Mhimili wa nne wa DOLA vipi? Mbona hamtimizi wajibu wenu?

Kitumbo

JF-Expert Member
Jun 16, 2010
549
185
Vyombo vya habari siku zote vimejinasubu kuwa ni mhimili wa nne wa Dola na kwamba una jukumu la kufichua maovu ili kusudi jamii wakati wote iujue ukweli na kufanya maamzi kwa haki.


Lakini kinachoendelea katika kipindi hiki cha kutangaza nia inadhihirika wazi kwamba vyombo vya habari vimefumbwa macho kuona maovu na vumefungwa midomo kuyasema waziwazi badala yake navyo sasa vimebaki kuwa vya kusifu tu.


Kuna mengi yanatokea katika mikutano ya watangaza nia sasaivi na vyombo vya habari vinayashuhudia lakini hayasemwi. Kuna ishara zote kuwa bahasha za kaki zimetembea na mhimili wa nne ukaamua kukaa kimya na kuacha wajibu wake.


Watangaza nia wa CCM wapo katika kutafuta wadhamini. Wengine wanatumia kipindi hicho kufanya kampeni zisizo halali. Kama mngekuwa huru naamini tayari Mangula angeshahojiwa na kusema neno na wananchi wangetaarifiwa kuwajua wagombea wanaowalaghai. Bahati mbaya mmefungwa midomo!!!!!


Bodaboda wanaandamana katika mikutano ya watangaza nia kudai fedha walizoahidiwa ili kushiriki maandamano ya watangaza nia ili wapate publicity, mhimili upo kimya, umezibwa mdomo


Watangaza nia wanakodi blue guard kuwapiga watangaza nia wenzao wanaotafuta saini jirani na mikutano yao, vyombo vya habari mpo kimya tu!


Mhimili wa nne wa DOLA vipi? Mbona hamtimizi wajibu wenu?
 
Back
Top Bottom