Mhimil mmoja wa serikali unaingilia kazi za mihimili mingine

Gagnija

Platinum Member
Apr 28, 2006
11,819
10,353
Kinadharia, jamhuri yetu inasimamiwa na mihimili mitatu. Mihimili hiyo ni Bunge ambalo kazi yake ni kutunga sheria, serikali ambayo kazi yake ni kusimamia na kutekeleza sheria zinazotungwa na bunge, na mhimili wa tatu ni mahakama ambayo kazi yake ni kutafsiri sheria hizo.

Majuzi tumeshuhudia utiaji saini wa mbwembwe uliofanywa na rais kwenye muswada ambao hata hivyo, baada ya kujadiliwa bungeni, iligundulika kuwa kuna wahuni waliochomeka baadhi ya vifungu ambavyo havikuwemo kwenye muswada uliopitishwa na bunge.

Kama hiyo haitoshi, Werema (AG), wakati wa mjadala wa muswada wa uharamia baharini, alisema mahabusu wanaosubiri utekelezwaji wa hukumu ya kifo kazi wanayofanya huko gerezani ni kula na kupewa matibabu wanapokuwa wanaumwa.

Swali:1 Kazi ya bunge ni kutunga sheria, lakini sheria iliyotungwa na bunge haitakuwa sheria hadi rais akubali. Hapo rais haingilii kazi za bunge?

2. Kazi ya mahakama ni kutafsiri sheria. Jaji anatoa hukumu stahiki ya kifo kwa mshitakiwa, lakini hukumu hiyo haiwezi kutekelezwa kwa kuwa tu rais ambaye hata kisheria (Kitaaluma)siyo learned hataki itekelezwe na kusababisha msongamano usio wa lazima magerezani. Huko si kuingilia kazi za mahakama? Nawasilisha kwa wataalamu wa sheria!
 
Back
Top Bottom