Mheshimiwa Zitto Kabwe aache siasa za kuchanganya wapiga kura. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mheshimiwa Zitto Kabwe aache siasa za kuchanganya wapiga kura.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Richard, Oct 6, 2012.

 1. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Hivi karibuni kumekuwa na taarifa na habari mbalimbali zinazomhusu mwanasiasa mbunge Zitto Zuberi Kabwe.

  Moja ya taarifa hizo ilikuwa ni uamuzi wake wa kutangaza dhamira ya kugombea uraisi kwa kupitia chama chake cha CHADEMA kwenye uchaguzi wa uraisi mwaka 2015.

  Kufikia azma yake hiyo Mheshimiwa Kabwe ambae ni naibu katibu mkuu , kwa uratatibu wa chama inabidi ashindane na katibu mkuu wake mheshimiwa Freeman Mbowe.

  Lakini baadae mheshimiwa Kabwe akaja na kutangaza uamuzi wa kujitoa katika kinyang'anyiro cha kugombea nafasi hiyo ndani ya chama chake. Pia akaeleza kwa baadhi ya vyombo vya habari kwamba uamuzi wake huo umetoka moyoni na kwamba ni uamuzi wa kulinda heshima ya chama chake kutoka kwenye wingu la mpasuko ambalo lingekikumba chama cha CHADEMA.

  Sasa kitendo hiki cha mheshimiwa Kabwe kuonyesha au kutangaza nia yake ya kutaka kugombea nafasi ya kuchaguliwa na chama chake kuwa mgombea uraisi bila kushauriana na wanachama waandamizi wa CHADEMA ambao wangetoa ushauri wao juu ya azma hiyo ya mheshimiwa Kabwe , kinaonyesha ubinafsi alio nao mheshimiwa Kabwe.

  Mheshimiwa Zitto Kabwe ana umri wa miaka 35 kwa sasa na ifikapo mwaka 2015 atakuwa na umri wa miaka 38 kama sikosei.

  Huu ni umri mdogo sana kwa siasa za Tanzania achilia mbali siasa za nchi za Magharibi na Marekani. Ni vema mheshimiwa Kabwe ametoa uamuzi wa busara kuhusu hili.

  Mimi ntaongelea baadhi ya viongozi watatu ambao wamechaguliwa kuwa maraisi au viongozi wa nchi tatu wakiwa na umri mdogo lakini ni kuanzia miaka 40.

  Viongozi wengi wa nchi hizo Uingereza ( David Cameron miaka 46) Russia (Dmitry Medvedev miaka 47 ) na USA (Barak Obama miaka 51 ) walichaguliwa kuwa viongozi wa nchi hizo wakiwa na umri mdogo ambao umeonyesha kukomaa kisiasa.

  Lakini kuna sababu zake, sababu kwamba Cameroon na wenzie niliowataja walionekana wataleta picha ya mabadiliko kwenye vyama vyao vya siasa kwa kuzingatia vyama hivyo vilikuwa na sura za wazee na mambo yaliyopitwa na wakati ambazo hazikuonyesha kutokea mabadiliko yoyote yale.


  Cameroon mwaka 2005 akashindana na mzee Davis Davis akiwa na umri wa miaka 39 na akashinda nafasi ya kuwa kiongozi wa Conservative na akakaa bungeni akishindana na Gordon Brown na baadae akazoeleka kwa wapiga kura kwamba msimamo wake na wa chama ni upi na kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 akashinda uchaguzi na kuwa Waziri Mkuu akiwa na umri wa miaka 44.

  Lakini Cameroon alikuwa na watu wanamsaidia katika kufikia azma ya kuwa kiongozi wa chama hicho kwahio ilikuwa kazi rahisi kupita kwenye uchaguzi ndani ya chama cha Conservative. Ilikuwa ni umri wake ambao ungewavuta wapiga kura vijana ambao kwa miaka mingi walikuwa wakiona siasa kwamba ni shughuli za wazee.

  Barak Obama nae mwaka 2008 aligombea na mama Clinton kuwa mgombe wa chama cha Democrat wa uraisi wa Marekani na wakati huo alikuwa ana umri wa miaka 47 na baadae akamshinda mgombea mzee John McCain kwenye uchaguzi wa uraisi.

  Obama kabla ya hapo alikuwa ni bunge au Senator wa Illionis na alikuwa na uzoefu wa siasa karibu miaka minane. Obama alishinda uchaguzi wa Marekani kwa kutumia silaha moja tu nayo ni mabadiliko na akakonga nyoyo za vijana wan chi hiyo na watu wa umri wake na hata wadogo wakawa wanamuelewa.

  Lakini kikubwa zaidi ni kitabu chake kiitwacho "Dream from My Father" ambacho kinaelezea maisha yake tokea alikotoka.


  Waziri mkuu wa sasa wa Russia Dmitry Medvedev alichaguliwa kuwa raisi wa nchi hiyo mwaka 2008 akiwa na umri wa miaka 43 na yeye tena alipitishwa na vyama vitatu tofauti kuwania uraisi na akapita bla taabu na kuwa raisi wa nchi hiyo.

  Lakini hizi siasa za mataifa haya ni siasa zilizojengwa kwa miaka na miaka na hazikuanza leo. Ni lazima mheshimiwa Kabwe atambue tofauti ya siasa hizi na siasa za nchi yetu.

  Tanzania kabla ya mwaka 1992 haikuwa na vyama vingi vya siasa na baada ya kutambulishwa kwa watanzania, sasa kila mtu anafahamu kuhusu siasa hizi na yupo tayari kuchagua sera za chama chochote zinazoonekana zinafaa kuleta maendeleo katika taifa letu.

  Mheshimiwa Zitto Kabwe atambue kuwa uraisi si tuzo wala cheo cha bure kinachogawiwa bila uangalifu. Ili mtu achaguliwe kugombea uraisi kuna sifa zake.

  Hayati mwalimu Nyerere aliwahi kutoa moja ya sifa kuu za mtu anaeutaka uraisi :


  Kwamba ataheshimu na kuilinda katiba- kwa maana kwamba mheshimiwa Zitto Kabwe ataheshimu katiba ya nchi na kufuata inavyosema hasa kuhusu kipengele cha umri wa wagombea ambapo umesimama kwenye miaka 40.

  Mheshimiwa Zitto Kabwe pia anaonyesha dhamira ya kutaka kuleta nyufa ndani ya chama chake.

  Kwahio, kwenye suala la umri kwa yeye Zitto Kabwe ni kwamba anataka kuwahi mno na hata hao wanaomshauri jambo hili wanafahamu hilo, lakini kwakuwa wanataka kukiharibia chama cha CHADEMA nafasi yake ya kukishinda chama cha CCM mwaka 2015 basi wanajaribu kutaka kuteka wanachama wasio na uzoefu na na siasa za Tanzania mmoja wao ni Zitto Kabwe. na kama hana uzoefu basi anao na anatumiwa ili kufanikisha azma hiyo.

  Pia kitendo cha yeye kutangaza nia ya kutaka uraisi pia ni ishara kwamba ama anatumiwa na kikundi cha watu au anajituma yeye mwenyewe kwa matakwa yake binafsi.

  Nawapongeza wazee wa CHADEMA ambao wameona jambo hilo mapema na kukaa kitako na kijana huyu mwenzetu kumuasa juu ya mwenendo wake.

  Mpaka sasa CHADEMA kimeonyesha juhudi kubwa katika kukikosoa chama tawala kiasi cha kutikisa mhimili wa chama hicho ambapo sasa kumefanywa mabadiliko ya baadhi ya viongozi waandamizi na kuwepo kwa mpasuko usioeleweka na kupelekea chama hicho kuanza kuandaaa mikakati ya kukidhibiti chama cha CHADEMA.

  Michezo michafu michafu katika siasa za Tanzania Mheshimiwa Kabwe anaifahamu, lakini ni lazima atambue kwamba kwa sasa hawezi kutumika au kujituma kutaka kutuchanganya sisi wananchi ambao tunapenda siasa za amani lakini zenye kuonyesha mabadiliko kwenye ngazi ya uongozi wana nchi.

  Jambo hili halikubaliki kabisa.
   
 2. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo mbowe na slaa tu ndio wanatakiwa kuzungumzia urais ndani ya chadema? Msikifanye chama hiki kaa KANU ya moi na kijana wake uhuru
   
 3. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  jaman enough with zito stuff aaaggghhhrrrr
   
 4. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Tusubiri kipindi cha campaign kifike!
   
 5. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Tusilinganishe siasa za Tanzania na za Kenya.

  Majirani zetu pamoja na siasa zao za kutupiana makonde bungeni utaona maendeleo ukifika Nairobi.
   
 6. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  we kama utaki hama chama
   
 7. peri

  peri JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  wamekimbia kwenye ule uzi wa kauli ya mtei baada ya kuona wameshindwa kumchafua zito.
  Kaja kuanzisha mada nyingine kutimiza malengo.

  Maswali rahisi ya kujiuliza, ni kipengele kipi cha katiba ya cdm ambacho zito amekikiuka?

  Mlimnyima asigombee uenyekiti, akakubali kwa maslahi ya chama, leo mnamnyima tena asigombee uraisi, demokrasia inayohubiriwa na cdm iko wapi?

  Kama mtei anakipenda chama na hataki mpasuko utokee, kwa nini anapingana na zito kwenye media na sio kwenye vikao halali vya chama?

  Mtei Anafanya hivyo kwa maslahi ya nani?

  Zito amesema ataomba idhini ya chama na asipo ruhusiwa atampigia kampeni mgombea atakae pitishwa na chama, huo ubinafsi hapo uko wapi?

  Mbona mnamuhofia sana zito, kwanini msiache demokrasia ifanye kazi yake?
   
 8. peri

  peri JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  mbona wewe umelinganisha siasa zetu na za uk na nchi nyingine kibao?

  Pili unashindwa kuielewa kenya, nairobi pako vizuri, tembelea maeneo mengine kama kaskazini karibu na somalia uone palivyo sahaulika.

  Tofauti na bongo, mikoa mingi haitofautini sana lakini kenya kuna tofauti kubwa sana kati ya nairobi na maeneo mengi ya nchi.
   
 9. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Zitto hana haja ya urais wala nini. Anafanya kazi aliyopewa na Usalama wa Taifa kuvuruga vyama vya upinzani. Zitto hajawahi kupigania maslahi ya nchi zaidi ya yake binafsi. Kwa tunaomjua, Zitto hana tofauti na akina Mrema, Seif, Mbatia, Kafulila, Cheyo, Kaboro na nyemelezi wengine wengi ambao watafanya lolote ili kupata tonge mdomoni. Hivyo, msihangaike na Zitto bali CCM ambao wamempandikiza hapo.
   
 10. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Kwa haya uliyoyasema hapo juu naweza kusema "you are part of the problem"

  Zitto kabwe alitangaza kuondoa nia yake hiyo kupitia vyombo vya habari likiwamo gazeti la Daily News mwaka 2009.

  Edwin Mtei pia ameelezea jambo hilo kupitia pia vyombo vya habari. Kwahio hawapingani kwenye media isipokuwa wanaitaarifu jamii baada ya kuzungumza ndani ya chama.

  Sasa tatizo liko wapi?
   
 11. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi binafsi napenda sana mabadiliko kama kijana, kwa staili anayotumia zitto kwa kisingizio cha demokrasia hizo ni vurugu na ni ulimbukeni wa kisiasa, na hii inatudhalilisha sisi vijana tu loose credibility mbele ya jamii kiujumla! Huwezi kutangaza nia mapema hivi hii ni kuhamisha concentration kwenye kuwaunganisha watanzania kuelekea kwenye ukombozi wa kweli! Kwa tabia kama hii ya zitto vijana tunaweza tusifanikiwe kwenye ukombozi wa taifa letu. Zitto ametoa maneno ya kuwabagua wazee kwa kusema eti anayefaa kuongoza taifa hili ni aliyezaliwa baada ya uhuru. , kauli hii itafanya asiungwe mkono na wazee na akina mama. Na wapongeza vijana kama january makamba.john mnyika nk.
   
 12. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Huu ujinga kabisa kwa sisi vijana kutumika kwenye siasa chafu.

  Lakini haya yote yangeondolewa endapo wapiga kura wangekipigia kura CHADEMA kwa wingi mwaka 2010.

  Pengine Zitto Kabwe angekuwa mmoja wa mawaziri wadogo kabisa kwenye baraza la mawaziri.

  Sasa kwa kuwa nafasi ikaja kupotea zikaanza hizi mbinu chafu.

  Hii ni hatari sana.
   
 13. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #13
  Oct 7, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Apendwe achukiwe... Akubalike asikubalike.. Kweli Zitto ana make 'headlines' inaelekea ana mvuto mzito sana kwa wasiompenda na wanaompenda. Kwamba whether you like it or not lazima umjadili...

  As if Zitto hajui yoote hayo ambayo umeongea? Hapo ndio wengi wanakosea (my IMO); You keep on underestimating him.
   
 14. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kutangaza nia si kosa tatizo kwa kijana mwenzetu zzk ni kutoangalia time, sasa ona ameanza jadiliwa mapema hii itapelekea wapinzani wake esp. Ccm kumaliza kisiasa mapema! Na ndo maana watu wana make Headlines!
   
 15. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #15
  Oct 7, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Ungonella kama hutajali naomba nikuulize, unadhani kuwa ZZK haelewi anachofanya?
   
 16. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haiwez ikawa enough kwa sababu zitto kijana mwenzetu amefanya kosa la kiufundi, unapotangaza nia mapema hivo una ruhusu watu wakujadili na unakuwa umefungia milango, pia wapinzani wake watammaliza mapema nje ya uwanja kisiasa esp. Ccm! Hilo litamgharimu kisiasa!
   
 17. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  zzk ni binadamu na si nabii au malaika inawezekana kwa fikra zake anafikiri yuko sahihi, lakini hilo ni kosa la kiufundi, siwez jua kama ana washauri au la!
   
 18. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #18
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona petition ya kumwondoa waziri mkuu alisimamia zzk? Ukweli uachwe tusipotoshe vyote!
   
 19. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #19
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Umeona ee! Kitu ukomavu wa kisiasa kwa pamoja ni vitu muhimu sana. Mwenye bongo linalofanya kazi sawa sawa hawezi kupigia debe katiba ya nchi ibadilishwe kwa ajili yake binafsi wakati waliowengi wanamshauri asubiri wakati ufika na katiba ikimruhusu umri kugombea.

  Urais upo, watu wanagombea na muda ukiisha mwingine atakalia kiti, tatizo ni nini kwa Zitto kusubiri mambo yote yawe yamekamilika ili aweze kupata fursa nzuri ambayo haitamletea utata?

  Kama mnakumbuka alianza ndoto za kugombea akiwa bado na umri chini ya miaka 30, maana yake miaka 10 kabla ya sheria au katiba inavyotaka. Haraka ya nini wakati bado kijana na muda ukifika atakuwa amejifunza na kupata uzoefu zaidi katika uongozi.
   
 20. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #20
  Oct 7, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Vitu ambavyo hujadiliwa sana mara nyingi huwa na pande nyingi sana za kuzielezea (in terms of schools of thoughts za makundi mbali mali); Inawezekana kauli yako ni kweli... Na pia inaweza kuwa sio kweli kutegemeana na mtazamo wa mwingine. Na hapo hapo kunaweza kuwa na mwingine na maelezo mengine kabisa...

  Hta hivyo nikichukulia kuwa kauli yako ni kweli (kitu ambacho siamini) then kwa kweli jamaa ni mbishi na haelewi somo. Nikiichukulia kuwa sio sahihi ndio pale pale tunaporudi kwenye post yangu ya kwanza kuwa anakuwa underestimated. Na huo ndio mtazamo wangu. Kuwa he knows exactly what he is doing na haya matokeo ya lawama, making headlines na mikanganyiko anaelewa kabisa nini anafanya na kwa nini...
   
Loading...