Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja...

mcfm40

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,393
2,000
Ndugu Spika,

Kwa kuwa hakuna ugomvi kati ya Rwanda na Tanzania bali kuna ugomvi kati ya Kikwete na Kagame;
Na Kwa kuwa ugomvi huu umeanza kubadilishwa na kulazimishwa uwe ugomvi kati ya Tanzania na Rwanda;
Na kwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje ndio amekuwa mstari wa mbele wa kuchochea ugomvi huu kwa kuropoka ovyo badala ya kuutafutia utatuzi wa kidplomasia, badala yake anawashangilia wabunge wenzake wakati wakiiponda nchi jirani;
Na kwa kuwa watanzania hatutaki mgogoro huu uendelee na hatutaki kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, yasije yakatupata yale ya Kenya na Alshabab;
Na kwa kuwa uongozi wa Kikwete ukimaliza muda wake huu mgogoro ungeisha rasmi kwa sababu kimsingi upo baina ya watu wawili zaidi na sio nchi;
Na kwa kuwa Membe anataka kugombea urais wa tanzania mwakani;
Na kwa kuwa ikitokea Membe akipata urais wa JMT huu mgogoro utaendelea kutokana na matamshi yake ambayo amekuwa akiyatoa kuhusu Rwanda;

Natoa hoja kwamba kwa maslahi ya kurejesha uhusiano mzuri na majirani zetu hawa na kwa usalama wa Taifa Ndugu MHESHIMIWA BERNAD KAMILIUS MEMBE ASIRUHUSIWE KABISA KUGOMBEA URAIS WA NCHII HII KWA SASA.

Mheshimiwa Spika Anne Makinda, Naomba kutoa hoja!
 

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,939
2,000
Dawa za akili unatumia dawa gani mkuu,inaonekana hazikusaidii sana eeeeeeeeeee!
 

idoyo

JF-Expert Member
Jan 13, 2013
3,020
2,000
inaonekana ndiyoooo na siyoooo zimelingana, tutapiga kura ya siri!
katibu, kuhusu utaratibu
 

Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
inaonekana ndiyoooo na siyoooo zimelingana, tutapiga kura ya siri!
katibu, kuhusu utaratibu

Kuhusu Utaratibu,zitapigwa kura za siri na za wazi...................Haaaaaaaaaaahhhhhaaaaaaaaaaaaaaaaaa hapo ndipo penyewe.
 

mcfm40

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,393
2,000
Labda kuna mahali umemchanganya kama alivyofanya Halima Mdee leo kwa Professor wa Uchumi aka Waziri wa majumba na maghorofa.

Du ni kweli! Ila waziri mh mtoto mdogo km mdee anampelekesha puta vile! Prof. alivurugwa akakubali kuvurugika!
 

Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
Du ni kweli! Ila waziri mh mtoto mdogo km mdee anampelekesha puta vile! Prof. alivurugwa akakubali kuvurugika!

Ila nilimuonea huruma,alivyotoa macho na yale mawani utadhani kamjusi kadogo kamebanwa kwenye lango la kuingili mjengoni.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom