Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,013
- 144,371
Mheshimiwa Baba,wakati watu wanajiuzulu ili kuunga mkono juhudi, na kusababisha tuingie kwenye chaguzi za marudio, wako watu wengi walipaza sauti kupinga vitendo vile kwasababu mbalimbali mojawapo ni kuingiza Taifa hasara ya mabilioni kutokana na chaguzi katika maeneo/majimbo yao kurudiwa ili kujaza nafasi zao.
Wakati wazalendo mbalimbali wakipinga chaguzi zile,wewe mwenyewe na mashabiki wa chama chako, hatukuwahi kuwasikia mkikemea watu kujiuzulu ili tuokoea fedha za walipa kodi bali tulijibiwa hiyo ndio gharama ya demokrasia.
Sasa Mheshimiwa kwa hali hiyo, leo unapotaka watu wasijitokeza kuku-challenge ili kuokoa gharama,ina maana leo ndio umeguswa na gharama za uchaguzi na huko nyuma hukuguswa na gharama hizo?
Mheshimiwa, nini hasa unachoamini na kusimamia katika hili au labda wamekunukuu vibaya?