Mheshimiwa Waziri Mkuu Piga Maruufuku Viroba Kwanza Kabla Ya Shisha

Abu Hamdy

Member
Jun 27, 2016
29
17
Mheshimiwa Waziri Mkuu nashukuru sana kwa agizo lako la kupiga marufuku uvutaji wa Shisha, lakini ningekushauri Na Viroba vinafaa kupigwa marufuku pia kwani Viroba vimeleta maafa makubwa nchini kwa vijana na athari kubwa tumepoteza na tutaendelea kupoteza idadi kubwa ya vijana kwa matatizo ya (Liver Failure) jaribu kuwasiliana Na Wizara ya Afya ili upate idadi ya vijana waliopoteza maisha yao na vijana wanaotibiwa matatizo ya INI sababu ya Viroba.
Leo hii viroba vinauzwa madukani kama pipi na wenye maduka wanauzia vijana bila kujali umri, Serikali isipochukua hatua ya haraka tutapoteza kizazi cha vijana wetu.
 
Hiyo kweli na ukifika rombo Kilimanjaro ndo utajua kiroba kiboko hata ukimwambia kijana wa kirombo amfukuze kuku atakwambia we njoo kesho asbhi utamkuta lkn kwa mda huo ngumu
 
FAILURE..../
NADHANI VYOTE VIACHIWE VIENDELEE VISAJILIWE RASMI NA VIUZWE SEHEMU MAALUM/ SEREKALI IJIPATIE KIPATO CHAKE...../
~~HUWEZI ENDESHA NCHI KWA STAILI YA KAMA UNAENDESHA FAMILIA YAKO NYUMBANI KWAKO....
 
FAILURE..../
NADHANI VYOTE VIACHIWE VIENDELEE VISAJILIWE RASMI NA VIUZWE SEHEMU MAALUM/ SEREKALI IJIPATIE KIPATO CHAKE...../
~~HUWEZI ENDESHA NCHI KWA STAILI YA KAMA UNAENDESHA FAMILIA YAKO NYUMBANI KWAKO....
Maafa ya viroba haijakufikia ndio maana unaropoka ovyo ama una kiwanda cha viroba nyumbani kwenye. Hii Serikali ya Magufuli haitaji kodi ya viroba vyako kuendesha nchi.
Hapa tuna discuss athari za viroba
 
Pombe ya kiroba ni Kali sana kiukweli haina tofauti na spirit
Na bahati mbaya vijana wanatumia bila hata kuwa na kiasi

Mfano kuna siku tunaangalia mpira uku tunapata zetu soft drink akaja jamaa akakaa karibu yetu akaagiza pombe ya eagle pmj na viroba saba akawa anachanganya anakunywa

Sasa akiwa anafanya ivi kila Siku itakuwaje kiafya!

Viwanda vipunguze alcoholic ya viroba asee
 
Hapo point Si "Viroba"!!!! Point Ni Kuwa Pombe Za Aina Zote Zipigwe Marufuku Wasiangalie Gongo na Viroba tu,, Hapo itakuwa ni Kuwaonea Baadhi na Kuwaacha Baadhi.

Elewa Hakuna Kitu Kama Hichi Kusema "Ulevi Mzuri na Mbaya" "Pombe Halali na Pombe Haramu".

Ulevi Wowote ni Mbaya Hakuna Mzuri, Na Pombe Zote Ni Haramu Hakuna ya Halali.

Ni Ukumbusho tu wakuu....!
 
viroba tayari vimeshapigwa marufuku, pengine kuanzia mwakani havitoonekana mtaani.

tatizo sio viroba. tatizo ni sheria ya biashara ya vileo... maana siku hizi utakuta ht duka la kawaida vilevi vipo na vinauzwa muda wowote.

khs shisha, matumizi yataendelea kama kawaida... maana sheria inazuia madawa ya kulevya na bado vijana wanatumia, sembuse hiyo shisha ambayo sheria haisemi chochote..
 
•HAPA PANA MADHAIFU YA SHERIA.
-->>>POMBE KALI NA SOFT IWE NI MWIKO KUUZWA MADUKANI KOTE TANZANIA PAMOJA NA KWENYE STAND ZA DALADALA,
POMBE ZIUZWE KATIKA BAR PEKEE.licenced./
•KUUZA POMBE KILA PAHALA INACHANGIA WATU KUONA KWA KUWA INAPATIKANA TUNYWE TU.
•IWE NI KINYUME CHA SHERIA KUKUTWA UMELEWA MCHANA.
ADHABU IWE KIFUNGO AU FINE 50000/-.
 
Umesahau mabosi konyagi walienda mpk bungeni ili wabunge wasikataze konyagi ya pakiti wakasambaza dustbin kila bar. Hiyo kitu inaingiza faida kubwa sn sio rahisi kuifungia kirahisi.
 
Umesahau mabosi konyagi walienda mpk bungeni ili wabunge wasikataze konyagi ya pakiti wakasambaza dustbin kila bar. Hiyo kitu inaingiza faida kubwa sn sio rahisi kuifungia kirahisi.
Konyagi inauzwa hadi Marekani kwa sababu inatengenezwa kwa standard za kimataifa. Kiroba ni gongo iliohalalishwa na serikali. Naunga mkono hoja 100%
 
Back
Top Bottom