"Mhindi huyu anawamaliza wanetu" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Mhindi huyu anawamaliza wanetu"

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee wa Gumzo, Jul 16, 2008.

 1. Mzee wa Gumzo

  Mzee wa Gumzo Senior Member

  #1
  Jul 16, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni kweli na wala haina chenga.
  Nilikuwa moshi jana tu na kuthibitisha.Kuna grocery moja maarufu maeneo ya shanty town karibu na hospitali ya KCMC ijulikanayo kama 'UP TOWN GROCERY'.

  Ilianza kama tetesi kuwa grocery hiyo ni kituo cha madawa ya kulevya.Kisha nikamtafuta mwenyeji wa pale na mtu mzima na mnywaji wa hapo nikamuuliza akaniambia ni kweli tena akanitajia hadi wateja wakubwa wa madawa hayo kuwa ni wanafunzi wa INTERNATIONAL SCHOOL MOSHI,moja ya shule bora kabisa za kimataifa.

  Nikamvizia mwanafunzi mmoja wa shule hiyo na kumbana kona nikijifanya teja nataka unga nibwie.Kiulaini akanielekeza kuwa yeye siyo muuzaji bali mtumiaji ila kama nataka kununua niende kwenye ile grocery kwa wahindi nitapata mara moja.

  Hii siyo hadithi ni kweli.Nimeitoa kwenye jukwaa kusudi tuungane kummaliza huyu jamaa na wengine wote wanaofanana nae.
  Nilikuwa moshi kwa muda mfupi tu na sikupata nafasi ya kushughulikia hili na ningali safarini kikazi.
  Naombeni namba ya Lucas Ngoboko (kamanda kilimanjaro) au IGP Mwema.
   
 2. C

  Chuma JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  MKUU ahsante naona wakuu watafutilia...ila ukipata wasaa toa taarifa ya hapo shuleni pia...maana wengine tumewapeleka vijana wetu huko wasome kumbe kuna upuuzi unaendelea. hapo wa kukamatwa ni wote wabwiaji na wauzaji....
   
 3. Mzee wa Gumzo

  Mzee wa Gumzo Senior Member

  #3
  Jul 16, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninataraji kurudi huko soon na kufanya jambo.in the mean time lazima watu wa hapo wachukue hatua
   
 4. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Tunakushukuru sana mzee wa gumzo ... sote tutajaribu kuwa kama wewe nadhani kwa kufanya hivyo tunawanusuru watoto wetu na taifa kwa jumla .. JF members who are in Moshi please give us a hand ila msimshutue mhindi
   
 5. I

  Ipole JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2008
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 296
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni habari mbaya kwa kizazi kjacho cha msingi ni kumripoti polisi maana kulalamika kwenye kwenye mtandao hakutatusaidia
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Dah hii kweli sad news watoto wa taifa la kesho tutawapoteza hivihivi.
  Lakini usikute maafande wote wanajua hapo kuwa huyo muhindi anauza mzigo.Lakini hapo usikute wao wanachukua mshiko kisha wanapita kama hawajui hivi polisi ndo zao kila kukicha tunawapigia kelele.Sasa inabidi kuwachongea kwa IGP tu.
  Hivi ile list ya madawa ya kulevya kwa nini Rais ameikalia tu au naye iwa anaingiza mzigo nini hatuoni hatua zinazo shughulikiwa zaidi ya Rais wa chama cha ngumi naye atatoka tuu hivi kalibuni Munitanga.
  Haya jama hii ndo Danganyika.
   
 7. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  Wauza unga wamesharipotiwa polisi sana.
  Kutoa ripoti kwenye mtandao kama alivyofanya mzee wa gumzo naona ndio njia muafaka kwa sasa.
  .
   
 8. kkiwango

  kkiwango Senior Member

  #8
  Jul 16, 2008
  Joined: Aug 27, 2007
  Messages: 168
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ndugu ungefanya hima kuripoti kabla hata ya kuja hapa kwenye mtandao, maana unakuwa umempa Muhindi muda muafaka wa kujiandaa, mtandao unasomwa na wengi, usisubiri mpaka urudi tena huko, piga simu kwa kamanda wa polisi mkoa mambo yaendelee. Mwenye number ya simu tafadhali, au unaweza omba msaada wa number ya simu kwenye kituo chochote cha polisi. Hili ni taifa la kesho jamani, tusizembee
   
 9. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Very true! madai yao anauza pizza
   
 10. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwanza hongera kwa hilo maana hii grocery naipata poa maana kipindi fulani nilikuwa nakaa karibu na Glacier Club hivyo nikasikia hizi habari ila nikaignore sasa zimefika humu nadhani zimekuwa issue.Huyu jamaa asivumuliwe taarifa zifikishwe kwa wahusika.
   
 11. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135  Hicho ndicho cha kwanza kunijia akilini. Ila pengine juhudi za kuwafikisha hawa watuhumiwa kwenye vyombo vya sheria ziko nje ya uwezo wetu kwa mazingira yalivyo leo Tanzania. Tunachoweza kufanya ni kuhakikisha unga hauuzwi kwa kuripoti mahali kama hapa.

  .
   
 12. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2008
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Awekewe mtego halafu watu waucounter via PCCB ili kusiwe na mpenyo wa rushwa na nadhani huyu jamaa hafanyi hii kitu peke yake lazima aleleze madealer wake wakubwa pamoja na hao distributors. Ukicheki kiini chake utakuta kuna kiongozi tu wa serikali anahusika. Siko negative na viongozi wetu lakini huyu jamaa lazima atakuwa na shelter yake inayomkinga na mvua nayo inabidi watu wachunguze wajue kimya kimya. Na Kama atakuwa anaperuzi JF pia ajue kuwa upuuzi anaoufanya haukubaliki kabisa katika jamii. Nami ninalaani kwa nguvu zote kama wachangiaji wengine waliopita.
   
 13. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,231
  Likes Received: 5,619
  Trophy Points: 280
  guseni muone hayuko pekeyake i assure u itabaki story yuko10yrs ago hatari
   
 14. M

  Mbeba Maono Senior Member

  #14
  Jul 17, 2008
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 108
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Magabacholi ndo zao. ufisadi kila eneo. hakuna hata biashara moja ambayo magabacholi huwa si ya kifisadi. kuanzia kwenye viwanda, hadi kwenye grocery. huwezi amini, viwanda vingi hapa tz, tunajua ni vya wahindi, kumbe vya viongozi wetu wanaiba hela zetu halafu wanawapa wao kama kivuli. pia hata madawa haya ya kulevya, watu wakubwa wa selikalini(ila so wote) wanaingiza halafu wanawatumia wao pamoja na wazalendo wachache kuyauza. ndo zao hao. hao viongozi wetu ambao wana immunity fulani ya kutokaguliwa viwanja vya ndege ndo wanaingiza sana, pamoja na wazalendo wachache wanaojitoa muhanga kuyameza tumboni.

  kuna siku tutavuta pua za magabacholi hawa hadi zitakuwa ndefu zaidi ya hapo, na huo wembamba wao, watatembea ya mguu hadi india, hawataogopa kuliwa na samaki humo baharini. ni mafisadi wakubwa sana. kama hamuamini, jaribuni kuchunguza kupitia wafanyakazi wao, watawaambia.
   
 15. Single D

  Single D JF-Expert Member

  #15
  Jul 17, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 459
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Igp Mwema= +255 754-785557
   
 16. Nzokanhyilu

  Nzokanhyilu JF-Expert Member

  #16
  Jul 17, 2008
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,087
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Kuna dogo fulani ndio anga zao, na yamewamaliza. Sad man.
  Ishu inajulikana longtime.
   
 17. Mzee wa Gumzo

  Mzee wa Gumzo Senior Member

  #17
  Jul 18, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thaks kwa wazo zuri.Nimeshapeleka suala hili kwa wahusika.Tusubiri matokeo.Kuna makachero wa JF wanafuatilia kwa karibu.
   
 18. C

  Chiluba Member

  #18
  Jul 18, 2008
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Aripoti wapi ndugu yangu..kama mkuu wa nchi alishakiri majina ya wahusika wakuu anayo lakini hadi leo hakuna kilichofanyika..itakuwa polisi wa Moshi!
   
 19. K

  Kungurumweupe JF-Expert Member

  #19
  Jul 18, 2008
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 317
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0

  Tunashukuru. Lakini huyu muungwana wetu inabidi tumlaumu sana kwani alipewa orodha ya wahusika wa unga lakini hajawashughulikia. Ndo maana wanaendelea na biashara yao kwa vile wanajua serikali yetu iko likizo.
   
 20. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #20
  Jul 18, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 135
  Hivi kuna anayejidanganya kwamba hii ni breaking news kwa polisi? Iweje wewe mpita njia tu tena uliyeko safarini ugundue kitu kama hiki wakati kuna mijitu inaishi hapo na inalipwa mishahara ili ijue mambo kama haya na isijue siku zote?
   
Loading...