MHESHIMIWA RAIS WANANCH WAKO WA MKOA WA NJOMBE TUNAKUFA

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,255
1,563
MHESHIMIWA rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sisi wananch wa mkoa wa Njombe, tunatoa malalamiko kwako na waziri wako wa Wizara ya Ujenzi kwa kile tulichofanyiwa na mkuu wa mkoa bibi Rehema Nchimbi,
Mkoa wa Njombe ,wakazi wa mkoa huu tunategemea kilimo cha mazao yatokanayo na misitu kama chanzo cha kipato, tunategemea kilimo cha miti ambacho huzalisha mbao,nguzo,milunda na pia tunategemea viazi kama chanzo cha kipato chetu toka Tanzania imepata uhuru
Biashara hii hufanyika kwa kutoa mazao kutoka Lupembe,ludewa na makete kupeleka Dar Es salaam na mikoa mingine kwa njia ya gari kubwa(maarufu semi teller na vipisi)..
Wilaya zote za mkoa wa Iringa ambako mazao haya yanatoka na ndio uhai wa wananch barabara zake ni za vumbi.
Kwa kipindi chote toka tupate uhuru tumekuwa tukitumia barabara hizi kwa kuingiza gari kupakia mizigo huku tukilipia vibali maalum vya Tanroads,..
Msingi wa Tatizo, mnamo tarehe 26 /02/2016 mkuu wa mkoa alitoa siku tatu kuwa kila mkulima/ mfanyabiashara awe awe ametoa mazao yake shambani la sivyo atalazimika kusafirisha kwa kutumia canter au fuso mpaka ilipo lami ili aweze pakia kwenye semi teller au kipisi bila kuzingatia kuwa siku tatu nichache mno kwa mtu aliyekuwa na mizigo ya kutoa shambani kwa muda wa miezi mitatu, bila kuzingatia watu wana mikopo bank, bila kuzingatia kuwa kuna wakulima walikuwa wanaendelea kuchana mbao ambazo haiwezekani kuzitoa ndani ya siku tatu, bila kuzingatia wakulima tunatumia gari za kukodi kwa hiyo sio rahisi kupata gari ndani ya siku tatu,
Mheshimiwa rais mpaka naandika hapa tumefanya jitihada zote za kuongea na mkuu wa mkoa bila mafanikio na mazao yetu yanaoza piling,uchumi umesimama,
WATANZANIA WENZETU TUSAIDIENI TUWEZE KUTOA JAPO MAZAO YALIYOKWISHA VUNWA SHAMBANI
 
Tumieni viongozi wenu wa kiroho waweze kwenda kumuona na kumshawishi naamini atakubali, mbona nyerere alikubali pale alipofuatwa na kiongozi wa kidini kumuomba amuachie yule mzungu mlarushwa
 
Haya ndio malipo ya kuchagua wabunge wa ccm, sasa sie tukakusaidie vipi? Msaada wetu mliukataa mlipo amua kukumbatia ccm, endeleeni kulialia tu ipo siku mtasikika.
 
Eleza sababu za mkuu wa mkoa kutoa tamko hilo la siku tatu ninyi kutumia canter na sio semi au vips?
 
Back
Top Bottom