Mheshmiwa Majaliwa ziarani Kigoma tutarajie lolote au kama mtangulizi wake tu

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,908
2,889
tulizoezwa na ziara za watu tuliowakabidhi madaraka ya kutuongoza wakifanya ziara za kuja na kuondoka mkoani kwetu huku wakituacha vilevile na kero zetu tunakuomba mzee plz usiende kuuza sura huko ondoa kero za wananchi wako kuondoa kero sio mpaka kinana atishie kukung'oa au mnyika atangaze maandamano ya bila kikomo nakuomba mzee tumekupa hilo shangingi ili iwe rahisi kutufikia sio la kujidaia kwa washkaji zako litendee haki plz usiwaamini sana watendaji wako pindi wakikupa ripoti inayotuhusu njoo upate uhakika kwetu wakikwambia wananchi wanakula milo 3 kwa siku usiishie kuwaamini uje utizame sura zetu ujiridhishe
 
Mh.waziri mkuu karibu sana Kigoma lakini serikali zilizopita zimetusahau sana, tuna kero kibao, Angalia barabara ya kigoma to Kasulu haipitiki ni mbovu sijapata kuona, Angalia barabara ya kibondo Kasulu haipitiki, pori la Maragalasi limevamiwa wafugaji wanaharibu Mazingira.Waziri kilio chetu ni barabara, Umeme, na Maji tunaomba mtukumbuke.
 
karibu sana Kigoma mheshimiwa Majaliwa ila kuna jirani yako anaitwa Paulo Kagame mchokozi anatuharibia biashara na ujirani mwema na Burundi,Drc ati watu pekee wanaotakiwa kuishi ni watu wa jamii yake halafu eti hapendi tufanye biashara sie hatujui
 
JK bana???? et kigoma itakuwa dubai halafu kala kona teh teh teh!!!!
 
Mhe. Majaliwa piga kambi KUWASA. Mji wa Kigoma unapakana na ziwa Tanzanyika ambalo ni la pili kwa kina duniani. Ajabu wakaazi wa mji huu wanataabika na maji wakati ziwa lipo mita 10 tu! Waliaminishwa kuwa tatizo la maji lingeisha mwaka huu 2015 baada ya kulazwa mabomba mapya karibu mji mzima na kupata chanzo kingine cha kuvuta maji toka ziwani. Wananchi hawaambiwi mradi umepata nuksi gani ya kutokamilika? Ni ajabu sana kwa miji kama ya Singida na Dodoma kupata maji ya uhakika yenye "pressure" kubwa wakati mji wa Kigoma unakosa maji ya uhakika wakati kuna ziwa Tanganyika jirani tu! Uwekezaji na huo mji wa Dubhai ndogo utafanikiwa vipi katika mji huu wakati hamna maji ya uhakika?
Kama kuna jipu likamuliwe bila ganzi!
 
Back
Top Bottom