Mhiringitu

Ngonalugali

JF-Expert Member
Jan 12, 2008
659
100
Kulikuwa na jamaa mmoja wa kibantu aliyepata ajira kwa wawindaji wa kizungu. Hao wazungu walikuwa watatu na mara nyingi walikuwa wakienda pamoja kuwinda huku mmbongo akiwa amewabebea vifaa vyao vya uwindaji.
Siku moja mmoja wa wawindaji aliyejulikana kama Mhiringitu alimchukua kibarua wao na kwenda naye kutafuta chochote porini. Baada ya muda walivamiwa na nyati na yule nyati akafanikiwa kumrarua mzungu na kumuua. Yule mmbongo alifanikiwa kupanda juu ya mti na kuwa salama.

Wale jamaa wengine walikaa kambini na baada ya muda walipata hofu kuona jamaa yao na kibarua hawajarudi ndipo walipoanza kuwafuatilia huku wakiita.
Wazungu: Mhiringituu, where are you?
Porini: Kimya
Wazungu: Mhiringituu, where are you?
kimya. Wakapiga miruzi na makofi kuita, lakini hawakufanikiwa kupata majibu kutoka upande wowote.

Baada ya muda yule kibarua alizisikia sauti zao na akaanza kupiga kelele za kuomba msaada. Walipomsikia yule kibarua walielekea alipokuwa na maongezi yao yakawa hivi:-

Wazungu: Where is Mhiringitu
Kibarua: mhiringitu iz ku-dediz
Wazungu: What???!!!!
Kibarua: Mhiringitu iz kudediz iz nyatiz kumnyating!
 
tafadhari ndugu,uwe unaweka habari ambazo zina kichwa na miguu,kabla ya kifo cha huyo mzungu kutokea,huyo kibarua alikuwa anawasiliana vipi na hao wazungu?mie ungekaa tena mezani
 
tafadhari ndugu,uwe unaweka habari ambazo zina kichwa na miguu,kabla ya kifo cha huyo mzungu kutokea,huyo kibarua alikuwa anawasiliana vipi na hao wazungu?mie ungekaa tena mezani
Usilolijua ni sawa na usiku wa giza.

Jamvi limetandikwa na kuna maelezo ya Jokes/Udaku.
Ama na hapo unahitaji mkalimani.

Kaa kwenye screen yako uelewe vizuri.
 
hata mie naona jamaa hapo kachemsha,maana udaku gani ambao matukio yake yanajikanganya namna hiyo
 
wacha na mie nitoe moja

kuna jamaa alikuwa akikaa na wAzee wake na mtaani kwao kulikuwa kuna vijana wakora.

sasa wazee wake kwa hofu ya kumpoteza kijana na wao na kuingia kwenye vitendo vya kihuni wakamshauri aowe.

jamaa alipoowa sasa usiku mkewe akaanza kumshika shika kwa ajili ya kufanya nae mapenzi, jamaa akaruka na kumwambia nimeamua makusudi ili niache kufanya vitendo vya kihuni sasa unanifanya nnn?

mkewe alibaki na mshangao!!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom