Mheshimiwa Rais uanzishwaji wa viwanda, uendane na suala la uwezeshaji wa Wajasiramali pia tafadhali

Uso wa nyoka

JF-Expert Member
Mar 17, 2014
4,791
2,372
Nafurahi kusema kwamba, mwelekeo wa Rais katika maamuzi mengi una viashiria chanya zaidi kuliko hasi, hasa kwa sisi wengi tunaoona mbali. Sizungumzi kwa niaba ya wale wenzetu wachache ambao kwao, jema huwa wanapendelea lionekane baya na lile baya liwe baya zaidi. Hapa nazungumzia wale walio na mtazamo wa kimaendeleo ulio na makusudio ya kulifanya taifa letu kuwa mahala ambapo unafuu na maendeleo ndiyo kwake kama mataifa mengine ambayo yamefikia kuitwa ya uchumi wa kati n.k

Wakati huu wa vuguvugu la mwamko wa kiuchumi nchini ambalo tumeliita zama za viwanda, ni wakati mwafaka sasa wa kuangalia njia mbadala zitakazoweza kutufikisha kule tunakoelekea. Nasema hivi kwa sababu, ni wajasiriamali wachache walio na uwezo na rasilimali za kuwasaidia kushiriki katika juhudi za kulifanya taifa letu liendelee kwa viwango tunavyotaka, hasa kwa kuwa wengi kati yao ni wale walio na uchumi mdogo ama wa kati unaowawezesha kumudu baadhi ya gharama za kimaisha za kila siku na pengine nyongeza ya biashara ndogondogo ambazo hazihitaji uwekezaji mkubwa.
Tulio na mtazamo mpana tunajua mtazamo wa Rais na malengo mema aliyonayo. Hii ni kwa sababu fursa zinaoneakana wazi kuanzia katika uwekezaji katika mazao ya kilimo na ufugaji, vifaa vinavyotumika kila siku majumbani na hata katika maeneo mengine ambayo ni promising kama uchakataji na usindikaji , mazao ya misitu, mazao ya bahari na hata ushiriki katika miradi mikubwa n.k

Nilifurahi sana kusikia mapendekezo ya Rais ya kutaka vianzishwe viwanda vya madawa hapa kwetu ili viwe mbadala wa vyanzo vinavyogharimu pesa nyingi na milolongo mirefu katika uagizaji n.k. Ni kati ya mambo ambayo Rais amegusa mahala panapostahili kwa wakati mwafaka. Rais unaonaje hilo wazo ukiliextend hadi katika sekta zingine? Wezesha wajasiriamali wazalendo walio na shughuli katika maeneo mbalimbali ili wakuze na kupanua wigo wa uzalishaji wanaoufanya katika maeneo yao ya kiuwekezaji kwa kupitia mikopo nafuu ambayo itasimamiwa na Wizara husika ili wapate nguvu ya kiuchumi ya kushindana. Mjasiriamali apewe mtaji tuseme kama ni wa kiwanda cha kutengeneza cheese au sausages ambao wizara itausimamia kwa muda hadi ule mtaji utakaporudi na kumwacha aendelee. Itakuwa ngumu mwanzoni lakini naamini itasaidia wengi. Serikali isitoe fedha mikononi, bali ishiriki katika kutatua changamoto za wajasiriamali katika maswala kama ununuzi wa mitambo, uboreshaji wa uzalishaji na kugawa ujuzi kwa kukabidhi majukumu kwa wizara husika kupitia utaratibu maalum utakaoziwesha kudhibiti na kusimamia mitaji inayotolewa kupitia wizara husika.

Ningependa kusema kuwa, maono ya nchi ya viwanda, ni jambo linalowezekana na tunakokwenda ni kuzuri kuliko tulikotoka ingawa kuna ugumu tutakaokutana nao mwanzoni. Rais endeleza hizo juhudi na usiziache. Walio na mawazo ya msingi karibuni kuchangia, mnaojiandaa na milalamo, sina la kuwaambia.
 
Back
Top Bottom