Mheshimiwa rais, umechuma janga. Gwajima sio DUDE ila George H.W. Bush ni DUDE

Mwenye Mada yuko sahihi, Ukitaka Kuwashinda Mapepari, tena Wenye Shadowy dealings, usiingie na Deal halafu baadaye Uwa double-cross. Wataona Umewadhulumu. CCM msijifanye kulia lia wakati mlishangilia kuingia Mikataba ya Kijambazi. Historia inaonyesha hakuna mtu anagusa Pesa, au Interest za Wamarekani Akachomoa. Wamarekani Mtukane Yesu atasema haimhusu, Mtukane Mama yake haimhusu. Gusa Pesa yake au Tukana Nchi yao, and Kiss your ass Goodbye! Wamarekani wana miungu miwili Pesa na National Pride, hivyo usiguse!
Kama wewe ni Mtanzania, je, national pride yako iko wapi?
 
Where is Hugo Chavez, Utawanyosha Marekani wewe! Ukitaka wakuone fair nenda nao kisheria, kisheria hapa Magufuli amelikoroga big time, Mmarekani sio wa Kumwambia, " Submit your passport now!, You bogus I will deal with you"
You seem to be eating from the same plate as those thieves. Sometimes i wonder whether some of you are really Tanzanians.
 
Kama Mh Rais Magufuli kweli atakuwa na dhamira na nia ya kupambana na wanyonyaji na matapeli wanaofilisi rasilimali zetu kama madini na gesi tutasimama naye na pia Mwenyezi Mungu atamlinda. Lakini akileta mambo ya siasa na partisan issues kama siku za nyuma, hatutafanikiwa.

Umoja wa wananchi wa Tanzania ni muhimu sana, kwani kama hatutaungana na kuunganishwa na Utaifa wetu badala yake siasa na ukada vikaingizwa tutakwama kwa hasara yetu wenyewe.
 
kwahiyo tuendelee kuibiwa tu some time tusikae tu na kuanza kupinga hata ukweli jamaa yukoi sahh kabisa bushi co mungu km unamuogopa unamuogopa ww na ndgzako
:rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes:
 
Hakuna Mtanzania mzalendo anayeunga mkono huu wizi bali tunashauri umakini wa hali ya juu kwenye kushughulika na hawa watu. Tukibugi step madhara yake ni makubwa kiasi cha kugharimu vizazi na vizazi. Mungu ibariki Tanzania.
 
Kuna wakati inabidi uvuke highway ukiwa umefumba macho hata hama unasikia muungurumo.....
 
Watanzania mpo radhi mpigane vita wenyewe kwa wenywe lkn sio kupigania mali zenu
 
Ukikufika sehemu wasomi wanadharaulika na mbumbumbu wanasifiwa jua hakuna maendeleo bali majungu, fitna na ububusa mtupu pita nenda zako.
 
Pamoja na ujambazi na ukibaka wooote huo marekani inazidi kuwa dhaifu siku mpaka baada ya siku

Lazima waafrika tudhibiti vitu vyeti visiibiwe, kwa kufanya hivi si tu kwamba tutalinda utu na heshima yetu bali pia tutalinda mustakabali wetu na vizazi vyeti

Wazungu wanapofanikiwa kutuibia au kututapeli ndio wanazidisha dharau dhidi yetu, uafrika wetu

Tupate mapato yanayostahili, na si kwa matakwa ya bushi
 
Mleta nyuzi,wewe ni mtumwa wa kifikra.
118377_004_1F256C6E.jpg

Ramani ya kulia kwako kwenye kijani ndipo wanapo patafuta usiku na mchana.
 
Mchuma janga hula na wakwao! Na tutakula wote tu, hamna ujanja.
Sasa kwakuwa umechokoza li dege lililotulia, sasa na wewe utulie tuli usikie sauti yake.

George H.W Bush anahusikaje na Acacia?

Nov.27,2014 Cecilia Jamasmie anaandika ,'African Barrick imebaki historia, imebadili jina kuwa Acacia mining.'
Moja kati ya malengo yake ilikuwa kuendeleza kazi zake North Mara na kuzalisha ounce 450,000 ndani ya miaka mitano kwa gharama ya chini ya dola 750 kwa ounce.

Jan.03,1997 Anton Chaitkin anaandika Inside story juu ya genge la Bush na Barrick Gold Corporation. Anasema;
☆ Barrick Gold ni shirika linalojihusisha na mikakati ya siri katika siasa za George H W Bush.
☆ Shirika hili lenye makao yake Canada ndio biashara pekee ya Bush iliyofahamika wakati huo.
☆ Shirika hili lilianzishwa na marafiki wa kisiasa wa Bush, Wawezeshaji wakubwa wa biashara za madawa ya kulevya, wafanyabiashara haramu wa silaha na watakatishaji wa fedha.
☆ Shirika ni kubwa, liko USA, Canada, South America: Argentina, Chile, Peru, Bolivia na Brazil. Lipo pia Africa.

Majina makubwa kwenye shirika ni ya kina nani?

1. George Herbert Walker Bush
Baba yake alikuwa partner kwenye taasisi binafsi kubwa na yenye nguvu, ya kibenki - Brown Brothers Harriman.
Bush alikuwa makamu wa rais na chief kwenye operations za siri katika utawala wa Reagan (1981-89).
Bush alikuwa rais wa Marekani (1989-93).
Bush alikuwa chief lobbyist wa Barrick, mwanahisa na mshauri mkubwa wa heshima wa bodi ya kimataifa ya washauri wa Barrick.

2. Adnan Khashogi.
Billionea wa saudi na mfanyabiashara haramu ya silaha .
Muanzilishi wa Barrick Gold Corp.
Maarufu sana kwa biashara yake haramu ya kuiuzia Iran silaha.

3. Peter Munk na 4. Brian Mulroney ; hawa ntawaacha kwa sasa.

Hili ni janga kwasababu kwao Magufuli hatoshi hata kwa breakfast;
Angalia hapa chini!

$ Uwekezaji mkubwa katika shirika ulifanywa na Khashogi na mapartner wake katika biashara haramu ya silaha. Wakati huo wakihangaika na biashara iliyojulikana kama 'guns and cocaine triangle' kati ya Iran - Israeli - na Nicaragua. 1986 biashara hii ilikuja kubumburuka na ikawa maarufu kama 'Iran - contra' scandal.

$ Bush na yeye aliingia kwenye shirika kwa staili yake. Mwaka 1986-87 Barrick Gold Corp ilinunua ardhi, mali ya serikali ya Marekani, yenye thamani ya zaidi ya dola billion 10 kwa dola million 63 tu, kwaajili ya uchimbaji wa dhahabu.
Hapa ni USA ukumbuke, na sio mandazi republic kama hii yakwetu.
Bush alipochaguliwa 1988 akawezesha utaratibu wa kupata hati miliki kwa ajili ya eneo hili.Utaratibu huu ulikuwa special kwaajili ya Barrick tu!

♀Bush alishirikiana bega kwa bega na CIA na FBI katika kujaribu kupindua Serikali ya Fidel Castro katika uvamizi uliopewa jina maarufu kama Bay of Pigs invasion.
Walitumia mgongo wa kampuni ya Zapata Oil Bush akiwa kama rais wa kampuni na baadae Zapata Offshore Bush akiwa kama mmiliki.
Hapa kuna Memo kibao za ushahidi.

Nov.22, 1963 Bush alishiriki katika mauaji ya J.F.Kennedy, rais wa Marekani wakati huo kwasababu tu alikataza ndege za Marekani kutumika kwenye Bay of Pigs invasion. Kennedy pia alistopisha rogue operations zote za CIA na FBI .

Bush amefanya maovu mengi mno! Ana links na shetani wa kila aina;
☞ wa Nazi.
☞ wafanyabiashara ya madawa ya kulevya.
☞ Wafanyabiashara haramu ya silaha.
☞ Wauaji - assassins
☞ CIA
☞ FBI
☞ Na taasisi nyingi za kijeshi sehemu mbalimbali ulimwenguni.
Bush hajazaliwa hapo chini ya mfereji kwamba unaweza kumtumbua hata ukiwa grocery!

Kwenye moja ya mkutano mkuu wa umoja wa mataifa, siku moja baada ya Bush kuhutubia, Marehemu Hugo Chavez, Mungu ailaze roho yake mahali pema, Anasema, “ Shetani alikuja hapa jana, na mpaka leo hii, hii meza niliposimama inanuka sulfur.” Kisha Chavez akapiga ishara ya msalaba halafu akaangalia juu akiweka mikono yake kama mtu anayesali kumuomba Mungu.

Mdau unajua kwanini Chavez aliongelea harufu ya sulfur?
Bush unayemuongelea kwa mambo ya madini ni Bush Sr, baba yao. Bush wa Hugo Chaves Jr, ni mtoto.
 
Kwenye moja ya mkutano mkuu wa umoja wa mataifa, siku moja baada ya Bush kuhutubia, Marehemu Hugo Chavez, Mungu ailaze roho yake mahali pema, Anasema, “ Shetani alikuja hapa jana, na mpaka leo hii, hii meza niliposimama inanuka sulfur.” Kisha Chavez akapiga ishara ya msalaba halafu akaangalia juu akiweka mikono yake kama mtu anayesali kumuomba Mungu.

Mdau unajua kwanini Chavez aliongelea harufu ya sulfur?
Alazwe Pema Hugo Chaves Frias (Mtume na Nabii)
 
Kweli Bongo tuna Mapoyoyo wengi sana. Yaani lijitu linatoa povu kutetea wezi? Wanaotuibia kama taifa.
 
Jpm kashalianzisha ni haki yake na kwa Taifa letu piya. Acha kuogopa jambo usilolijua siasa za dunia sasa hivi zimebadilika hao kina Bush wameshazeeka siyo kama kipindi kile. Now ni era ya kina Trump, JPM et al... ambao wao hufanya mambo yale walio watangulia waliogopa kuyagusia.

Kwa maoni yangu namuunga mkono JPM kwa uamuzi wake wewe tulia hiyo tume nyingine inayoendelea na kazi nayo iwasilishe ripoti yake ili tujue the way forward.

Mkuu Paul Alex punguza woga kumbuka uko nchini kwao na siyo Ukimbizini nje ya nchi. Acha mchezo uendelee na safari hii ushindi ni wetu kwenye mechi hii ngumu na ya kimataifa.
Ndio maana JPM haachi kuwaasa wananchi wake tumuombee kwa Mungu kwani anajua amejitoa muhanga kwa nchi yake kwenye vita ambayo maraisi wengi wa nchi za Ulimwengu huu imewashinda.
 
Bush unayemuongelea kwa mambo ya madini ni Bush Sr, baba yao. Bush wa Hugo Chaves Jr, ni mtoto.
Hata mimi niliona hili nikataka kusema lakini nikaona labda nitakuwa nina nitpick.

Mtu anaandika kiintelijensia halafu anatuchanganyia George H.W Bush (baba) na George W. Bush (mtoto).

Ananipa shakakama amefanya uchambuzi wa kina katika habari zake.

Hapa kitu kikubwa cha kuhofia zaidi ya hao kina Bush ni hawa viongozi wetu waliosaini mikataba mibovu, wamesaini London huko ambako arbitration courts ziko biased kutetea wawekezaji hata kwenye mkataba fair, na sisi mikataba yetu si fair kwa sababu hatuna wataam wa mikataba na pia viongozi waliosaini wamehongwa hela.

Magufuli alikuwa wapi wakati mikataba inapitishwa/

Waliopitishwa mikataba watachukuliwa hatua gani?
 
PAUL ALEX , Naomba usiendelee na hiyo stori utaleta HOFU nchini ngoja tusubiri repoti ya mwisho.
 
Back
Top Bottom