Mhispania aweka rekodi ya kupanda mlima Kilimanjaro kwa kutumia baiskeli

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,251
spain.jpg

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

MPANDA milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli ,Juanito Oiarzabal ameweka rekodi ya kuwa Mhispania wa kwanza kupanda Mlima Kilimanjaro huku akitumia saa 31 akiendesha baiskeli katika siku tano hadi kufika kilele cha Uhuru.

Juanito na wenzake wawili , Eduardo Pascuaz na Ramon Abecia waliianza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli ,wakianza safari yao kupitia lango la Kilema ,aina hi ya utalii ikiwa ni bidhaa mpya katika Milima huo mrefu kuliko yote barani Afrika.

Aina hii mpya ya utalii ambayo kwa sasa imeanza kushika kasi katika Hifadhi za Taifa ,za Mlima Kilimanjaro,Arusha na Saadan inatokana na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kuendelea kupanua wigo wa vivutio katika Hifadhi zake 16,

Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete anaeleza hatua ya Juanito na wenzake kufika katika kilele cha Uhuru inaashiria kuanza kufunguka kwa aina hii mpya ya utalii katika Hifadhi za Taifa .
 
Baisikeli ili bebwa tu, then akafika kule akapigia picha, usifikiri alifika kule akiendesha, ukitaka kuamini, basi jaribu kutembelea huu mlima then njoo hapo utupe taarifa hiyo baiskeli iliendeshwaje hadi Uhuru Peak
 
Sasa namimi naenda kuvunja rekodi ya kupanda huo mlima scooter,

Kila siku wao tuu
 
"huku akitumia saa 31 akiendesha baiskeli katika siku tano hadi kufika kilele cha Uhuru" saa 31 = siku 5 naomba ufafanuzi hapo au alikuwa anaendesha na kupumzika?
 
"huku akitumia saa 31 akiendesha baiskeli katika siku tano hadi kufika kilele cha Uhuru" saa 31 = siku 5 naomba ufafanuzi hapo au alikuwa anaendesha na kupumzika?
Nafikiri alitumia wastani wa masaa 6 kwa siku! Hivyo alikuwa akipumzika ndiyo kama taarifa hiyo ni sahihi.
 
Sijaelewa hapo siku tano Haina Masaa 31


"huku akitumia saa 31 akiendesha baiskeli katika siku tano hadi kufika kilele cha Uhuru" saa 31 = siku 5 naomba ufafanuzi hapo au alikuwa anaendesha na kupumzika?



inamaana huyo mzungu roboti aendeshe siku 5 nzima bila kupuumzika
hayo masaa 31 ni running time akiwa juu ya baiskeri hayo masaa mengine katika siku tano anapumzika
 
Iv kwanini kila mtu akifika kilimanjaro huwa anaweka historia
kwa sababu sio kila mtu anaweza kufika kileleni. ofisini kwetu huwa tuna program ya kupanda mlima Kilimanjaro watu wakirudi hizo sura wamebabuka wako hoi....

Next year nina plan ya kushiriki hopefully na mimi nitafika KILELENI.
 
Back
Top Bottom