Mhezi: Mabilioni ya JK hayukazaa matunda; Serikali ilitanguliza fedha badala ya elimu ya ushirika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhezi: Mabilioni ya JK hayukazaa matunda; Serikali ilitanguliza fedha badala ya elimu ya ushirika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 17, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  *Serikali ilitanguliza fedha badala ya elimu ya ushirika

  Na Arodia Peter, Dar es Salaam

  MWANZONI mwa miaka ya 1960 na 1970, mikoa ya Kagera na Kilimanjaro ilikuwa mstari wa mbele katika masuala ya ushirika.

  Uimara wa ushirika wa mikoa hiyo unatajwa kuwa kichocheo cha kuwa na wasomi wengi kuliko mikoa mingine hapa nchini.

  Hata hivyo, hali ni tofauti katika miaka ya hivi karibuni, sababu kubwa ikitajwa kuwa ni kutokana na kudorola kwa ushirika nchini.

  Ushirika ninaozungumzia hapa ni ule wa njia ya vikundi (Saccos) badala ya ile ya mazao ya miaka ya nyuma.

  Hakuna elimu ya maana inayotolewa ili kuhamasisha wananchi kujiunga na ushirika wa kujiwekea akiba kwa njia ya vikundi (Saccos) ili kujikwamua kiuchumi.

  Ulipoanza mchakatao wa kuanzisha jumuia ya nchi za Afrika Mashariki kwa mara ya pili, tofauti na ule wa awali uliovunjika mwaka 1977 Watanzania tulipiga kelele sana kwa hofu ya ‘kumezwa’ na nchi za Kenya na Uganda.

  Kisingizio cha kukataa jumuia hiyo ni elimu, kwamba nchi za Kenya na Uganda zinatuzidi sana kielimu.

  Lakini kimsingi sioni kama elimu ni kikwazo kikubwa kwa Watanzania ikizingatiwa ukweli kwamba tunazizidi nchi hizo kwa kila hali, ikiwamo jambo muhimu la rasilimali, amani, utulivu pamoja na mshikamano wa kitaifa.

  Hofu waliyonayo Watanzania inatokana na jambo moja kubwa, hatutaki kufikiri vitu vipya, tunaogopa kuthubutu na hatujiamini!

  Tofauti na wenzetu, wao wanafikiri vitu vipya, na hawaogopi kuthubutu, hawaogopi kuthubutu na wanajiamini. Hizi ndizo tofauti zetu. Tunahitaji kuthubutu

  Mathalani, Tanzania ndiyo nchi ya kwanza katika jumuia hiyo kuwa na Chuo Kikuu cha Ushirika chenye hadhi kubwa miongoni mwa nchi hizo, lakini tazama utendaji na ufanisi wa vyama vyetu vya ushirika nchi nzima.

  Kwa mfano, Saccos zinazoundwa kwa ajili ya wananchi kujikwamua kiuchumi kila kukicha zina changia kiasi gani katika kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja.

  Habibu Mhezi, ni Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo Tanzania (SCCULT) anasema, kama Serikali haitaweka mpango maalumu kwa ajili ya elimu Tanzania itakuwa na safari ndefu kufikia mafanikio katika SACCOS zilizopo nchini.

  Anasema, kutokana na Watanzania kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu masuala ya kujiwekea akiba kwa njia ya vikundi (Saccos) wanajikuta wakijiingiza katika mikopo ambayo inawafilisi hata kile kidogo walichonacho.

  Anabainisha kuwa, elimu inayohitajika kwa Watanzania ni pamoja na taratibu za kuanzisha Saccos, umuhimu wa kujiwekea akiba, na namna ya kuchanganua na kubaini mbinu za baadhi ya taasisi za fedha ambazo zinawarubuni kuingia mikopo yenye riba kubwa.

  Akigusia fedha zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania miaka michache iliyopita maarufu kama mabilioni ya Jk, anasema fedha hizo hazikuzaa matunda mazuri kwa sababu Serikali ilitanguliza fedha badala ya elimu ya ushirika.

  “Watanzania waliposikia kuna mabilioni ya JK walikimbilia kuanzisha na kujiunga kwenye Saccos, lakini walipozikosa basi Saccos hizo zimekufa, na wao wamebaki nyuma kiuchumi, sasa marejesho uliotegemewa umefikiwa?” anahoji.

  Anatolea mfano nchini Kenya, kwamba asilimia 15 hadi 16 ya wananchi wake wamepata elimu ya ushirika, maana yake ni kwamba kati ya watu mia moja wa Kenya 16 wamepata elimu hiyo.
  Wakati nchini Uganda wenye elimu ya ushirika ni asilimia nane hadi tisa, Tanzania elimu hiyo imewafikia watu watano tu kati ya 100.

  Aidha, Mhezi anakwenda mbali zaidi na kusema kuwa elimu ya ushirika inahitajika kwa Watanzania wote bila kujali cheo wala nafasi ya mtu, kwa sababu hata wabunge wengi wamekuwa wakihamasisha wapiga kura wao kuanzisha saccos bila wao wenyewe kujua hata taratibu za uanzishwaji wake.

  “Ndiyo maana tunahitaji nguvu ya Serikali, tatizo la ukosefu wa elimu liko kila sekta, wabunge na wanasiasa wanahamasisha wananchi kuanzisha Saccos bila kuwapa kwanza elimu ya kuanzisha Saccos zenyewe,” anasema

  Mhezi anazionya Saccos nchini kuwa makini na baadhi ya benki zinazowarubuni kukopa kwao lakini zina masharti magumu na riba kubwa.

  Kwamba, baadhi ya Saccos ziko taabani kifedha na nyingine zimeshindwa kuimarika kiuchumi kutokana na mikopo mikubwa waliyongia na benki bila kufanya utafiti wa kutosha.

  Kuhusu uhusiano wa SCCULT na taasisi za kibenki, Mhezi anabainisha kuwa, awali hawakuwa na uhusiano mzuri katika kile kinachoaminika kutoaminiana, kati ya taasisi hizo.
  “Awali uhusiano haukuwa mzuri, tulikuwa na hali ya kuogopana, hatupaswi kufika hapo, tuwe wamoja, tujenge mtandao mmoja ili kwa manufaa ya wote.” Anasema
  0755 556 270
   
Loading...