ni computer moja tu ya laki tatu na nusu.

  Ukifuatilia vyuo vya short cources navyo ubabaishaji mwingi, mtu anamaliza course lakini hawezi kufanya hata vitu basic.

  vyuo vibadirike, wasibaki kuongea maneno matupu.
   
 8. Damson88

  Damson88 JF-Expert Member

  #8
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu nashukhuru sana kwa changamoto ulizozigundua na kuzidadavua hapa. Kifupi inabidi sisi watanzania tutambue kuwa kuajiajiri sio kwa mjasiriamali pekee bali ata yule aliyesoma rasilimali watu anaweza kuanzisha kampuni kama consultancy au kitu kama hicho. Sasa hapa naona umejaribu kuelezea tatizo kwa kina na siyo suruhisho la tatizo hili. Ni mtazamo tu.
   
 9. Damson88

  Damson88 JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Unachokiongea ni kweli mkuu nashukhuru kwa kulitambua hili
   
 10. T

  Tewe JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Kupanga ni kuchagua, hapo ulipo ni matunda ya chaguo lako miaka 3/4 iliyopita sasa ndio unatambua kwamba chaguo halikuwa sahihi.
  Poleni mnaosheheleke tu allocation za TCU simply umepata chuo. Kifuatacho unawatia wazazi ghalama halafu unakuja kuduwaa mitaani
   
 11. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #11
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mkuu ni kweli Kabisa na Ikitaka kujua kwamba Tanzania Hakuna Elimu bali watu huenda CHUO KIKUU ILI NDUGU, JAMAA, MARAFIKI, MAJIRANI NA KAZALIKA WAFURAHI ndo hilo,

  Mfano: Mtu unakuta ameaply Kozi tofauti zaidi ya 5 unashindwa kabisa kujua huyu maishani mwake ametageti kuwa nani?
  Utakuta mtu kafanya hivi:

  1. First Choice- Acounting

  2. Second- Human Resorces Managment

  3. Education

  5. IT

  na kazalika, so kwa staili hii ni lazima haya Yatokee, Na watanzania wengi huwa wanafurahi sana Kufika Chuo KIKUU BILA KUJALISHA KULE ANACHUKU UTALAMU GANI, YEYE NI ULIMURADI KAFIKA CHUO KIKUU, na kwa maisha ya sasa ni lazima tubadilike, Ni si kwa jamaa pekee bali iko kwa watu wengi leo hii kawaulize hao wanaoingi firs Year kwa nini walichagua Kozi hiyo na wana malengo gani nayo, Utasikia wanasema waliona kuliko kukaa nyumbani bali aende hata hiyo kozi,
   
 12. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #12
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Wakuu na Tatizo kubwa kuliko yote na ambalo nilisha wahi kulitolea maeleo kwenye jukwaa la Biashara ni hili hapa

  1. MFUMO WA UCHUMI WETU
  Ujamaa wetu, ilichangia sana kutufikisha hapa tulipo, na mfumo wa kijamaa mara zote unalemaza hadi akili na unafanya watu tuamini kila kitu ni serikali ndo inatakiwa kufanya, cheki nchi kama Kenya walio anza na mfumo wa Kibepari, wao hawana matatizo kama yetu, Vijana wana jijairi bila tatizo lolote

  2. WAZAZI WETU

  - Wazazi wanachangia asilimia kubwa sana kuharibu feature za watoto wao bila kujua lakini, Mdao hapo juu pamoja na kwamba amesomea UJASIRIMALI, lakini wazazi wake Tangia akiwa mdogo walikuwa wana mwambia asome aje kuwa Meneja, Mkrugenzi, Rubani wa Ndege na kazalika, Hii ikakaa kichwani mwake na alisoma kwa bidii ili aje kuwa Mkurugenzi au Menbeja
  HAKUNA MZAZI HATA MMOJA ANAYE MHIMIZA MTOTO WAKE ASOME AJE KUWA MFANYA BIASHARA MKUBWA KAMA MENGI,

  3. JAMII INAYO TUZUNGUKA/MARAFIKI/MAJIRANI
  Mkuu sucess is Genetic mkuu kama MAJIRANI, WAZAZI, MARAFIKI NA NDUGU wote ni Wafanyakazi uwezekano wa wewe kuja kuwa Mfanya biashara ni mdogo kwa sababau umekua ukiwaona wakienda kazini wakipiga tai zao, wakilietwa na magari ya Kampuni/serikali, hii inakuwa inakuvutia sana na wewe kutamani siku moja uje kuwa kama wao

  CHUKULIA MFANO WA WAHINDI: Hawa watu watoto wao wanakuwa wakiwaona Wazazi wao wanashinda madukani. Marafiki zao wazai wao ni wafanya biashara, Majirani zao wote ni wafanya biashara, HAPA AUTOMATICALY WATOTO NAO WATAKUJA KUWA WAFANYA BIASHARA WAZURI, ndo maa huwaoni wakitafuta kazi kama WABONGO,

  4. VYUO VYETU/SHULE ZETU
  Hapa napo elimu zetu na cyuo vyetu vimekaa ki theory zaidi, na hata walimu nao wanasisitizi watoto wasome waje kuwa Wakurugenzi, so ni lazima watoto waje kuwa wafanya biashara


  SO WAKUU DHANA YA UJASIRIMALI INATAKIWA IANZIE MBALI SANA NA SI VYUONI PEKEE
   
 13. Mr.mzumbe

  Mr.mzumbe JF-Expert Member

  #13
  Oct 2, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 800
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 60
  kweli elimu ya bongo kichekesho!yaani mpaka wewe uliyekuwa na shahada ya ujasiriamali bado unataka ushauri kutoka kwa mangubwaru kama sisi??
   
 14. Sunman

  Sunman Member

  #14
  Oct 2, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yote haya ni mfumo
   
 15. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #15
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  Ingia sehemu ambayo unahisi utaimudu, yenye ufahamu nayo, na unayoipenda
  Fikiria itakayokuja kichwani mwako ndio hiyo hiyo

  Pia uangalie na mtaji utakaokuja nao kwenye biashara
   
 16. K

  KOMWAA Member

  #16
  Oct 2, 2012
  Joined: Mar 26, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi ninachoona cha muhimu mhusika aangalie utaalamu alonao na anataka kufanya nini, kitu gani amekosa? manake mtaji nao inabidi ujue unataka kutumia wapi, mana kuna watu wana mitaji lakini hawajui wafanye biashara ya aina gani...FIKIRIA tena unapenda kufanya kitu gani alafu unahitaji kubustiwa wapi...
   
Loading...