Mheshimiwa Spika Napenda kutoa Hoja!!!

Status
Not open for further replies.

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Sijui ndo uzee umeanza kuniingia au ndo nimepitwa na wakati... Kwa sababu fulani Spika Sitta anaanza kuliendesha Bunge utadhani kigenge.. ati leo amepiga marufuku neno "Kukazana" kwa sababu lina maana inayochanganya kijamii!! Kama ni hivyo si apige marufuku neno "Kutia", "Kulala", "Kuwekwa", "Kuchomeka", n.k

Sasa anaanza kuniudhi, kuna visheria na viutaratibu ambavyo vimepitwa na wakati na matumizi yake Bungeni yakome. Badala ya kujipatia umaarufu kwa kulazimisha mawaziri wajibu maswali na wabunge waulize maswali yenye mantiki ameng'ang'ani vitu ambavyo havina maana yoyote!! Badala ya kusubiri hadi wabunge waingie Bungeni ndo awatimue kwanini asiitishe kikao, au kusambaza kijarida kinachoelezea ni nguo zipi zaruhusiwa Bungeni, n.k badala ya kusubiri kuwadhalilisha wabunge!!?

I'm not impressed with the new Speaker!!! he's gettin on my last nerve! What is his problem anyway?
 
Mzee Mwanakijiji said:
Sijui ndo uzee umeanza kuniingia au ndo nimepitwa na wakati... Kwa sababu fulani Spika Sitta anaanza kuliendesha Bunge utadhani kigenge.. ati leo amepiga marufuku neno "Kukazana" kwa sababu lina maana inayochanganya kijamii!! Kama ni hivyo si apige marufuku neno "Kutia", "Kulala", "Kuwekwa", "Kuchomeka",......
I'm not impressed with the new Speaker!!! he's gettin on my last nerve! What is his problem anyway?

Nakubaliana nawe mwanakijiji,..miye nipo hoi, sijui yeye akili yake inakwenda wapi anaposikia neno kulala, kuwekwa, nk. ?? Nadhani inabidi tuhoji vitu anavyokuwa anafikiria akiwa bungeni.

Sasa utata wa hii sentensi ni nini?
Darhotwire.com said:
"...Mzee Ngwali Zubeir aliyeuliza kuwa pamoja na Wazanzibar kukazana katika elimu bado nafasi ni finyu kwa wanafunzi wa visiwa hivyo kupata nafasi katika vyuo vya Juu...."?
http://www.darhotwire.com/dar/Habari/2006/07/05/21297.html
 
Kinachoudhi ni kuwa wabunge na wenyewe wanacheka cheka tu na kukubali mambo!! Sitta siyo Rais wa Bunge na hawezi kujiamulia mambo y ake alimradi ana nyundo ya Uspika. Mbunge asimame amuulize Mhe. Spika maneno yote ambayo asingependa yatamkwe bungeni.
 
Kwa vile inaonekana Mhe. Spika ana muda mwingi wa kusikiliza maneno yanayotumika Bungeni kuliko maana yake na ana muda mwingi wa kusoma vikaratasi vya nani kavaa nini.. nimeona nijitolee kwa moyo wangu wa ukarimu kumpa somo la bure la Kiswahili na pia kutoa hoja ya kuwa kuna njia rahisi ya kuwashughulikia wale wanaovaa mavazi "yasiyoruhusiwa" bungeni.
 
Ndugu Mwanakijiji,

Nadhani kauli yako umeinza vibaya na huyu Mheshimiwa Spika wa Bunge hatafurahishwa hata kidogo kwani "UMEWEKA" oops umeandika KICHWA cha habari na kutumia neno "KUTOA", sidhani kama litapokelewa vizuri huko bungeni.....Nadhani utampandisha hasira au sijui yatampeleka wapi ........Yote inategemea akisoma hicho KICHWA cha habari yeye atafikiria nini!!

:lol: nadhani hata mimi bila kujua nishatumia maneno ambayo kwake Mh Spika atayaona si mazuri
 
Choveki,
Nilitaka kusimika hoja lakini naona mheshimiwa Spika atanishikia bango!
 
very funny Jasusi... "Kusimika" una maana ya kutia, kuchomeka, kuweka, kuingiza???
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom