Mhindi katili na jela binafsi kuwafungia wateja wanawake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhindi katili na jela binafsi kuwafungia wateja wanawake

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Candid Scope, May 27, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]

  RAIA WA INDIA ADAIWA KUNYANYASA WANAWAKE IRINGA ANAMILIKI MAHABUSU BINAFSI ,POLISI WAMSAKA

  JESHI la polisi mkoani Iringa linamsaka mkurugenzi wa taasisi ya mikopo ya Brac ambaye ni Raia wa India kwa tuhuma za kumnyanyasa kwa kumfungia katika mahabusu binafsi ofisini kwake mwanamke mmoja Edina Panzi (47) mkazi wa Ilala katika Manispaa ya Iringa akimdai kiasi cha shilingi 5800 .

  Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Peter Kakamba alisema kuwa raia huyo wa India anasakwa na jeshi la polisi mkoani Iringa baada ya kumfungia katika mahabusu mwanamke huyo ambaye alikopeshwa fedha na taasisi yake hiyo ya Brac tawi la Ilala mjini Iringa.

  Bila kumtaja jina raia huyo wa India ,kamanda Kakamba alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 11 jioni katika eneo la Ilala ambako zipo ofisi za taasisi hiyo ya Brac baada ya jeshi la polisi kupata taarifa kutoka kwa rai wema kuhusiana na mwanamke huyo kufungia katika mahabusu katika ofisi hiyo kabla ya polisi kufika kumfungulia mlango mwanamke huyo.

  "Jeshi la polisi lilipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuhusuana na mwanamke huyo kufungia katika mahabusu hiyo kwa sababu ambavyo raia huyo wa India anazijua yeye na ndipo polisi walipofika na kufanikiwa kufungua mahabusu hiyo na kumtoa mwamamke huyo "

  Kakamba alisema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikijishughulisha na utoaji wa mikopo kwa wanawake jambo ambalo si baya ila ubaya unakuja pale ambapo mkopeshaji huyo anajichukulia sheria mkononi kwa kutoa adhabu iliyo kinyume na sheria za nchi hii kwa kuwafungia mahabusu wakopaji wake.

  Kwani alisema kuwa haipo sheria inayomruhusu mtu awaye yeyote yule ama taasisi ya ulinzi kumiliki mahabusu kwa kukamata watu na kuwafungia mahabusu kwani kufanya hivyo ni kosa na wanapatikana na tuhuma kama hizo wakikamatwa hufikishwa mahakamani.

  Hivyo alisema kuwa jeshi la polisi linaendesha msako mkali wa kumsaka mkurugenzi huyo wa Brac ambaye ni rai wa India ili kufikishwa mahakamani .

  Kwa upande wake mwanamke huyo anayedaiwa kufungiwa mahabusu alisema kuwa alifungiwa katika mahabusu hiyo juzi kuanzia majira ya saa 4 asubuhi hadi saa 11 jioni kabla ya waandishi wa habari wa mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) kuweza kufika eneo hilo na kutoa taarifa hiyo polisi .

  Mwanamke huyo alisema kuwa jumla ya deni lote alilokopa lilikuwa ni kiasi cha shilingi 500,000 na hadi anakamatwa na kufungiwa katika mahabusu hiyo alikuwa akidaiwa kiasi cha shilingi 5800 pekee .

  Diwani wa kata hiyo ya Ilala ambaye pia ni naibu meya wa Manispaa ya Iringa Grevas Ndaki alisema kuwa uongozi wa kata hiyo hauungi mkono hata kidogo unyanyasaji unaofanywa na Raia huyo wa India kwa wanawake wa kata hiyo na kuwa kutokana na tabia hiyo kuendelea kuchukua kasi wanaona ni vema ofisi hiyo kuondolewa katika kata hiyo .

  Source: Blog ya
  Francis Godwin
   
 3. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Hii habari inatakiwa ichunguzwe vizuri: kwenye ofisi za taasis ya mikopo inayoitwa PRIDE(buguruni), wateja wakiingia hawaruhusiwi kutoka mpaka wamelipa deni la siku hiyo, iweje BRAC iwe ni habarai ya kuita polisi na TGNP?
   
 4. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  lakini Dawa ya DENI KULIPA.
   
 5. m

  mabhuimerafulu Member

  #5
  Jun 1, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 89
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu mpende msipende, hawa wakopeshaji sijui BRAC, PRIDE, FINCA nk vimekuwa kama vituo vya kudhalilisha wanawake. Utawakuta mama zetu wanavyonyanyasika kwa kila hali ikiwemo kuombwa ngono na watoa mikopo. Yote hiyo ni kutokana na umaskini. Umaskini kitu kibaya sana.
  Si Mhindi wa BRAC tu mwenye rumande binafsi, barabara ya Nyerere kuna Mhindi ana magodown mengi lakini wanawake wanaoingia humo kufanya kibarua cha kupembua choroko, kunde, mpunga nk, wanafungiwa kama mahabusu. Mambo ya ajabu kwelikweli kwenye nchi huru. Tembelea viwanda vya eneo la Chang'ombe jijini Dar, hutaamini kama hayo utakayoyaona yanatokea Tanzania. Wananyanyasika kwelikweli
   
 6. m

  mabhuimerafulu Member

  #6
  Jun 1, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 89
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wee wa ajabu kweli. Kwako ungeruhusu mkeo ama mumeo aswekwe rumande na Mhindi? Lazima utakuwa unafanya kazi kwa Wahindi na unawasaliti Waswahili wenzio kwa sana tu. Ungekuwa karibu nami ningekudelete sasa hivi kutoka uso wa dunia!
   
Loading...